Halloween party ideas 2015
Showing posts with label Habari. Show all posts




Na Zephania Kapaya

Watanzania wametakiwa kuhudhuria semina ya ufunguzi wa onesho la chimbuko la Binadamu wa Afrika  ikiwa ni onesho na matokeo ya tafiti mbalimbali zilizofanyika bonde la Olduvai na Laetoti hifadhi ya mamlaka ya Ngorongoro.

Hayo yamesemwa na Prof.Audax Mabula ambaye ni mkurugenzi wa Makumbusho Taifa ambapo ameekeza kuwa  Makumbusho ya ya Taifa ikishirikiana na ubalozi wa Spain Tanzania,Makumbusho ya Aikolojia ya Madrid,Taasisi ya chimbuko la Binadamu(IDEA) Madrid,Chuo kikuu cha Acla Madrid na Makumbusho ya Cosmocaixa Barcelona- Spain na kampuni ya siment ndio waliondaa onesho hilo wakiwa na lengo la kuwaonesha na kuwafunza watu mbalimbali kuhusiana na chimbuko la Binadamu Afrika.

Aidha Prof.Mabula amesema mgeni rasmi katika onesho hilo ni Waziri wa Maliasili na Utalii Dr Hamis Kigwangwalla na litazinduliwa saa 11:00 jioni Makumbusho ya Taifa jijini dar es salaam na wageni mbalimbali wanatariwa kuwepo wakiwamo Mabalozi,wananchi,na viongozi mbakimbali.

Prof.Mabula ameendelea kwa kusema kuwa vionyeshwa vyote katika onesho hilo vimepatikana hapa Tanzania kutokana na tafiti za kisayansi na vimehifadhiwa Makumbusho ya Taifa vioneshwa hivo ni pamoja na Masalia ya Zamadamu,Zana za Mawe na Masalia ya Wanyama walioishi takribani tangu milioni 4 iliyopita.

Prof Mabula amemaliza kwa kuwataka wananchi wote kuhudhuria kwa wingi  katika onesho hilo pamoja na semina kwani hakuna kiingilio na kwa siku ya pili kiingilio kwa MTU mzma ni shilingi 1500,mtoto ni shilingi500.
IMG-20171210-WA0045
Na Christina Mwagala
 MSTAHIKI Meya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita ameondoka Jijini hapa jana jioni kuelekea  Addis Ababa, kuhudhuria mkutano wa kujadili changamoto zinazo wakabili viongozi wa serikali za mitaa.
Mkutano huo wa siku tatu umeandaliwa na Umoja wa Mataifa ambapo unalengo la kujadili na kutoa majibu ya changamoto ambazo wanakutana nazo viongozi wa serikali za mitaa wakiwepo Mameya wote.
Miongoni mwa changamoto ambazo zitajadiliwa katika mkutamo huo pamoja na mambo mengine ni  suala la bajeti katika halmashauri na ukusaji wa mapato.
Mbali na Mameya ,mkutano huo pia utahudhuriwa na viongozi wengine wa serikali za mitaa kutoka Nchi mbalimbali.
Aidha Meya Mwita atazungumza na mkutano huo kuelezea changamoto zilizopo katika jiji la Dar es Salaam , namna ambavyo  kwa asilimia kadhaa wameweza kuzitatua.
Aidha katika mkutano huo ataeleza pia mafanikio yaliyopo katika jiji la Dar es Salaam kupitia sekta mbalimbali za Maendeleo.
” Katika mkutano huo hatuta kuwa jiji la Dar es Salaam pekee ,ni Nchi mbalimbali Duniani zitakuwepo, tutajadili changamoto zinazo tukabili kwenye halmshauri zetu, mafanikio,lakini pia kujengeana uwezo kwenye utendaji kazi” alisema Meya Mwita.

Imetolewa leo Desemba 11
Na Christina Mwagala , Afisa Habari Ofisi ya Mstahiki Meya wa jiji

Picha-no.-5-1

Na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete
 Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na Taasisi ya Okoa Moyo wa Mtoto (Save a Child’s  Heart – SACH) ya nchini Israel zimewapeleka  watoto sita (6) wenye umri wa mwaka mmoja hadi  miaka kumi na tatu  nchini Israel kwa ajili ya matibabu ya moyo.

Katika safari yao ya matibabu nchini humo watoto, wauguzi pamoja na wazazi wao wameondoka alfajiri ya jana tarehe  10/12/12. Baada ya matibabu ya watoto kukamilika  Maafisa Wauguzi wawili watabaki kwa ajili ya kuhudhuria mafunzo ya mwaka mmoja ya jinsi ya kuwahudumia wagonjwa waliopo katika wodi ya uangalizi maalum (ICU) na chumba cha upasuaji.

Taasisi  yetu inatibu magonjwa mbalimbali ya moyo kwa watoto  kupitia  wataalamu wazalendo tulionao. Hata hivyo tunamkataba na Israel kwa baadhi ya wagonjwa wachache wanaohitaji utaalamu wa juu zaidi kuwapeleka nchini humo kwa ajili ya matibabu.

Tunaushirikiano mzuri na nchi ya Israel kwani gharama za matibabu ya watoto hawa zinagharamiwa na SACH. Licha ya Maafisa Wauguzi wawili kubaki nchini humo kwa ajili ya kuhudhuria mafunzo pia tuna madaktari bingwa wa magonjwa ya moyo sita   na wauguzi wawili ambao wamesoma nchini Israel na hivi sasa wanatibu wagonjwa katika Taasisi yetu.Aidha Daktari wetu mmoja bado anaendelea na masomo nchini humo.

Hili ni kundi la tano  la watoto kwenda kutibiwa magonjwa ya moyo nchini Israel tangu mwaka 2015 ambapo Taasisi ya Moyo ilianza ushirikiano  na Taasisi ya Okoa Moyo wa Mtoto (Save a Child’s Heart –SACH)  ya kuwapeleka wagonjwa nchini humo. Hadi sasa watoto 46 wameshatibiwa nchini humo na wanaendelea vizuri.

Taasisi inaendelea kutoa wito kwa wazazi na walezi wasisahau kupima afya za watoto wao pale watakapoona kuna hali ya tofauti katika ukuaji wa mtoto kwani magonjwa mengi ya moyo yanaanzia utotoni. Mtoto akianza kuuguwa magonjwa ya moyo wazazi wengi wanadhani ni matatizo ya kifua baada ya kumfikisha mtoto Hospitali na kufanyiwa vipimo  ndipo inagundulikwa kuwa mtoto anasumbuliwa na magonjwa ya moyo.

Imetolewa na :

Kitengo cha Uhusiano na Masoko
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete
11/12/2017

Na Mwandishi wetu
……………………………………………………..
Wadau wa Utalii Jijini
Arusha wamempongeza Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla kwa
kukubali kuyafanyia kazi mapendekezo yao ya kuwaingiza wajasiriamali wadogo katika
utoaji wa huduma za kusafirisha watalii nchini.
Kauli hiyo imetolewa
jana na
Mwenyekiti wa Chama cha Waongoza
Watalii Tanzania (TATO), Wilbard 
Chambulo wakati akichangia
mapendekezo ya viwango vipya vya leseni za biashara ya utalii zilizowasilishwa
kwao na Uongozi wa Wizara ya Maliasili na Utalii Jijini humo.
Chambulo
alisema kwa muda mrefu sasa kanuni zinazotumika zinamtaka mfanyabiashara ya
usafirishaji watalii awe na magari matatu kwa kiwango cha chini ikiwa ni pamoja
na kulipia ada ya leseni ya Dola za Kimarekani 2,000 sawa na wafanyabiashara
wengine matajiri 
jambo ambalo limekuwa likiwabagua wafanyabiashara wadogo.
“Tunakupongeza
sana Mhe. Waziri kwa kutupa angalao hilo moja, tuliomba mwenye kagari kamoja nae
aruhusiwe na apewe leseni walau ya dola 200 ili afanye biashara kidogo kidogo
mwishowe atanunua gari tano na kuendelea, tunataka sisi Watanzania wote tufaidike
na rasilimali zetu,” alisema Chambulo.
Awali
akiwasilisha mapendekezo ya viwango hivyo vipya vya leseni ya biashara ya
utalii, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utalii, Wizara ya Maliasili na Utalii,
Deogratias Mdamu alisema kwa upande wa watanzania ambao ni wajasiriamali wadogo
wenye gari moja hadi magari matatu watatakiwa kulipa ada ya leseni ya dola za
Kimarekani 200.
Kwa upande
wa wafanyabiashara wenye magari kuanzia manne hadi kumi alisema imependekezwa walipe
Dola za Kimarekani 2,000, wenye magari 11 hadi 50 Dola za Kimarekani 3,000,
magari 51 hadi 100 Dola za Kimarekani 10,000 na magari 100 na kuendelea Dola za
Kimarekani 15,000.
Kwa upande
wa wafanyabiashara ambao sio Watanzania wenye magari 10 hadi 30 imependekezwa
walipe Dola za Kimarekani 10,000, magari 31 hadi 100 Dola za Kimarekani 15,000
na magari 101 na kuendelea Dola za Kimarekani 20,000.
Kwa upande
wake Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla alisema lengo la
kuwasilishwa kwa mapendekezo hayo ya viwango hivyo vipya vya leseni ya biashara
ya utalii kwa wadau ni kuweka ushirikishwaji na makubaliano ya pamoja ya
kutekeleza kanuni hizo.
Alisema sehemu
kubwa ya mapendekezo hayo imezingatia maombi na maoni ya wadau hao ambayo
yaliwasilishwa kwake awali. “Kilio chenu nimekisikia mimi mwenye mamlaka ya kufanya mabadiliko, lengo kubwa la mapendekezo haya ni kuwawezesha wajasiriamali
wadogo wenye gari moja waweze kuingia kwenye biashara hii ya utalii pamoja na
kuongeza mapato ya Serikali na jamii kwa ujumla,” alisema Dk. Kigwangalla.
Katika
hatua nyingine amewaagiza watalaamu ndani ya Wizara yake kuhakikisha
wanakamilisha kanuni hizo mpya ndani ya mwa mwaka huu ili utekelezaji wake
uanze mapema mwakani, 2018.
Akizungumzia
wafanyabiashara wanaofanya biashara ya kuwasafirisha watalii nyuma ya pazia
bila kulipia leseni, alisema Wizara yake inaandaa mfumo maalumu wa
kielektroniki utakaowezesha ukaguzi wa magari kwenye mageti ya kuingilia hifadhini
ili kudhibiti vitendo hivyo.

Aidha,
ametoa onyo kali kwa wafanyabiashara hao na kuwataka kufanya biashara hiyo kwa
weledi na kuzingatia kanuni na taratibu zilizowekwa ikiwemo kulipa ada ya leseni
husika kwa mujibu wa sheria. 
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla (kulia) akizungumza na wadau wa utalii
Jijini Arusha jana ambapo Wizara yake iliwasilisha mapendekezo ya viwango vipya
vya leseni za biashara ya utalii na tozo ya ada za malazi katika viwango vya
ubora wa nyota. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii,
Dk. Aloyce Nzuki. 
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza na wadau wa utalii
Jijini Arusha jana ambapo Wizara yake iliwasilisha mapendekezo ya viwango vipya
vya leseni za biashara ya utalii na tozo ya ada za malazi katika viwango vya
ubora wa nyota. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Dk.
Aloyce Nzuki na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utalii, Wizara ya Maliasili na
Utalii, Deogratias Mdamu (kushoto).
Baadhi ya
viongozi wa Wizara ya Maliasili na Utalii na Taasisi zilizopo chini ya Wizara
hiyo wakiwa kwenye mkutano huo.
 Baadhi ya viongozi wa Wizara ya Maliasili na Utalii na Taasisi zilizopo chini ya Wizara hiyo wakiwa kwenye mkutano huo.
 Baadhi ya
wadau wa Utalii walioshiriki mkutano huo.
Mwenyekiti wa Chama cha Waongoza Watalii Tanzania (TATO),
Wilbard 
Chambulo
akichangia mapendekezo ya viwango vipya vya leseni za biashara ya utalii zilizowasilishwa
kwao na Uongozi wa Wizara ya Maliasili na Utalii katika mkutano huo.
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla (kulia) akitambulishwa na Naibu
Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Dk. Aloyce Nzuki (kushoto) kwa Mjumbe
wa Bodi ya Wadhamini ya
Chama cha Waongoza Watalii Tanzania (TATO), Merywn Nunes muda mfupi baada ya
kikao na wadau wa utalii Jijini Arusha jana ambapo Wizara yake iliwasilisha mapendekezo
ya viwango vipya vya leseni za biashara ya utalii na tozo ya ada za malazi
katika viwango vya ubora wa nyota.



Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa, Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa Akizungumza kwenye Mkutano Mkuu Maalumu wa Umoja wa Wanawake wa CCM Mkoa wa Mbeya uliofanyika katika Ukumbi wa Shule ya Kutwa ya Mbeya, Jana Novemba 28, 2017.
Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa Akisakata rumba kwenye Mkutano Mkuu Maalumu wa Umoja wa Wanawake wa CCM Mkoa wa Mbeya uliofanyika katika Ukumbi wa Shule ya Kutwa ya Mbeya, Jana Novemba 28, 2017.
Makada wa CCM Mkoani Mbeya wakimlaki Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa Wakati akiondoka kwenye Mkutano Mkuu Maalumu wa Umoja wa Wanawake wa CCM Mkoa wa Mbeya uliofanyika katika Ukumbi wa Shule ya Kutwa ya Mbeya, Jana Novemba 28, 2017.
Makada wa CCM Mkoani Mbeya wakimlaki Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa Wakati akiondoka kwenye Mkutano Mkuu Maalumu wa Umoja wa Wanawake wa CCM Mkoa wa Mbeya uliofanyika katika Ukumbi wa Shule ya Kutwa ya Mbeya, Jana Novemba 28, 2017.
 
Na Mwandishi Wetu, Mbeya
 
Wajumbe wa Jumuiya mbalimbali za Chama Cha Mapinduzi (CCM) wametakiwa kuchagua viongozi waadilifu, weledi na wenye maono ya kuziongoza Jumuiya hizo ila kuendana na kasi ya Mwenyekiti wa CCM Taifa ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
 
Akizungumza wakati wa Mkutano Mkuu Maalumu wa Umoja wa Wanawake wa CCM Mkoa wa Mbeya uliokuwa na Ajenda ya uchaguzi wa viongozi wa Jumuiya hiyo Mkoa na Taifa, Mhe Mwanjelwa ambaye ni mjumbe Halmashauri kuu ya CCM Taifa, Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa aliwasisitiza wajumbe hao kutochagua viongozi kwa matakwa ya urafiki na kujuana Bali kuchagua viongozi wa kazi watakaoisaidia jumuiya kuendana na mtazamo mpya wa CCM Mpya na Tanzania Mpya.
 
Mbali na kuwashukuru makada hao kwa kumchagua kuwa Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Mbeya jambo lililopelekea Mhe Rais John Pombe Magufuli kumteua kuhudumu nafasi muhimu ya Kuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo, Mhe Mwanjelwa alisema kuwa serikali ya awamu ya tano ni ya kazi hivyo uchaguzi huo ni vyema kumalizika kwa kuwapata viongozi wachapakazi.
 
“Tunaelekea kwenye Mbeya Mpya, CCM Mpya, UWT Mpya na Tanzania Mpya hivyo msichague viongozi kutokana na makundi au watakaoendeleza makundi baada ya uchaguzi Bali chagueni viongozi shupavu na wachapakazi” Alikaririwa Mhe Mwanjelwa
Mhe Mwanjelwa (MNEC), alisema kuwa atafanya ziara katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Mbeya ili kuangalia jinsi utekelezaji wa ilani ya CCM inavyotekelezwa.
 
Mkutano huo Maalumu ulimalizika kwa salama hapo Jana Novemba 28, 2017 katika Ukumbi wa Shule ya Sekondari Mbeya ambapo viongozi mbalimbali walichaguliwa katika ngazi ya Mkoa na Taifa.

  Mkurugenzi Mkuu wa MSD,  Laurean Bwanakunu (kulia), akizungumza na maofisa wa Hospitali ya Rufaa ya Amana wakati wa ziara yake ya kikazi ya siku moja Dar es Salaam leo ya kujua changamoto za upatikanaji wa dawa katika hospitali hiyo na kuzitafutia ufumbuzi. Kushoto ni Mganga Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Amana, Meshack Shimwela.
 Mganga Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Amana, Meshack Shimwela, akisisitiza jambo katika mkutano huo.
 Maofisa wa Hospitali ya Rufaa ya Amana wakimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa MSD,Laurean Bwanakunu.
 Meneja wa MSD Kanda ya Dar es Salaam , Celestine Haule akichangia jambo wakaz8i akizungumza na maofisa wa Hospitali ya Rufaa ya Amana.
 Mfamasia wa Hospitali ya Rufaa ya Amana, Anna Kajiru (kulia), akisisitiza jambo kwenye mkutano huo.
 Mkurugenzi Mkuu wa MSD,  Laurean Bwanakunu (wa sita kushoto), akiwa katika picha ya pamoja na maofisa wa Hospitali ya Rufaa ya Amana. 
 Mkutano ukiendelea.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road Dk. Julius Mwaiselage akizungumza katika mkutano huo.
 Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Laurean Bwanakunu akisisitiza jambo wakati akizungumza na maofisa wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road katika ziara hiyo ya siku moja.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road Dk. Julius Mwaiselage ( kulia), akiteta jambo na Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Laurean Bwanakunu wakati wa ziara hiyo.
Mkurugenzi Mkuu wa MSD,  Laurean Bwanakunu (wa tano kulia), akiwa katika picha ya pamoja na maofisa wa Taasisi ya Saratani Ocean. 
 
Na Dotto Mwaibale
 
TAASISI ya Saratani ya Ocean Road wameipongeza Bohari ya Dawa (MSD), kwa usambazaji wa dawa katika taasisi hiyo na maeneo mengine nchini.
 
Pongezi hizo zimetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road Dk. Julius Mwaiselage wakati akizungumza na watendaji wa MSD ambao walifanya ziara ya kikazi ya kujua changamoto mbalimbali za usambazaji dawa katika taasisi hiyo wakiongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Laurean Bwanakunu.
 
Katika hatua nyingine  upatikanaji wa dawa za saratani,vifaa tiba na vitendanishi  vya maabara katika taasisi hiyo ni asilimia 80  kutoka asilimia nne mwaka 2015.
 
Kutokana na hatua hiyo taasisi hiyo imesema ipo haja jamii kutambua mchango mkubwa unaotolewa na Bohari ya Dawa MSD katika kupunguza changamoto za huduma za saratani ambapo ilikuwa kero miaka miwili iliyopita.
 
 Mwaiselage alisema hapo awali  upatikanaji wa dawa vifaa tiba na vitendanishi ilikuwa ni changamoto kubwa katika utendaji.
 
“2015 taasisi hiyo ilikuwa ikipata dawa,vifaa tiba na vitendanishi asilimia nne sasa ni asilimia 80 haya ni matokeo mazuri ya utendaji wa kazi wa MSD,” alisema.
 
Alisema bajeti ya taasisi hiyo mwaka 2015 ilikuwa ni sh.milioni 790 na sasa ni sh.bilioni saba jambo ambalo linatia faraja.
 
Mkurugenzi Mkuu wa MSD,  Laurean Bwanakunu alisema taasisi hiyo inatambua kuwa dawa za kansa ni gharama lakini atahakikisha zinaendelea kupatikana kwa wakati ili kuokoa maisha ya watanzania.
 
Alisema suala la vifaa vya maabara ni tatizo linalohitaji mpango wa kitaifa wa manunuzi.
 
“Nawahakikishia Ocean Road ni mteja muhimu hivyo nipo tayari muda wote kuwahudumia leteni orodha ya mahitaji ya dharura hata leo,” alisema.
 
Mfamasia wa Hospitali ya Rufaa ya Amana, Anna Kajiru alisema katika Hospitali hiyo upatikanaji wa dawa kutoka MSD ni asilimia 80 na kuwa hali hiyo imetokana na ushirikiano mzuri baina yao.
 
“Hivi sasa hali ya upatikanaji wa dawa ambazo zinahitajika sana na wananchi ni mkubwa mkubwa tofauti na zamani na hii inatokana na kazi nzuri inayofanywa na ninyi MSD” alisema Kajiru.
 
Mkurugenzi wa MSD, Laurean Bwanakunu na maofisa wake yupo katika ziara ya kikazi ya kutembelea Hospitali za Mkoa wa Dar es Salaam ambapo leo alitembelea Hospitali ya Rufaa ya Amana na Saratani ya Ocean Road na kesho atazitembelea Hospitali ya Taifa ya  Muhimbili, Vijibweni na Temeke.
 

Na Ofisi ya Waziri Mkuu.

Amesema mfuko huo unalenga kufanikisha ukusanyaji wa fedha za kutosha amabazo ni muhimu kwa Taifa wakati huu tunapoazimia kumaliza ukimwi ifikapo mwaka 2030..

Waziri Mkuu alitoa kauli hiyo leo (Jumanne, Novemba 28, 2017) wakati akifungua kongamano la Kitaifa la maadhimisho ya siku ya ukimwi duniani, lililofanyika jijini Dar es Salaam.

“Nitoe wito kwa Bodi ya Mfuko huu na watendaji wake kuhakikisha wanasimamia kikamilifu fedha hizi ili ziweze kufanikisha malengo ya kuanzishwa kwa Mfuko huu. “

Waziri Mkuu amesema Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Dkt. John Magufuli itaendelea kutenga fedha za mfuko huo na kuhamasisha wananchi, wadau na sekta binafsi kuchangia mfuko huo muhimu.

Wakati huo huo, Waziri Mkuu amesema Serikali imedhamiria kujenga nchi ya viwanda ili waweze kufikia uchumi wa kati, jambo ambalo haliwezi kufikiwa iwapo wananchi wake watakuwa hawana afya bora.

“Hatutaweza kufikia malengo haya kama Taifa iwapo watu wetu hawatakuwa na afya bora kwani nguvu kazi kwa ajili ya Tanzania ya Viwanda itatokana na wananchi wenye nguvu na afya bora.”

“ Hivyo kama Serikali tutahakikisha tunaendelea kutoa huduma bora za afya ili wananchi wetu waweze kuwa na afya bora. Tutaendelea kuwakinga wananchi wetu hususan ni vijana ili Taifa letu liwe na nguvu kazi ya kutosha hasa wakati huu tunapoanza mageuzi makubwa ya kiuchumi na kimaendeleo.”

Pia Waziri Mkuu amesema kwamba kwa sasa Watanzania wengi wana uelewa mkubwa wa ukimwi lakini changamoto iliyopo ni kubadili tabia na kuachana na tabia hatarishi zinazosababisha kupata maambukizo mapya.

Amesema jambo hilo ni hatari kubwa kwa nchi yetu kwa sababu bado wananchi wengi wanaendekeza tabia ya kuwa na wapenzi wengi tena kwa wakati mmoja na hakuna uaminifu katika ndoa.

Kauli mbiu ya maadhimisho hayo kwa mwaka huu “changia mfuko wa udhamini wa udhibiti ukimwi, okoa maisha”.

Kongamano hilo lilihudhuliwa na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-Walemavu Bibi Stella Ikupa Alex, Naibu Waziri Wizara ya Afya, Ustawi wa Jamii, Wazee, Jinsia na Watoto Dkt. Faustine Ndungulile, Makamishna wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS).
Wengine ni Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS), Dkt Leonard maboko, Mwenyekiti wa Baraza la Wanaoishi na virusi vya Ukimwi (NACOPHA), wawakilishi wa wadau wa maendeleo na wadau  wa ukimwi nchini.


Na florah Raphael
MKURUGENZI wa tehama wizara ya ardhi,nyumba na Maendeleo na makazi amepewa miezi saba kukamilisha mradi wa mfumo unganishi wa taarifa za ardhi(ILMIS).
Ujenzi huo wa mfumo wa tehama katika wizara ya Ardhi unadhaminiwa na Benki ya Dunia ikishirikiana na kampuni ya IGN FI unategemewa kumalizika June 2018.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Dar es salaam Waziri wa Ardhi, Nyumba maendeleo na makazi William Lukuvi amesema kuwa serikali inaendelea kubadirisha mfumo wa kutunzia takwimu ili kupunguza ulasimu.
"Tunataka mfumo wa kutunza Kumbukumbu za ardhi huwe wa kisasa ili kupunguza wizi na uzalilishaji na lengo letu nikusambaza mfumo huu nchi nzima na kuongeza ufanisi katika kazi" amesema lukuvia
" Na 1juni 2018 tutazindua hati ya kidigitali ambayo taarifa zote zitakuwa zinapatikana kupitia mfumo hui kwani kutakuwa na uwezo wa kumtambua kila MTU ambaye ajalipa Kodi,kupunguza makanjanjana nani anayedaiwa kodi, pia serikali itaongeza kipato" ameongeza Lukuvi.
Aidha Shabani Pazi Mkurugenzi wa tehama Wizara ya ardhi,Nyumba maendeleo na makazi amesema dhumuni la mradi huu ni kuimarisha usalama katika umiliki wa ardhi  na kuboresha  usahihi wa manunuzi ya ardhi.
Vilevile Pazi amesema kuwa mradi huu umeanzia Kanda ya Dar eso salaam na manispaa ya kinondoni, mradi utahusisha usimamizi wa ardhi, usajili na upimaji, na kuhamisha taarifa za ardhi na Ramani katika mfumo wa kielektroniki.
Pia pazi amesema kuwa utatoa huduma za ardhi nafuu, usalama sahihi wa wateja, kuzuia uvamizi wa ardhi, misitu, na hifadhi ya barabara, kupunguza rushwa katika malipo, usajili na uhamishaji wa hati.
"Mfumo huu utamtambua kila MTU Mwenye hati na tutaongeza mapato kwa kiasi kikubwa, MTU akimiliki hati tutapunguza migogoro ya ardhi,kununua kuuza, kukodisha,ati itatumika kama dhamana ya mkopo Benki au taasisi za kifedha" amesema pazi.

Na. Zephania. j kapaya

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) inasema ina mpango wa kuwaongezea wazee waliofikia umri wa miaka 70 fedha za pensheni jamii zinazotolewa kila mwezi, endapo vyanzo vyake vya kukusanyia mapato vitaimarika au hali itakapo ruhusu.
Kaimu Mkurugenzi Idara ya Wazee,Ustawi wa Jamii Zanzibar, Mhaza Harib Juma, amesema kufuatia malalamiko ya wazee kuwa pesa wanayopewa na serikali kila mwezi haikidhi mahitaji yao, amewataka wafanyabiashara kulipa kodi kwa wakati na wananchi kudai risiti wanaponunua bidhaa ili mapato yaweze kuongezeka na kuiwezesha serikali kufanikisha suala hilo la kuongeza pensheni jamii.
Amesema endapo serikali itakusanya kodi vizuri kupitia vyanzo vyake vya mapato, pensheni hiyo itaweza kuongezwa nakuwataka wazee kuwa wastahamilivu na waridhie na pesa wanazopokea kila mwezi hivi sasa.
Aidha Mhaza ametoa ushauri kwa watoto wa wazee wanaopokea pensheni jamii kuzifanyia biashara fedha hizo ili ziweze kujizalisha na kuweza kukidhi mahitaji ya wazee wao na kuwacha tabia ya kuzitumia fedha hizo kwa mahitaji yao binafsi.
Hata hivyo amesema serikali inalengo zuri la kuwasaidia wazee waliofikia miaka 70 kutokana na kuthamini juhudi na michango yao kwa taifa.
Zaidi ya wazee 27,000 waliofika umri wa miaka 70 wanafaidika na pensheni jamiii, ambayo ni shilingi 20,000 kwa mwezi inayotolewa na serikali tokea April 2016 mwaka jana.



Miongoni mwa vitendo vinavyochangia uharibifu mkubwa wa mazingira nchini ni ukataji miti kwa ajili ya kilimo, nishati ya mkaa na kuni Hali kadhalika utengenezaji wa fanicha.



Vitendo hivyo vya ukataji wa miti bila kibali maalumu vimedhidi kukithiri siku hadi siku huku serikali ya tanzania ikiendelea kukemea vikali uharibifu huo wa mazingira kwa ukataji wa miti, pamoja na kuwafungulia mashitaka wale wote wanaojihusisha na ukataji wa miti bila kibali maalum.

Mkuu wa wilaya  ya Temeke Mh. Felix Lyaniva akiongea na wananchi waliokumbwa na 
adha ya ukataji wa miti.



Hali hiyo imepelekea Mkuu wa wilaya Temeke felix Lyaniva kumpa siku tatu mwenyekiti wa Mwenyekiti wa mtaa wa msakala kata yombo makangalawe Bw Denis Moyo kujisalimisha katika kituo cha polisi mara baada ya tuhuma za kuruhusu kukatwa miti hiyo. 



Agizo hizo la Mkuu wa wilaya Temeke Dsm, Felix Lyaniva limekuja kufuatia kuhusika na ufyekaji wa msitu wa Serikali baada ya kukamata magogo ya miti iliyokatwa katika bonde la msakala wilyani humo kwa idhini ya mtendaji wa mtaa na Mwenyekiti wa mtaa wa msakala jambo ambalo linadaiwa kuwa kinyume cha sheria.



DC Lyaniva ameeleza kuwa mpaka sasa anashikiliwa mtendaji wa kata hiyo, na Kwamba wamepokea taarifa kuwa Mwenyekiti wa mtaa huo Denis Moyo amekimbia na hivyo amempa siku mbili ajisalimishe mwenyewe kwenye kituo cha Polisi Cha Temeke.

Watuhumiwa wanaoshikiliwa na Jeshi la Polisi kwa kosa la ukataji wa miti bila kibali maalumu wakiwa chini ya ulinzi wa polis katika kituo cha polisi cha chang"ombe jijini Dar es salaam

Kwamujibu wa mkazi wa eneo hilo Mohamed Mmeya amemueleza DC Lyaniva kuwa walipojaribu kufuatilia kwa watu waliokuwa wakikata miti hiyo walijibiwa kuwa viongozi hao wa Serikali ndio waliotoa vibali vya kuvuna miti hiyo.




Kwa upande wake mkuu wa kituo cha Polisi mkoa wa Kipolisi Temeke SSCP Muhudhwar Msuya amethibitisha kuwashikilia watu 10 akiwemo mwanamke mmoja katika tukio hilo, na kwamba wamewakuta na mashine moja ya kuchania magogo na kwamba wanaendelea na upelelezi na mahojiano.

Na Yusuph Mwamba

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda leo amezindua mradi wa wa  ujenzi wa Ofisi za kisasa 402 za Walimu Mkoa wa Dar es Salaam Shule ya Msingi Majoe ikiwa ni moja ya ajenda zake za kutaka kuboresha miundombinu ya Walimu katika Mkoa wa Dar es Salaam katika kuleta matokeo mazuri kama ilivyofanya mwaka huu.

RC Makonda amesema kuwa ujenzi wa Ofisi hizo  utaenda kwa kasi ya hali ya juu chini ya kwa sababu una Vijana shupavu wanaousimamia wakitokea JKT, Magereza na Jeshi la Polisi.

Miongoni mwa mambo yatakayojumuishwa kweye ujenzi huo wa Ofisi za kisasa ni pamoja na  Ofisi ya Mwalimu Mkuu, Mwalimu Mkuu Msaidizi, Ofisi ya Walimu wa kawaida, Mhasibu, Karani, Chumba cha kuhifadhi Mitihani, Vyoo vya kisasa, Stoo, Jiko, Chumba cha Mikutano na sehemu kuweka Mafaili ambapo ndani ya ofisi zitafungwa AC, Feni, Samani, Taa za kisasa na Umeme.
Akizungumza Katika uzinduzi huo ulioenda sambamba na upandaji wa Miti RC Makonda, amesema kuwa lengo la ujenzi huo ni kuwezesha Walimu kufanyakazi katika Mazingira mazuri yatakayowapa morali na hamasa ya kufundisha Wanafunzi.

Aidha RC Makonda amesema kama Walimu wakiboreshewa Mazingira ya kufanya kazi itasaidia kukuza ufaulu.

RC Makonda amepongeza Walimu kwa kuwezesha Mkoa wa Dar es salaam kushika nafasi ya kwanza kitaifa katika mtihani wa Darasa la saba ikitokea nafasi ya nne mwaka jana na kuwahimiza kukamatia nafasi hiyohiyo.
"Rais Magufuli ameshatuonyesha dira kwa kutoa elimu bure na sisi wasaidizi wake ni lazima tuendeleze maono yake, mimi sio kiongozi wa kusubiri kuagizwa ndio nifanye kazi kama ilivyo kwa Remote hadi ibonyezwe ndio ifanye kazi, mimi ni kiongozi wa kujiongeza, sijachaguliwa kuwa mzigo kwa serikali bali kuleta matumaini kwa wananchi" Alisema RC Makonda.

Amewataka Viongozi kuacha Siasa kwenye mambo ya Msingi yanayolenga kuleta maendeleo kwakuwa Maendeleo hayana chama wala ubaguzi wa Dini.

Uzinduzi huo umehudhuriwa na Wakuu wa Wilaya, Kamanda wa Polisi kanda maalumu Dar es Salaam Lazaro Mambosasa Kamati ya Ujenzi wa Ofisi za Walimu, Maafisa Elimu, Wakuu wa Shule ambapo Wote kwa pamoja wamepongeza hatua ya RC Makonda kujenga ofisi za Walimu

JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.wabunifumedia.blogspot.com ku-install App ya wabunifumedia,  bila ya kuingia websiteTweet@wabunifumediaonline, youtube@wabunifumediaonline TV, Fb@wabunifumediaonline, insta@wabunifumediaonline

Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam alievaa koti jeusi akiwa pamoja na viongozi wa vyombo vya ulinzi na usalama katika eneo la Police ufundi aliejifunga kitambaa ni mkurugenzi wa kampuni hiyo ya magari kutoka DAR COACH Manmeet Lal.

Muonekano wa magari hayo ambayo yamechukuliwa siku ya leo na kwenda kufanyiwa ukarabati na kuboreshwa zaidi ili yawe na muundo wa kisasa.



Rc Makonda akiwa kwenye moja ya gari hilo.


Wakijadiliana jambo na baadhi ya viongozi toka vyombo mbali mbali vya ulinzi na usalama Mkoa wa Dar es salaam


Viongozi hao kwa pamoja wakisubiria kushuhudia magari hayo yakiwa tayari kuondoka na kupelekwa katika ofisi za matengezo ya kampuni hiyo yaliyopo mkuranga mkoani pwani





Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mheshimiwa PAUL MAKONDA leo amekabidhi Mabasi 10 chakavu ya Vyombo vya Ulinzi na Usalama kwa kampuni ya DAR COACH LTD kwaajili kufufuliwa upya na kuwa ya kisasa.

Mabasi hayo 10 chakavu yanatoka kwenye Vyombo vya Ulinzi na Usalama ikiwemo Jeshi la Wananchi wa Tanzania JWTZ Magari 3, Jeshi la Polisi Magari 4 pamoja na Jeshi la Magereza Magari 3 ambapo yote kwa pamoja Matengenezo yake yameokoa kiasi cha Shilingi Billion 1,110,000,000 ya Serikali.

RC MAKONDA amesema kuwa Gari hizo zitatengenezwa na kukamilika ndani ya Siku 90 ambapo ameipongeza Kampuni ya DAR COACH LTD kwa kujitolea kukarabati Magari hayo bila kutumia pesa ya Serikali.

Aidha MAKONDA amesema Magari hayo yatafungwa Vifaa vya Kisasa ikiwemo Kiyoyozi (AC), Mfumo wa Chaji ya Simu kila Seat, Runinga, Radio, Viti vya kisasa, Vyoo vya Ndani, Bodi mpya pamoja na mwonekano mzima wa Gari ili ziwe za kisasa.

RC MAKONDA amesema mpango wake wa kuendelea kuongezea nguvu Vyombo vya Ulinzi na Usalama hautokoma kwakuwa lengo lake ni kuwatumikia Wananchi na Askari wajivunie kufanyakazi chini ya RC MAKONDA.

Amemuagiza Kamanda wa Polisi kanda maalumu ya Dar es Salaam Lazaro Mambosasa kuhakikisha Ving'ora vya Jeshi la Polisi vinakuwa tofauti na kampuni za Ulinzi na Usalama, Magari ya Wagonjwa ili kupunguza Mkanganyiko kwa wananchi na kujengea heshima Jeshi la Polisi.

Katika hatua nyingine amewataka Wanasiasa kufanya Sasa za kistaarabu badala ya kutukana na kutoa lugha chafu kwa Serikali.

Makabidhiano hayo yameshuhudiwa na Viongozi wa Vyombo vya Ulinzi na usalama akiwemo Kamanda wa Polisi Dar es Salaam LAZARO MAMBOSASA, Mkurugenzi wa usafirishaji JWTZ Kanal RAJAB MWENYUMBU, Mnadhimu wa Jeshi la Magereza ACP. NOEL JAMES ambapo wote kwa pamoja wamempongeza RC MAKONDA
Theme images by Maliketh. Powered by Blogger.