Halloween party ideas 2015
Showing posts with label Burudani. Show all posts




                       Na Zephania
Baada ya siku ya jana rapper Stamina kumvisha pete ya uchumba mpenzi wake wa siku nyingi, Veronica, amefunguka mambo machache.
Stamina ameeleza changamoto za mahusiano yao kwa ufupi. Kupitia ukursa wake wa mtandao wa Instagram Stamina ameandika;
Safari yetu ilianzia mbali sana mpaka hapa tulipofikia,,na bado tunaenda mbali mbali zaidi ya tulikotoka,,umenivumilia mengi sana,,vikwazo na matatizo hapa kati tumepitia mengi sana ila bado tukasimama pamoja,,MUNGU ABARIKI KILA HATUA YETU KATIKA MAISHA YETU,,wanga hawakosekanagi katika hili swala ila wamechelewa maana tuna protein za kutoshaa.
Pia Stamina amewashukuru mashabiki wake na watu wake wa karibu kama Roma na mkewe, Nancy kwa kueleza wanamchango mkubwa katika hatua hiyo aliyofikia




Na Florah Raphael

Makumbusho ya Taifa imeandaa onesho  la urithi wa kihistoria la "Fumo Liongo" iliyoandikwa na Prof. Emmanuel Mbogo ambapo wasanii kutokana kikundi cha "kaleleo" watashiriki  ikiwa ni mwendelezo wa programu ya sanaa inayoitwa "museum art explosion" inayofanyika kila ijumaa mwisho wa mwezi, mgeni rasmi katika onesho hilo anatarajiwa kuwa waziri wa habari na utamaduni, Sanaa na michezo Dk. Harrison Mwakyembe.
Akiongea Leo kwa niaba ya mkurugenzi mkuu wa Makumbusho ya taifa, mkuu wa idara ya programu hiyo chance ezekieli amesema kuwa lengo  kubwa la Makumbusho ya taifa ni kurithisha utamaduni wa mtanzania kwa vizazi vilivyopo na vijavyo pamoja na kuwapa nafasi wasanii nchini ya kuona na kujifunza njia bora ya uigizaji kwenye jukwaa.
Pia amebainisha faida zinazopatikana kutokana na mwendelezo wa "museum art explosion"na kusema kuwa zipo faida nyingi zilizopatikana lakini kubwa zaidi imeongeza mwamko wa wasanii kufanya kazi za maonyesho kwenye majukwaa pamoja na kuinua ari za wasanii kuendelea kufanya kazi za sanaa baada ya eneo zuri la kuonyeshea kazi zao.
Kwa upande wake muongozaji mkuu wa mchezo huo wa"Fumo Liongo" Ghonche materego amewashukuru Makumbusho ya Taifa kwa   kuwaalika kikundi kichanga cha "kaleleo" na kusema kuwa lengo lao kubwa ni kuhakikisha wanafufua tamaduni kubwa ambazo zimeonekana kufifia pamoja na kuwarithisha na kuwajenge uwezo wa kufanya maonyesho jukwaani vijana wanaochipukia.
Aidha Ghonche amesema kuwa wanajitahidi kurudisha utamaduni ndani ya jamii wa kwenda kutazama maonyesho ya sanaa kwenye majukwaa.
"Tunarudisha utamaduni wa kwenda kutazama maonyesho ya sanaa majukwaani"amesema Ghonche materego
Kuhusiana na suala la kufifia kwa michezo ya jukwaani Ghonche amesema kuwa sababu kubwa inayopelekea jambo hilo ni maslahi kutokana na kuanzishwa kwa runinga hivyo kupelekea wao kujipatia kipato kiurahisi.
Pia Ghonche ameongeza kuwa sababu nyingine inayopelekea maonyesho ya jukwaani kufifia ni kuwepo kwa ugumu wakupata kumbi za kufanyia mazoezi na maonyesho ambazo ni chache sana nchini.



Na Yusuph Mwamba, Dar
  
MSANII mahili  wa muziki wa uswazi maarufu kama Singeli, Aman Hamis, kwa jina la usanii ‘Man Fongo’amefunguka baada ya kuachia ngoma yake mpya ijulikanayo kwa jina la ’Pop cone mabisi’ akimshirikisha vyema msanii wa miondoko ya RB, Ben Poul
 

Man Fongo, mzaliwa wa Dar es salam, anayetamba kwa kibao chake cha ‘Hainaga ushemeji’alichomshirikisha mwana dada mtanashati Shilole, hivi karibuni aliachia ngoma kali ambayo inaendelea kutamba hapa mjini.
Katika harakati za kutaka kujua ni kwanini aliamua kumshirikisha Ben Poul, Gazeti la Raia Tanzania lilifanya mahojiano naye katika ofisi yake iliyopo Bamaga Makumbusho ili kujua historia yake kwa ufupi na mafanikio yake
Man Fongo, alizaliwa tarehe 15/4/1992 mkoani Dar es salaam, ni mtoto wa 7 kati ya watoto 8 wa mzee Hamis Kibwagale,  alifanikiwa kuhitimu elimu yake ya msingi katika shule ya msingi Kijitonyama Kisiwani mwaka 2008 na kufanikiwa kufaulu lakini alishindwa kuendelea na elimu ya Sekondari kwa sababu binafsi ambayo hakutaka kuitaja.

Akizungumza na Rai Tanzania, Man fongo alianza kuwa DJ wa kupiga nyimbo za Singeli za uswahilini  huku baadhi ya wasanii wa nyimbo hizo wakimchukua kufanya mdananda pale wanapoalikwa, hivyo hakuwahi kufikiria kama ipo siku atakuja kuwa msanii mkubwa licha ya yeye kuupenda mziki huo.

Wakati akiwa shule ya msingi, Man Fongo, alipenda sana kuwa na kazi nzuri ya kuajiriwa Serikalini hivyo ikampelekea kuyapenda  masomo ya sayansi lakini ndoto zake hazikutimia hatimaye akaibukia katika tasnia ya muziki wa uswazi maarufu kama Singeli ambapo mziki huo umetokea kuteka nyoyo za watu wengi hususani wakati wa masherehe mbali mbali.

Aidha, Man Fongo, alianza kuingia katika tasnia ya muziki wa Singeli rasmi mwaka 2006 kwa msukumo wa wasanii ambao alikuwa akiwapigia nyimbo zao akiwa DJ, kwa kuwa wenzake walikuwa wakimuahidi kuondoka nae kupiga nyimbo wakati wa kuondoka wanamuacha naye akaanza kupambana kwa kutunga nyimbo zake mwenyewe na hatimaye akafanikiwa ndipo jina la Man Fongo likipatikana kwa kutoa A katika Amani na kubakisha Man huku fongo liwa jina la kitaa hakusita kulipokea jina hilo na kulitumia katika kazi zake za kisanaa.

Akifafanua kwa nini aliimba na mwana dada Shilole, Man Fongo, alifunguka baada ya kusema kuwa  Shilole ni msanii mkubwa sana kwa upande wanawake,msanii ambaye hanaga majivuno  hivyo kuimba nae kulimfanya ang’are sana katika tasnia ya mziki wa uswazi  maarufu kama singeli kwa kuwa singeli ulikuwa haujashika kasi kama ulivyo sasa.

Kwa sasa msanii huyo aliyetamba na kibao cha ‘Hainaga ushemeji’ na sasa Pop cone mabisi , amefanikiwa kufikisha zaidi ya albamu mbili , hivyo kudondosha kibao kipya ni kwa ajili ya kuwaburudisha wadau wake na kuweza kuufanya muziki wa Singeli kupiga hatua kimataifa.

Hata hivyo, Man Fongo, hakusita kuzungumzia msanii anayempenda katika tasnia hiyo ya muziki wa singeli baada ya nyota yake kumdondokea Majid Migoma aliyetambaa kwa kibao chake cha ‘ mida ya kubeti’ kwa kudai kuwa msanii huyo waliishi wote pamoja walipambana sana kuhangaikia tonge.
Fongo alienda mbali zaidi, huku akisema kwamba katika nyimbo zake zote alizowahi kuzitoa nymbo moja tu ya ‘Safi tuu’ iliyotengenezwa na producer Yogo Beat ndiyo iliyogharimu kiasi kikubwa cha fedha kwa upande wa video kwani ilimgharimu kiasi cha fedha za kitanzania Mil 4.5 lakini nyimbo zote zilikuwa kawaida pamoja na kuonekana kupendwa sana.

Kwa sasa msanii huyo ambaye ni  kipenzi cha watu katika mziki wa singeli , anafanya kazi chini ya Menejimenti yake ijulikanyo kwa jina la Makers Entertainment  ambapo awali walikuwa na migogoro lakini kwa sasa mambo yanaonekana kuwa mubashara.

Miongoni mwa changamoto alizowahi kukumbaana nazo ni pamoja na kutokuwa na mawasiliano mazuri na Menejimenti yake ya Makers Entertainment jambo lililompelkea kushuka chini pamoja na kutoa ngoma mpya lakini hakufanikiwa kushika kasi kwa vile watu aliokuwa akifanya nao kazi hawakuwa na nguvu za kuusogeza muziki huo hivyo kuamua kukaa chini kutatua migogoro yao dhidi ya Menejimenti yake na hatimaye kuliamsha dude na Beb Poul.

Akizungumzia changamoto za jukwaani, Man Fongo, ameenda mbali zaidi kwa kusema kuwa wadau muda wote wanahitaji kupagawishwa hivyo kama msanii lazima awe na vitu tofauti tofauti vya kufanya wadau wamuelewe na kufurahia show.

Akifunguka kuhusiana na kibao chake cha  Hainaga ushemeji, alisema wimbo huo aliutunga kutokana na kuwepo kwa matukio hayo mtaani hivyo kama msanii lazima abadilike kutokana na wakati na mazingira halisi ili kuelezea jamii na kuhabarisha jamii matendo yapo na yanafanyika kwahiyo haikuwa jambo rahisi kutungunga nyimbo kama hivyo.

Akizungumzia uwezo wa ma-producer, Man Fongo, amemwagia sifa kede kede Producer mbunifu Abi dad ambaye ambaye ametokea kuwa  ni kipenzi cha watu kutokana na ubunifu wake aliyetengeneza ngoma kadhaa za wasanii nguli hapa nchini  ikiwemo Ally Kiba, Christian Bella pamoja na Kassim Mganga.

Kwanini kundi lake halina wanawake, Man Fongo amefunguka na kusema muziki huo unaonekana na watu wengi sana, na wanume wanauvaa uhusika wa wanawake, akiwa mwanamke ataanza kucheza na kumwaga radhi lakini mwanaume nae atakatika viuono na kuubeba uhusika wa mwanamke hivyo watazamaji watasema anacheza kama mwanmke kwa mantiki hiyo mwanamke anakuwa hana kazi tena.

Mpaka sasa mafanaikio aliyoyapata tangia aingie katika muziki huo wa singeli ni pamoja na kusafiri nchi za nje kama vile India katika miji ya Bangaloo pamoja na Newdehl kwa ajili ya show akiambatana na mwana dada Shilole, kupata tuzo ya msanii chipukizi mwaka 2016, mbali na hayo pia amaefanikiwa kufunga ndoa 2016 katika fungo  na sasa anatarajiwa kuitwa baba ifikapo mwezi wa 3 mungu akipenda,  kanunua kiwanja kilichopo Saranga Kimara , gari aina ya Voxy wagen new model, kushiriki katiaka fiesta 2016 akiwa pamoja na Wizkid, nyama choma Festival, hivyo anaendelea kula bata kwa kile alichokivuna.

Kuhusu msanii anayemuumiza kichwa katika singeli, Man Fongo amefunguka baada ya kusema kuwa hajaona msanii wa kumsumbua kwani yeye ni msanii pekee wa singeli aliyesafiri nje ya nchi, mwenye tuzo hivyo kama watatokea wasanii wenye CV za aiana yake ndipo atamtaja msanii anaye muumiza kichwa .
Kufanya ngoma na Ben Poul, Man Fongo, amesema kuwa Ben Poul, ni msanii mkubwa sana anayetambulika kimataifa  hivyo kufanya muziki na msanii huyo kutamfanya nae aweze kutambulika kimataifa hivyo wadau wa Ben Poul wakisikia ngoma yake watapenda kusikiliza hivyo kuufanya mziki wa singeli kuwa wakimataifa kama ulivyo kwa muziki mwengine kama vile Hip hop au Bongo Fleva, wadau wanataka ujumbe tofauti tofauti na ujazo wake hivyo ana anaamini Ben Poul atamsaidia kumtangaza Kimataifa.

Mpaka sasa Man Fongo, ameachia ngoma kali ijulikanayo Pop cone mabisi wenye ujumbe wa kuwahamasisha vijana wafanye kazi waondokane na utegemezi na njia za haramu za kujipatia fedha kama vile kubaka, kuuza dawa za kulevya kwani wakifanya biashara ndogo ndogo zitawasaidia kukimu mahitaji yao na hatimaye kusonga mbele kimaisha, pia amepongeza hatuaza vijana kuchipukia katika mziki huo wa singeli kwamba unaleta hamasa na changamoto katika tasnia hiyo ya nymbo za singeli.

Ushauri kwa Serikali, na wadau wengine, amesema kuwa singeli ni mziki wa kinyumbani, chimbuko la kitanzania hivyo lazima upewe kipaumbele kama ilivyo kwa mizki mingine hapa nchini ili kujivunia asili ya kitanzania.



JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.wabunifumedia.blogspot.com ku-install App ya wabunifumedia,  bila ya kuingia websiteTweet@wabunifumediaonline, youtube@wabunifumediaonline TV, Fb@wabunifumediaonline, insta@wabunifumediaonline



New York ,Marekani.

MSANII na mtunzi wa nyimbo kutoka Marekani, Beyonce Knowles, yupo mbioni kumiliki moja ya vilabu vikubwa vya Mpira wa Kikapu nchini Marekani ambapo anaipigia mahesabu ya kuinunua timu ya Houston.
 

Beyonce na mumewe ambaye ni msanii nguli wa Marekani, Jay Z, wanaonekana sio wageni katika biashara hiyo ya kuendesha timu ya NBA, kwa kuwa awali Jay Z alishawahi kuwa na hisa yake ndogo katika timu ya Brookly Nets mwaka 2003 hadi 2004, alikuja kuachana nayo bada ya kuibuka mgogoro wa kimaslahi baada ya kuunda Roc Nation Sports.


Hadi sasa, hakuna taarifa rasmi iliyotolewa kuhusiana na ununuzi wa timu hiyo inayoshiriki ligi ya NBA.



JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.wabunifumedia.blogspot.com ku-install App ya wabunifumedia,  bila ya kuingia websiteTweet@wabunifumediaonline, youtube@wabunifumediaonline TV, Fb@wabunifumediaonline, insta@wabunifumediaonline

Theme images by Maliketh. Powered by Blogger.