Mwenyekiti wa Kanisa la Good News for all Ministy Askofu Dr.Charles Gadi wakati kati akizungumza na wanahabari
wanahabari wakipiga picha
wanahabari
na wadau mbalimbali wakiwa kwenye maombi na Askofu Charles Gadi katika
ukumbi wa Habari maelezo jijini Dar es salaam(picha zote na Blog hii)
Mwenyekiti wa Kanisa la
Good News for all Ministy Askofu Dr.Charles Gadi ameipongeza Mamlaka ya Hali ya
Hewa kwa kutoa tahadhari mapema ya kunyesha kwa mvua kubwa mwanzoni mwa mwezi
novemba mwaka huu.
Askofu
Charles amezungumza
hayo leo jijini Dar es salaam wakati akizungumza na wanahabari ambapo
amesema
Mamlaka hiyo imefanya jambo jema kwa kutoa tahadhari ya kuwepo kwa mvua
kubwa kwani ni jambo litakalosaidia watu kujilinda maisha
yao pamoja na mali zao.
Amesema ni hatua kubwa
na yakimaendeleo kwa Mamlaka hiyo kwa kufanikisha kutoa taarifa ya hali ya hewa
itakayoweza kujitokeza nchini.
Askofu Charles amesema wao
kama viongozi wa dini lengo lao ni kuhakikisha wanafanya maombi yenye lengo la
kuzuia mvua ambazo zinazoweza kusababisha madhara kwa binadamu na mali zao.
“Vilevile mvua hizi ni
muhimu kwa mazao ya kudumu mfano kahawa,chai,korosho,katani,miti ya matunda
lakini pia bila kusahau malisho ya wanyama wa mwitu na wale wa kufugwa,pamoja
na mositu yake pia”amesema Askofu Charles
Hata hivyo wakiwa
pamoja na wanahabari wamemuomba Mungu kwa pamoja ili aweze kuepusha janga la
mvua za mafuriko.
Post a Comment