Watanzania wametakiwa
kuhamasika na kufahamu umuhimu wa utumiaji wa dawa za uzazi wa mpango ili
kuondokana na changamoto mbalimbali katika afya ya uzazi.
Meneja miradi wa afya
ya mama na mtoto kutoka shirika la Amref Heath Africa, Dkt Serafina Mkuwa
amebainisha hayo leo jijini Dar es salaam wakati wauzinduzi wa mradi wa afya ya
uzazi na mtoto wa Health System advocacy project wenye lengo la kuhamasisha
uwepo na upatikanaji wa dawa za uzazi wa mpango.
Dkt.Mkuwa amesema vifo
vinavyosababishwa na afya ya uzazi wastani wake kwa akina mama ni 556 ambao
wanafariki kwa mwaka katika kila vizazi laki moja.
Dkt.Mkuwa ameeleza
sababu zinazosabasha watoto na kina mama kupoteza maisha kwa wingi kuwa ni
pamoja na kutozingatia matumizi bora za utumiaji wa dawa za uzazi wa mpango.
Mkurugenzi wa Tanzania Youth Alliance (TAYOA) Peter Masika aliyevaa koti jeusi akizungumza na wanahabari
Kwa Upande wake Mkurugenzi
wa Tanzania Youth Alliance (TAYOA) Peter Masika amesema ili kuepukana na mimba
za utotoni ni vyema vijana wakahakikisha wanakuwa na malengo kwenye maisha yao.
Post a Comment