---------------------------------------------------------------------------
WAUMINI wa Kanisa la Waadventista Wasabato
(SDA) mtaa wa Chuo Kikuu uliopo
Conference ya Mashariki na Kati (ECCT) yenye Makao yake mkoani Morogoro,
wameshauria kusoma masomo ya Watafuta
njia na Wavumbuzi ili kuwa na kizazi kinachomjua Mungu kuanzia umri
mdogo, mwandishi mwandamizi Moris
Lyimo anandika.
Kwaya Kuu ya Kanisa la Waadventista wa Sabato Makongo Juu wakiimba wimbo muruwa wa `KUTETEREKA' wakati sikukuu ya Makambi kanisani hapo mwaka jana. Picha MORIS LYIMO kwa msada wa mtandao wa face book. |
Ushauri huo ulitolewa na Kiongozi Muadventista wa kanisa la SDA Makongo Juu, Geofrey Misana wakati akizungumza na waumini wenzake kupitia vipindi vya mchana katika sabato ya Mei 27, mwaka huu iliyoendeshwa na idara ya vijana ya mtaa huo.
Alisema tathimini inaonyesha kuwa idadi ya waumini wanaojitokeza kusoma masomo ya Watafuta njia (Master Guide) na Wavumbuzi (Adventure) pamoja na Kiongozi Muadventista hairidhishi licha ya juhudi za Kanisa kutangaza masomo hayo mara kwa mara.
“Kozi hizi ni muhimu kutokana na wajibu wa wahitimu
hao katika kanisa. Umuhimu wake unatokana na ukweli kwamba maandalizi ya watu
kumjua Mungu hufanywa na kundi hili kwa kuwafundisha vijana wadogo (PF) na
vijana wakubwa…kwa muktadha huu, msingi wa kanisa la Mungu hujengwa na watu
waliosomea kozi hizi, kufuzu na kutunukiwa cheti cha kufuzu,”alisisitiza
Misana.
Badala yake waumini wamekuwa wakikimbia kusoma
mafunzo hayo muhimu kwa visingizio mbalimbali jambo ambalo hajenga dhana ya
kukimbia kazi ya Mungu ambayo ni muhimu kwa kanisa la sasa na baadaye.
Kwa mujibu wa Kiongozi huyo Muadventista, kozi ya
Master Guide husomewa kwa miaka miwili ili kuwa mkufunzi na mlezi wa vijana
wadogo, Pathfinder (PF- Watafuta njia) na Wavumbuzi
(Adventure).
Kwa upande wa Kiongozi Muadventista husomewa kwa
mwaka mmoja kwa shabaha ya kuwa mlezi na mkufunzi wa Vijana Wakubwa wa kati ya
umri wa miaka 16 na kuendelea.
Ili kuthibitisha mwitikio mdogo wa waumini
kutoshiriki masomo hayo, alisema
Mkurugenzi wa Vijana wa ECCT aliwahi kuandaa kambi la vijana huko Msata mkoani
Pwani kwa lengo la kuendesha mafunzo hayo ingawa viongozi 3 pekee wa idara ya vijana kutoka mtaa huo ndio walioshiriki
ukilinganisha na mitaa mingine.
“Ukweli ni kwamba huduma za vijana zimepoa, shughuli
zao pia zimepoa, nawatia moyo tuamke tufanye kazi ya Mungu bila hofu kwani
ndiyo tuliyoitiwa…fikiria mimi ni mzee wa miaka 75, pamoja na kusoma kozi zote
mbili na kutunukiwa siwezi kuwa kiongozi wa vijana kwasababu viongozi wa vijana
wana umri wao,”alisema.
Alitoa wito kwa waumini hususan vijana kujitokeza
kwa wingi ambapo kupitia ibada hiyo zaidi ya watu 15 wengi wao wakiwa vijana
walijitokeza na kuandikishwa kusoma masomo hayo.
Mungu amekuwa akitumia Geofrey Misana maarufu kama
mzee Misana kanisani hapo kufanya shughuli mbalimbali za kanisa. Alihitimu kozi
ya miaka miwili ya Master Guide mwaka 2009 na Mei 20 mwaka huu alitunukia kwa
mara nyingine tunu ya kozi ya mwaka mmoja ya Kiongozi Muadventista, hafla
iliyofanyika huko Conference ya Kusini
Mashariki (SECT).
Amekuwa pia akitumika kama mzee wa kanisa na mlezi
katika kundi la SDA Makongo Juu Kaskazini na kabla ya kuhamia Makongo Juu,
miaka ya nyuma amewahi kuwa mzee wa kanisa katika makanisa mbalimbali ikiwamo
Magomeni SDA.
Historia kamili ya maisha yake katika SDA itaelezewa
katika ukurasa huu toleo lijalo ikiwamo historia ya Kanisa la SDA Makongo Juu. Karibu.
------------------
Habari
hii imeandaliwa na idara ya mawasiliano
ya Kanisa la SDA Makongo Juu. Mwandishi wetu, Moris Lyimo ni mmoja wa Washiriki wa kanisa hilo na mjumbe wa idara
hiyo.
-----------------------
Post a Comment