Halloween party ideas 2015




Na Zephania Kapaya

Watanzania wametakiwa kuhudhuria semina ya ufunguzi wa onesho la chimbuko la Binadamu wa Afrika  ikiwa ni onesho na matokeo ya tafiti mbalimbali zilizofanyika bonde la Olduvai na Laetoti hifadhi ya mamlaka ya Ngorongoro.

Hayo yamesemwa na Prof.Audax Mabula ambaye ni mkurugenzi wa Makumbusho Taifa ambapo ameekeza kuwa  Makumbusho ya ya Taifa ikishirikiana na ubalozi wa Spain Tanzania,Makumbusho ya Aikolojia ya Madrid,Taasisi ya chimbuko la Binadamu(IDEA) Madrid,Chuo kikuu cha Acla Madrid na Makumbusho ya Cosmocaixa Barcelona- Spain na kampuni ya siment ndio waliondaa onesho hilo wakiwa na lengo la kuwaonesha na kuwafunza watu mbalimbali kuhusiana na chimbuko la Binadamu Afrika.

Aidha Prof.Mabula amesema mgeni rasmi katika onesho hilo ni Waziri wa Maliasili na Utalii Dr Hamis Kigwangwalla na litazinduliwa saa 11:00 jioni Makumbusho ya Taifa jijini dar es salaam na wageni mbalimbali wanatariwa kuwepo wakiwamo Mabalozi,wananchi,na viongozi mbakimbali.

Prof.Mabula ameendelea kwa kusema kuwa vionyeshwa vyote katika onesho hilo vimepatikana hapa Tanzania kutokana na tafiti za kisayansi na vimehifadhiwa Makumbusho ya Taifa vioneshwa hivo ni pamoja na Masalia ya Zamadamu,Zana za Mawe na Masalia ya Wanyama walioishi takribani tangu milioni 4 iliyopita.

Prof Mabula amemaliza kwa kuwataka wananchi wote kuhudhuria kwa wingi  katika onesho hilo pamoja na semina kwani hakuna kiingilio na kwa siku ya pili kiingilio kwa MTU mzma ni shilingi 1500,mtoto ni shilingi500.




Na Zephania

Klabu ya Borussia Dortmund leo tarehe 10 Novemba 2017, imeushangaza ulimwengu wa soka baada ya kutangaza kumfukuza kazi kocha wake, Peter Bosz na kumuajili Peter Stöger.
 Peter Bosz amepoteza michezo 12 tangu ajiunge na klabu hiyo na kitu pekee cha kushangaza ni kwamba Dortmund wamemuajili kocha ambaye ametimuliwa na klabu ya inayoshika mkia wa ligi kuu nchini Ujerumani Bundesliga.
Kuchaguliwa kwa Peter  Stöger kumezua gumzo kubwa nchini Ujerumani kwani wadau wengi wa soka wanasema Dortmund wamekosea kumsajili Kocha ambaye mwenye historia mbaya kwenye kufundisha timu za Ujerumani.
Peter Stoger amepoteza mechi 8 na kupata sare 3 kabla ya kutimuliwa na klabu ya FC Cologne ambayo inashika mkia kwenye msimamo wa Bundesliga. Ambapo imeelezwa kuwa ndio kocha wa kwanza kuanza vibaya kwenye tangu ligi hiyo ianzishwe.
Na hii inakuwa ni hatua ya kwanza kwenye historia ya Ligi kuu nchini Ujerumani kwa kocha mwenye karba hiyo kuajiliwa na klabu kubwa nchini humo.




      Na Zephania
Klabu ya Manchester City imeendeleza ubabe wake kwenye ligi kuu soka ya England baada ya kumchapa hasimu wake wa jiji moja Manchester United goli 2-1.

Kwenye mchezo huo ambao City ilimiliki mpira wakati mwingi, ilipata goli lake la kwanza kupitia David Silva dakika ya 43 kabla ya Marcus Rashford kusawazisha dakika ya 45 na baadae Nicolás Otamendi kupachika la pili na la ushindi kunako dakika ya 54.
Meneja wa Manchester United Jose Mourinho amesema kwa sasa ni wazi asilimia kuwa ya ubingwa wa EPL msimu huu ukaenda kwa City.
Wamecheza vizuri, wengi walitarajia hili, ni vigumu kuwakabili kama hauna timu imara zaidi yao, tumemkosa Pogba ambaye angeweza kuleta madhara kwao, nafikiri wanaweza kuwa mabingwa msimu huu.’‘ amesema Mourinho kwenye mahojiano yake baada ya kumalizika kwa mchezo wa jana.
Kwa misimu miwili mfululizo Manchester City imefanikiwa kushinda michezo miwili ndani ya dimba la Old Trafford na hakuna timu iliyofanya hivyo




                       Na Zephania
Baada ya siku ya jana rapper Stamina kumvisha pete ya uchumba mpenzi wake wa siku nyingi, Veronica, amefunguka mambo machache.
Stamina ameeleza changamoto za mahusiano yao kwa ufupi. Kupitia ukursa wake wa mtandao wa Instagram Stamina ameandika;
Safari yetu ilianzia mbali sana mpaka hapa tulipofikia,,na bado tunaenda mbali mbali zaidi ya tulikotoka,,umenivumilia mengi sana,,vikwazo na matatizo hapa kati tumepitia mengi sana ila bado tukasimama pamoja,,MUNGU ABARIKI KILA HATUA YETU KATIKA MAISHA YETU,,wanga hawakosekanagi katika hili swala ila wamechelewa maana tuna protein za kutoshaa.
Pia Stamina amewashukuru mashabiki wake na watu wake wa karibu kama Roma na mkewe, Nancy kwa kueleza wanamchango mkubwa katika hatua hiyo aliyofikia
IMG-20171210-WA0045
Na Christina Mwagala
 MSTAHIKI Meya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita ameondoka Jijini hapa jana jioni kuelekea  Addis Ababa, kuhudhuria mkutano wa kujadili changamoto zinazo wakabili viongozi wa serikali za mitaa.
Mkutano huo wa siku tatu umeandaliwa na Umoja wa Mataifa ambapo unalengo la kujadili na kutoa majibu ya changamoto ambazo wanakutana nazo viongozi wa serikali za mitaa wakiwepo Mameya wote.
Miongoni mwa changamoto ambazo zitajadiliwa katika mkutamo huo pamoja na mambo mengine ni  suala la bajeti katika halmashauri na ukusaji wa mapato.
Mbali na Mameya ,mkutano huo pia utahudhuriwa na viongozi wengine wa serikali za mitaa kutoka Nchi mbalimbali.
Aidha Meya Mwita atazungumza na mkutano huo kuelezea changamoto zilizopo katika jiji la Dar es Salaam , namna ambavyo  kwa asilimia kadhaa wameweza kuzitatua.
Aidha katika mkutano huo ataeleza pia mafanikio yaliyopo katika jiji la Dar es Salaam kupitia sekta mbalimbali za Maendeleo.
” Katika mkutano huo hatuta kuwa jiji la Dar es Salaam pekee ,ni Nchi mbalimbali Duniani zitakuwepo, tutajadili changamoto zinazo tukabili kwenye halmshauri zetu, mafanikio,lakini pia kujengeana uwezo kwenye utendaji kazi” alisema Meya Mwita.

Imetolewa leo Desemba 11
Na Christina Mwagala , Afisa Habari Ofisi ya Mstahiki Meya wa jiji

Picha-no.-5-1

Na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete
 Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na Taasisi ya Okoa Moyo wa Mtoto (Save a Child’s  Heart – SACH) ya nchini Israel zimewapeleka  watoto sita (6) wenye umri wa mwaka mmoja hadi  miaka kumi na tatu  nchini Israel kwa ajili ya matibabu ya moyo.

Katika safari yao ya matibabu nchini humo watoto, wauguzi pamoja na wazazi wao wameondoka alfajiri ya jana tarehe  10/12/12. Baada ya matibabu ya watoto kukamilika  Maafisa Wauguzi wawili watabaki kwa ajili ya kuhudhuria mafunzo ya mwaka mmoja ya jinsi ya kuwahudumia wagonjwa waliopo katika wodi ya uangalizi maalum (ICU) na chumba cha upasuaji.

Taasisi  yetu inatibu magonjwa mbalimbali ya moyo kwa watoto  kupitia  wataalamu wazalendo tulionao. Hata hivyo tunamkataba na Israel kwa baadhi ya wagonjwa wachache wanaohitaji utaalamu wa juu zaidi kuwapeleka nchini humo kwa ajili ya matibabu.

Tunaushirikiano mzuri na nchi ya Israel kwani gharama za matibabu ya watoto hawa zinagharamiwa na SACH. Licha ya Maafisa Wauguzi wawili kubaki nchini humo kwa ajili ya kuhudhuria mafunzo pia tuna madaktari bingwa wa magonjwa ya moyo sita   na wauguzi wawili ambao wamesoma nchini Israel na hivi sasa wanatibu wagonjwa katika Taasisi yetu.Aidha Daktari wetu mmoja bado anaendelea na masomo nchini humo.

Hili ni kundi la tano  la watoto kwenda kutibiwa magonjwa ya moyo nchini Israel tangu mwaka 2015 ambapo Taasisi ya Moyo ilianza ushirikiano  na Taasisi ya Okoa Moyo wa Mtoto (Save a Child’s Heart –SACH)  ya kuwapeleka wagonjwa nchini humo. Hadi sasa watoto 46 wameshatibiwa nchini humo na wanaendelea vizuri.

Taasisi inaendelea kutoa wito kwa wazazi na walezi wasisahau kupima afya za watoto wao pale watakapoona kuna hali ya tofauti katika ukuaji wa mtoto kwani magonjwa mengi ya moyo yanaanzia utotoni. Mtoto akianza kuuguwa magonjwa ya moyo wazazi wengi wanadhani ni matatizo ya kifua baada ya kumfikisha mtoto Hospitali na kufanyiwa vipimo  ndipo inagundulikwa kuwa mtoto anasumbuliwa na magonjwa ya moyo.

Imetolewa na :

Kitengo cha Uhusiano na Masoko
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete
11/12/2017

Na Mwandishi wetu
……………………………………………………..
Wadau wa Utalii Jijini
Arusha wamempongeza Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla kwa
kukubali kuyafanyia kazi mapendekezo yao ya kuwaingiza wajasiriamali wadogo katika
utoaji wa huduma za kusafirisha watalii nchini.
Kauli hiyo imetolewa
jana na
Mwenyekiti wa Chama cha Waongoza
Watalii Tanzania (TATO), Wilbard 
Chambulo wakati akichangia
mapendekezo ya viwango vipya vya leseni za biashara ya utalii zilizowasilishwa
kwao na Uongozi wa Wizara ya Maliasili na Utalii Jijini humo.
Chambulo
alisema kwa muda mrefu sasa kanuni zinazotumika zinamtaka mfanyabiashara ya
usafirishaji watalii awe na magari matatu kwa kiwango cha chini ikiwa ni pamoja
na kulipia ada ya leseni ya Dola za Kimarekani 2,000 sawa na wafanyabiashara
wengine matajiri 
jambo ambalo limekuwa likiwabagua wafanyabiashara wadogo.
“Tunakupongeza
sana Mhe. Waziri kwa kutupa angalao hilo moja, tuliomba mwenye kagari kamoja nae
aruhusiwe na apewe leseni walau ya dola 200 ili afanye biashara kidogo kidogo
mwishowe atanunua gari tano na kuendelea, tunataka sisi Watanzania wote tufaidike
na rasilimali zetu,” alisema Chambulo.
Awali
akiwasilisha mapendekezo ya viwango hivyo vipya vya leseni ya biashara ya
utalii, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utalii, Wizara ya Maliasili na Utalii,
Deogratias Mdamu alisema kwa upande wa watanzania ambao ni wajasiriamali wadogo
wenye gari moja hadi magari matatu watatakiwa kulipa ada ya leseni ya dola za
Kimarekani 200.
Kwa upande
wa wafanyabiashara wenye magari kuanzia manne hadi kumi alisema imependekezwa walipe
Dola za Kimarekani 2,000, wenye magari 11 hadi 50 Dola za Kimarekani 3,000,
magari 51 hadi 100 Dola za Kimarekani 10,000 na magari 100 na kuendelea Dola za
Kimarekani 15,000.
Kwa upande
wa wafanyabiashara ambao sio Watanzania wenye magari 10 hadi 30 imependekezwa
walipe Dola za Kimarekani 10,000, magari 31 hadi 100 Dola za Kimarekani 15,000
na magari 101 na kuendelea Dola za Kimarekani 20,000.
Kwa upande
wake Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla alisema lengo la
kuwasilishwa kwa mapendekezo hayo ya viwango hivyo vipya vya leseni ya biashara
ya utalii kwa wadau ni kuweka ushirikishwaji na makubaliano ya pamoja ya
kutekeleza kanuni hizo.
Alisema sehemu
kubwa ya mapendekezo hayo imezingatia maombi na maoni ya wadau hao ambayo
yaliwasilishwa kwake awali. “Kilio chenu nimekisikia mimi mwenye mamlaka ya kufanya mabadiliko, lengo kubwa la mapendekezo haya ni kuwawezesha wajasiriamali
wadogo wenye gari moja waweze kuingia kwenye biashara hii ya utalii pamoja na
kuongeza mapato ya Serikali na jamii kwa ujumla,” alisema Dk. Kigwangalla.
Katika
hatua nyingine amewaagiza watalaamu ndani ya Wizara yake kuhakikisha
wanakamilisha kanuni hizo mpya ndani ya mwa mwaka huu ili utekelezaji wake
uanze mapema mwakani, 2018.
Akizungumzia
wafanyabiashara wanaofanya biashara ya kuwasafirisha watalii nyuma ya pazia
bila kulipia leseni, alisema Wizara yake inaandaa mfumo maalumu wa
kielektroniki utakaowezesha ukaguzi wa magari kwenye mageti ya kuingilia hifadhini
ili kudhibiti vitendo hivyo.

Aidha,
ametoa onyo kali kwa wafanyabiashara hao na kuwataka kufanya biashara hiyo kwa
weledi na kuzingatia kanuni na taratibu zilizowekwa ikiwemo kulipa ada ya leseni
husika kwa mujibu wa sheria. 
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla (kulia) akizungumza na wadau wa utalii
Jijini Arusha jana ambapo Wizara yake iliwasilisha mapendekezo ya viwango vipya
vya leseni za biashara ya utalii na tozo ya ada za malazi katika viwango vya
ubora wa nyota. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii,
Dk. Aloyce Nzuki. 
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza na wadau wa utalii
Jijini Arusha jana ambapo Wizara yake iliwasilisha mapendekezo ya viwango vipya
vya leseni za biashara ya utalii na tozo ya ada za malazi katika viwango vya
ubora wa nyota. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Dk.
Aloyce Nzuki na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utalii, Wizara ya Maliasili na
Utalii, Deogratias Mdamu (kushoto).
Baadhi ya
viongozi wa Wizara ya Maliasili na Utalii na Taasisi zilizopo chini ya Wizara
hiyo wakiwa kwenye mkutano huo.
 Baadhi ya viongozi wa Wizara ya Maliasili na Utalii na Taasisi zilizopo chini ya Wizara hiyo wakiwa kwenye mkutano huo.
 Baadhi ya
wadau wa Utalii walioshiriki mkutano huo.
Mwenyekiti wa Chama cha Waongoza Watalii Tanzania (TATO),
Wilbard 
Chambulo
akichangia mapendekezo ya viwango vipya vya leseni za biashara ya utalii zilizowasilishwa
kwao na Uongozi wa Wizara ya Maliasili na Utalii katika mkutano huo.
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla (kulia) akitambulishwa na Naibu
Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Dk. Aloyce Nzuki (kushoto) kwa Mjumbe
wa Bodi ya Wadhamini ya
Chama cha Waongoza Watalii Tanzania (TATO), Merywn Nunes muda mfupi baada ya
kikao na wadau wa utalii Jijini Arusha jana ambapo Wizara yake iliwasilisha mapendekezo
ya viwango vipya vya leseni za biashara ya utalii na tozo ya ada za malazi
katika viwango vya ubora wa nyota.
Theme images by Maliketh. Powered by Blogger.