PILI PILI hulimwa sehemu nyingi sana takribani ulimwengu mzima. Kumekuwa na tamaduni kwa watu wengi kula pili pili wakati wa kula chakula pia wengine huchanganya kwenye mboga
Pamoja na zao hilo kulimwa karibia ulimwengu mzima, lakini kuna aina mbali mbali za pili pili,kama pili pili kichaa, pili pili mbuzi, paprika, capsicum, bell pepper, capsicum frute scens, pamoja na caynne pepper n.k
Kwa leo ngoja nijikite kuelezea kuhusu pili pili mbuzi, hii ,ndio inayotumika sehemu nyingi Tanzania kutengeneza chachandu kwa sababu ina harufu nzuri na ladha.
Nimeuliza zaidi ya watu hamsini kujua kuwa wanajua jina la kitaalamu hakuna aliyenipa jibu zaidi ya kusema ni pili pili mbuzi.
Jina la kibotania huitwa Habanero peppers. Pili pili mbuzi ina Vitamini A,B,C,. Pili pili mbuzi hutumika kama kiungo katika mapishi mbalimbali.
Pili pili mbuzi hutumika sehemu nyingi mjini na vijijini kutengeneza chachandu ya kulia nyama choma, Samaki, Kuku, Ndizi pamoja na Mihogo n.k.
Licha ya kuwa ni kiungo cha chakula lakini, pili pili pia ina kimeng'enyo aina ya capsaicin ambacho kina manufaa makubwa ikwa afya ya binadamu. Pili pili mbuzi ikitumika vizuri huzuia kushambuliwa kwa moyo na kufanya usipate na shinikizo la juu la moyo, huzuia kupata kisukari kirahisi.
Pili pili mbuzi, hutibu maumivu ya viungo baridi yabisi (Rhehumatism), maumivu ya misuli, pili pili mbuzi ikiliwa mara kwa mara hudhibiti na kunguza lehemu mwilini (Bad Cholesterol), hudhibiti kuongezeka kwa uzito wa mwili kwa kuwa kuna capsaicin inayoongeza Thermogenesis ndani ya mwili, pili pili mbuzi ikitumika vizuri hufaa kwa mzunguko wa damu mwilini kuzunguka vizuri, huratibu kusagika chakula, hupunguza uwezekano wa kupata mafua ya mara kwa mara.
Pia vidonda vya koo, homa, kupunguza ulevi wa jana (hangover), pili pili mbuzi ya kijani ina vitamini C kwa wingi inayofaa kulinda kinga ya mwili, kuimarisha fizi, kuimarisha misuli ya mwili na kutibu vidonda weka unga wa pili pili juu ya vidonda.
Pia unaweza kutengeneza sosi ya pili pili mbuzi kwa mafuta ya Zeituni, karoti, Vitunguu maji, Vitunguu saumu, pili pili mbuzi, maji, jusi ya ndimu, siki nyeupe, nyama, chumvi kidogo na pili pili manga.
JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.wabunifumedia.blogspot.com ku-install App ya wabunifumedia, bila ya kuingia websiteTweet@wabunifumediaonline, youtube@wabunifumediaonline TV, Fb@wabunifumediaonline, insta@wabunifumediaonline
Post a Comment