Halloween party ideas 2015
Image

Na Isssa Ramadhani,
BAMIAI watu wengi wanadharau ule unyonge wa hii mboga basi ni duniani  haina msaada wowote katika matumizi ya kila siku,miili yetu sasa zitambue siri na umuhimu wa mboga ya bamia  nyingi  wewe unazoziona dhaifu kifikra zako ima kwa bei yake au muonekano wake mboga hiyo kuanzia sasa iangalie kwa jicho la tatu .huenda ikawa ndio mkombozi wa mwisho katika shida yako ya kimwili, sasa ni wakati wa kula  bamia kila siku waweza kutumia kwa kuchemsha, kuitafuna kila siku.

BAMIA;
Bamia ni chanzo kizuri cha Vitamin A na Beta Carotene ambavyo ni virutubisho vinavyosaidia kuboresha uwezo wa kuona.
Bamia inasaidia kuweka kawaida kiwango cha sukari mwilini na nyuzinyuzi(fibers) zake zinasaidia kurahisisha ufyonzwaji wa sukari mwilini.
Michirizi na utomvu unaopatikana katika bamia mara nyigi, husaidia kusawazisha  na kuweka sukari mwilini hasa  kwa wagonjwa wa kisukari kwa kuzuia kiwango cha sukari mwilini inayotumika katika mwili ili kutoka kwenye utumbo mkubwa.
Pia hudhibiti kiwango cha lehemu mwilini na hasa pale ambapo  inapokuwa mtu ametumia vyakula vingi vyenye mafuta.Hivyo  husaidia pia kulainisha choo.
Alikadhalika  bamia ni mboga ambayo hutumka  kwa Waafrika pia huongeza hamu ya kula na hata kurahisisha kazi ya kumeza chakula.
Wataalamu  wanaeleza kuwa bamia  ina wigi wa  virutubisho ambavyo  vinavyoweza kupambana na bakteria wanaoshambulia utumbo na kusababisha vidonda vya tumbo.
Pamoja na haya yote bamia huimarisha mifupa, huongeza kinga dhidi ya magonjwa ya figo, saratani pamoja na pumu. Utelezi wake huchuja uchafu unaoingia katika Kolestorali Cholesterol na asidi ya nyongo unaoingia kutoka kwenye ini ambao usipodhibitiwa huenda ukasababisha matatizo ya kiafya kwa binadamu.
Bamia husaidia kulainisha utumbo mkubwa Large Intestines kutokana na kazi yake ya kulainisha choo hivyo huzuia kufunga choo.

Bamia ina Vitamin C ambayo inawafanya watoto wanaougua ugonjwa wa pumu kupumua vizuri wanapoitumia. Nusu kikombe ya bamia iliyopikwa huwa na miligramu 13 ya vitamin C.
Bamia husaidia kuweka utumbo kuwa na hali nzuri kwa mtumiaji  hivyo kupunguza uwezakano wa kuugua ugonjwa wa kansa hasa kwenye utumbo mkubwa. Pia kula bamia kwa wingi kunasaidia kuimarisha mishipa midogo ya damu.
Nusu kikombe cha bamia iliyopikwa inakua na kiwango cha 460 IU ya vitamin A ambayo inapunguza uwezakano wa kupata ugonjwa wa mtoto wa jicho Cataracts
FAIDA ZA BAMIA NI HIZI ZIFUATAZO;
1. Inapunguza kolestrol mwilini na inasaidia kuondoa vimelea
vya sumu kwenye ngozi.

3. Inasaidia katika kutibu. magonjwa mbalimbali ya
zinaa kama vile kaswende, kisonono

4. Vilevile inaponya tatizo la kwenda hedhi mara kwa
mara na chango la kike

5. Inasaidia kutibu pumu(asthma)

6. Inaongeza kinga ya mwili

7. Ina utajiri mkubwa wa  Virutibisho aina ya fibre

8. Ina utajiri mkubwa wa virutubisho mwili aina ya
protini ( hamirojo ) . Ina saidia kuimarisha afya
ya nywele


10. Inasaidia. kupambana na tatizo la
uchovu wa mwili, na msongo
wa mawazo

1. Inasaidia kutibu tatizo la kukosa choo

12. Inawasaidia wanao sumbuliwa na tatizo la kisukari

13. Inasaidia kusafisha damu

14. Inasaidia kuponya mafua

15. Inasaidia kuondao sumu mwilini

16. Inasaidia kutibu vidonda vya tumbo

17. Inasaidia  kikinga tatizo la anemia


18. Ina kinga dhidi  ya utapia mlo(unene uliopitiliza)



19. Inasaidia kuimarisha mifupa



20. Inasaidia  kuimarisha mfumo wa uonaji






JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.wabunifumedia.blogspot.com ku-install App ya wabunifumedia,  bila ya kuingia websiteTweet@wabunifumediaonline, youtube@wabunifumediaonline TV, Fb@wabunifumediaonline, insta@wabunifumediaonline



Post a Comment

Theme images by Maliketh. Powered by Blogger.