Home Michezo DEAL DONE 'MARIO WELCOME BACK AT HOME NDIVYO WAWEZA UKASEMA DEAL DONE 'MARIO WELCOME BACK AT HOME NDIVYO WAWEZA UKASEMA WABUNIFU MEDIA 08:48:00 A+ A- Print Email Na Yusuph Mwamba MSHAMBULIAJI wa Kimataifa wa Ujerumani na klabu ya soka ya Bayern Munich,Mario Gotze , amerejea kunako klabu yake ya zamani ya Borussian Dortmund baada ya kuitumikia klabu ya Bayern kwa muda wa miaka mitatu. Mshambuliaji huyo wa Kijerumani, amesema atarejea kunako klabu yake ya zamani ya Borussian Dortmund akitokea klabu ya Bayern Munich kwa kandarasi ya miaka minne Endapo dili hilo litakamilika kwa mwanandinga huyo kurejea kunako klabu yake, basi itaigharimu klabu ya Borussian Dortmund kutoa kiasi cha fedha chenye thamani ya Pauni milioni 18.3m sawa na 22m ili uhamisho huo uweze kukamilika. Gotze, ambaye yupo kwenye vipimo kwa sasa na klabu yake hiyo ya zamani, amefanikiwa kumaliza msimu wa ligi kuu ya Ujerumani mwaka jana maarufu kama Bunda Siliga, amefanikiwa kufumania nyavu mara 22 katika jumla ya michezo 83 aliyoichezea kunako klabu ya Dortmund kati ya mwaka 2009 and 2013, na kuisaidia klabu yake kutwaa makombe mawili ya ligi hiyo maarufu kama Bundesliga Mwanadinga huyo aliyependwa zaidi na mashabiki wa klabu ya Borussan Dortmund,aliondoka kunako klabu hiyo miaka mitatu iliyopita na sasa anarejea tena na mashabiki wake wapo tayari kumpokea kwa shangwe. Akizungumza juu ya maamuzi ya kurejea kunako klabu yake ya zamani, CEO wa klabu ya soka ya Dortmund Hans-Joachim Watzke ameyasema haya: "Mimi binafsi sina chuki naye , tuliishi naye vizuri kama ndugu yetu, maamuzi aliyochukua si mabaya kwani hata kipindi anaondoka mwaka 2013,nilijua ipo siku atarudi kunako klabu hii".AlisemaHans-Joachim Watzke "Wakati narudi nyumbani, nahitaji kujaribu kuwashawishi mashabiki zangu katika soka haswa wale ambao hawakupokea ujio wangu wa kurejea, dhumuni langu kwa sasa ni kucheza mpira mzuri kwa ajili ya klabu pamoja na mashabiki wa BVB ". Alisema Gotze Gotze, ndiye mchezaji pekee aliyefanikiwa kuiwezesha timu ya Taifa ya Ujerumani kutwaa kombe la Dunia mwaka 2014 dhidi ya Argentina na kiwezesha klabu ya Bayern Munich kutwaa ndoo ya Bundesliga msimu uluiopita chini ya a Pep Guardiola. Miongoni mwa mafanikio aliyo yapata ni pamoja na kushinda makombe matatu ya ligi kuu ya Bundesliga , makombe mawili ya DFB-Pokals, tpamoja na UEFA Super Cup huku akifanikiwa kutwaa kombe la klabu bingwa Duniani kabla hajahamia kunako Dimba la Allianz Arena kwa ada ya uahamiasho wa Euro 37m mwaka 2013. JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.wabunifumedia.blogspot.com ku-install App ya wabunifumedia, bila ya kuingia website Tweet@wabunifumediaonline, youtube@wabunifumediaonline TV, Fb@wabunifumediaonline, insta@wabunifumediaonline Michezo Tweet Share Share Share Share Share
Post a Comment