WAKATI ligi kuu ikiendelea kushika kasi, homa ya pambano la watani wa jadi lazidi kushika kasi kuelekea mtanange huo unaotarajiwa kuwa wa kukata na shoka.
Simba na Yanga ni kati ya timu kongwe hapa nchini zenye mashabiki lukuki, watakutana katika mtanange huo unaotarajiwa kupigwa Oktoba mosi kwenye Uwanja wa Taifa Jijini Dar es salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari, Kocha msaidizi wa mabingwa hao watetezi wa Yanga, Mwambusi ameiambia WABUNIFUMEDIA kuwa timu yake haipewi nafasi kubwa ya kuibuka na ushindi kwenye mchezo huo kutokana na kiwango wanachokionyesha watani wao Simba lakini amewahakikishia mashabiki wao kuwa 'Mnyama' lazima akae muda ukifika.
Kocha huyo wa zamani wa klabu ya Mbeya city, alisema mechi hiyo wanaichukulia kawaida kama michezo mingine ya ligi na wachezaji wapo kamili kuhakikisha wanapata matokeo mazuri kwenye mtanange huo.
"Kama kuna watu wanafikiri tutapoteza mechi yetu dhidi ya Simba Oktoba mosi wanajidanganya, mashabiki wetu wasiwe na presha tuna wachezaji wazuri kuliko hao watani wetu muda ukifika kila mtu ataona kitakachotokea" alisema Mwambusi.
Kwa upande wake beki mpya wa mabingwa hao Andrew Vicent 'Dante' ambaye itakuwa mechi yake ya kwanza ya watani wa jadi , alisema kuwa mchezo huo utakuwa mgumu kutokana na timu zote kujiandaa vya kutosha pamoja na kufanya usajili mzuri ila wao wamejipanga kushinda.
Aidha Dante, alisema endapo atapata nafasi ya kucheza katika mechi hiyo atajitahidi kumdhibiti mshambuliaji mpya wa Simba raia wa Burundi Laudit Mavugo asilete madhara kwenye lango lao kutokana na umahiri wa nyota huyo.
Simba inaongoza katika msimamo wa ligi baada ya kujikusanyia alama 13 alama huku wakifuatiwa na Yanga wenye jumla ya alama 10 huku wakiwa nyuma kwa mchezo mmoja baada ya kushuka dimbani mara nne huku Simba akishuka dimbani mara tano.
JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.wabunifumedia.blogspot.com ku-install App ya wabunifumedia, bila ya kuingia websiteTweet@wabunifumediaonline, youtube@wabunifumediaonline TV, Fb@wabunifumediaonline, insta@wabunifumediaonline
Post a Comment