Na Issa Ramadhani
UTAFITI uliofanywa na wanasayansi ,umeonesha kuwa kati ya watu wa nne wenye dalili za
maambukizi ya ugonjwa wa kisonono na pangusa waliotumia dawa ya antbiotics wakipima kwa mara ya pili
watatu kati ya hao hawana tena magonjwa
hayo kutokana na ubora wa dawa hizo,ila mmoja ana vimelea vya magonjwa hayo ya
zinaa.
Utafiti huo ulifanywa na watafiti kutoka Hospital ya
St.Johnhuko Michgani na ulijumuisha sampuli ya watu 1,103, ambao waliugua
magonjwa hayo na kutumia dawa za
Antbiotics.
Watu hao ambao walitibiwa kwa dawa za
antibiotics,waliporudiwa hospital na kupimwa tena baada ya magonjwa hayo.
Miongoni mwa dalili za magonjwa hayo ya zinaa ni kama kuhisi maumivu au kuhisi
kichomi wakati wa kukojoa,kuongezeka kutokwa kwa majimaji ukeni,majimaji hayo
ambayo ni ya njano au yaliyochanganyika n damu.
DK.Karen Jones kutoka hospital ya St.Jones alikaririwa
katika mtandao wa health science akisema kuwa antbiotics ni miongoni mwa dawa
nzuri zilizothibitika katika kutibu baadhi ya magonjwa ya zinaa kama kisonono
na pangusa,ambazo hutoa majibu mazuri ikiwa zitatumiwa bila kukatishwa kwa
dozi.
Mbali na magonjwa hayo pia kuna magonjwa kama
kaswende,trichomoniasis,genitalwarts,ambayo yote huweza kutibiwa na antbiotics
kwa usahihi.
Pia DK.Karen alishauri kuwa watu wenye wapenzi zaidi ya mmoja wawe na tabia ya kwenda kupima magonjwa ya zinaa mara kwa mara ili kujua hli za afya zao.
Pia DK.Karen alishauri kuwa watu wenye wapenzi zaidi ya mmoja wawe na tabia ya kwenda kupima magonjwa ya zinaa mara kwa mara ili kujua hli za afya zao.
Pia alishauri ikiwezekana waachene na vitendo vya kuwa na
wapenzi zaidi ya mmoja au watumie Kondom ili kupunguza hatari ya maambukizi ya
magonjwa ya zinaa.
Ifahamike kuwa magonjwa ya zinaa yakikaa mwilini kwa muda
mrefu bila kutibiwa husababisha athari mbaya nyingi ikiwa ni pamoja na ugumba.
JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.wabunifumedia.blogspot.com ku-install App ya wabunifumedia, bila ya kuingia websiteTweet@wabunifumediaonline, youtube@wabunifumediaonline TV, Fb@wabunifumediaonline, insta@wabunifumediaonline
Post a Comment