Na Mwandishi wetu, Dar es salaam
TANZANIA ni nchi inayo ongozwa kwa misingi ya demokrasia na katiba, nchi yoyote ili iweze kusimama lazima iwe na katiba yake na wanachi pamoja na viongozi waitambue na kuilinda
Katiba ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
SEHEMU YA PILI
MALENGO
MUHIMU NA MISINGI YA MWELEKEO WA
SHUGHULI ZA KISERIKALI
Ufafanuzi Sheria ya 1984 Na.15ibara.6
6.Katika Sehemu ya Sura
Hii,isipokuwa kama maelezo yahitaji vinginevyo “Serikai”
Maana yake
ni pamoja na serikali ya Jamhuri ya Muuungano,Serikali ya mapinduzi ya
Zanzibar ,
Serikali za mitaa na pia mtu anayetekeleza
madaraka au mamlaka yoyote kwa niaba ya Serikali yoyote.
Matumizi ya masharti ya sehemu ya pili.Sheria ya 1984 Na.15
ibara6
7-(1) Bila ya kujali masharti ya
ibara ndogo ya
(2),Serikali,Vyombo vyake na watu wote au mamlaka yoyote
yenye kutekeleza madaraka ya utoaji
Haki,watakuwa na majukumu na wajibu wa
kuzingatia,kutia maanani na kutekeleza
masharti yote
Ya sehemu hii ya surah ii.
(2) Masharti ya sehemu hii ya surah ii hayataingiliwa nguvu
ya kisheria na mahakama yoyote .kuamua
Juu ya suala kama utendaji au kukosa kutenda
sheria,au hukumu yoyote,inaambatana na masharti
ya sehemu hii ya surah ii.
Serikali na watu ,sheria ya
ujenzi na ujamaa na kujitegemea sharia ya 1984.na15.ibara.6 sheria
na.4 ya 1992 ibara .6
8-(1 )Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni nchi inayofuata misinginya demokrasia nah
ski ya kijamii, na
Kwa hiyo-
(a)wananchi ndio msingi wa mamlaka yote,na Serikali
itapatikana madaraka na mamlaka yake yote,
Na serikali itapata madaraka na mamlaka yake
yote kwa mujibu wa katiba hii:
(b)Lengo kuu la Serikali litakuwa ni ustawi wa wananchi:
(c)Serikali itawajibika kwa wananchi:
(d)Wananchi
watashirikiki katika shughuli za
serikali yao kwa mujibu wa masharti ya katiba hii
(2) Muundo wa
serikali ya jamhuri ya muungano na
serikali ya mapinduzi ya Zanzibar, au wa
cheo
Chochote kati ya vyombo vyake na
uendeshaji wa shughuli zakeutatelekezwa kwa kuzingatia umoja
Wa jamhuri
ya Muungano na haja ya kukuza umoja wa kitaifa na kudumisha heshima ya Taifa.
9.Lengo la katiba hii ni kuwezesha ujenzi wa Jamhuri ya
Muungano na serikali ya mapinduzi Zanzibar au wa chochote kati ya vyombo vyake
na ndugu na amani kutokana na kufuata siasa ya Ujamaaa na kujitegemea,ambayo
inasisitiza utekelezaji wa misingi ya ujamaa kwa kuzingatia mazingira yaliyomo
katika jamhuriya muungano.Kwa hiyo,Mamlaka ya Nnchi na vyombo vyake vyote
vinawajibika kueleza sera na shughuli zake katika lengola kuhakikisha-
(a); Kwamba utu na haki nyinginezo zote za binadamu zinaheshimiwa
(b)Kwamba
sheria za nchi zinalindwa na kutelekezwa;
(c)Kwamba shughuli
za serikali zitatekelezwa kwa njia ambazo zitahakikisha kwamba utajili wa taifa
Unaendelezwa ,unahifadhiwa
na unatumiwa kwa manufaa ya wananchi wote kwa ujumla na pia
Kuzuia
mtu kumnyonya mtu mwingine;
(d)Kwamba
maendeleo ya uchumi wa Taifa yanakuzwa na kupangwa kwa uangalifu na kwa pamoja;
(e) Kwamba
kila mtu mwenye uwezo wa kufanya kazi anafanya kazi, na kazi maana yake
ni shughuli
Yoyote ya
halali inayompatia mtu riziki yake;
(f)Kwamba
heshima ya binadamu inahifadhiwa na kufuata Kanuni za Tangazo la Dunia Husika
kuhusu
Haki za
binadamu;
(g)Kwamba serikali na vyombo vyake vyote vya
umma vinatoa nafasi zilizo sawa kwa raia
wote,wake
kwa waume
,bila ya kujali rangi,kabila,dini au hali ya mtu;
(h)Kwamba aina
zote za dhuluma,vitisho,ubaguzi,rushwa,uonevu na upendeleo zinaondolewa nchini;
(i)Kwamba matumizi ya utajiri wa Taifa
yanatilia mkazo maendeleo ya wananchi na
hasa zaidi
Yanaelekezwa
kwenye jitihada ya kuondosha umasikini,ujinga na maradhi;
(j)Kwamba
shughuli za uchumi haziendeshwi kwa njiazinazoweza kusababisha ulimbikizaji wa mali
au njia kuu
za chumi katika mamlaka ya watu wachache binafsi;
(k)Kwamba nchi
inatawaliwa kwa kufuata misingi ya kidemokrasia au ujamaa;
Nafasi na mamlaka ya
chama sharia ya 1984.Na.15.ibara6
10.[ibara ya 10 ya katiba imefutwa na sharia na.4 ya 19920)
Itaendelea..
JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.wabunifumedia.blogspot.com ku-install App ya wabunifumedia, bila ya kuingia websiteTweet@wabunifumediaonline, youtube@wabunifumediaonline TV, Fb@wabunifumediaonline, insta@wabunifumediaonline
Post a Comment