NA TATU RAMADHAN
SHIRIKA la Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (Dawasco)
limesema kuwa litawafikisha mahakamani wadaiwa wote ambao hawajalipa bili ya
maji kwa zaidi ya mwezi mmoja.
Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo,
Cyprian Luhemeja imeeleza kuwa ambao wana madeni ya bili za maji kwa zaidi ya
mwezi mmoja waliea kabla ya Julai 6, mwaka huu.
Luhemeja amesema yeyote atakayeshindwa kulipa deni lake
ndani ya muda huo atalazimika kulipia bili yake, pamoja na gharama zote za
kuendesha kesi pamoja na faini kwa wale watakaofikishwa mahakamani .
”Wateja wote wanaohudumiwa na Dawasco katika Mkoa wa Dar es
Salaam na Mkoa wa Pwani, wanaodaiwa kwa zaidi ya mwezi mmoja, tunawataka walipe
bili zao za maji, vinginevyo Dawasco itawafikisha mahakamani,” amesema.
Luhemeja ameongeza kuwa, “Kumbuka Dawasco haipokei malipo
taslimu, malipo yote yafanyike kupitia huduma za kibenki, mawakala wa selcom na
Maxcom, pamoja na mitandao yote ya simu ambayo imeidhinishwa,”.
Aidha ametoa wito kwa Wananchi wote kutoa ushirikiano wakati
wa zoezi hilo.
Mwishooo
Post a Comment