NA JANETH JOVIN
WASANII nchini
wametakiwa kuacha kulewa sifa mara baada ya kupata mafanikio badala yake
wajitume zaidi na kutumia vipaji walivyonavyo kuelimisha jamii.
Hayo yalisemwa na Meneja wa msanii wa Ally Nipishe, Hafam
Fadhili wakati akizungumza na mwandishi jijini Dar es Salaam jana.
Alisema kama wasanii watajitambua na kujituma kwa bidii
wataweza kupata mafanikio makubwa na kutimiza ndoto zao walizojiwekea.
“Unajua mafanikio hayaji hivihivi ni lazima kujituma katika
kila jambo unalolifanya, wasanii wa bongo wengi wao wamekuwa wakibweteka na
kuzani kuwa bila kufanya jitihada unaweza kufanikiwa napenda kuwaambia kuwa
wananidanganya kama wanataka kupata mafanikio ni muhimu kujitambua na kujituma,”
alisema.
Hata hivyo Fadhili alisema msanii kujiwekea malengo ni
jambo la busara kwani suala hilo ndilo ufanikisha kila kitu ambacho mtu
anapanga kukifanya.
Mwishoo…..
Post a Comment