Halloween party ideas 2015
Image

Na Issa Ramadhani 
MAMLAKA ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania (TCRA) imevipa onyo na kuvipiga faini vituo viwili vya televisheni na kimoja cha redio kwa kukiuka maadili ya utangazaji.
Vituo hivyo ni  pamoja na ITV, Clouds Tv na Clouds Fm Radio, vyote vya jijini Dar es Salaam, ambavyo kwa ujumla vimetozwa  faini ya Sh milioni 19 kama adhabu ya kukiuka madaili ya vyombo vya habari na kanuni zake.
Akizungumzia juu ya kutoa uamuzi uliofikiwa na Kamati ya Maudhui ya TCRA, Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Joseph Mapunda ,alisema vituo hivyo vilibainika kukiuka Kanuni za Huduma za Utangazaji na kuvitaka kuwa wasimamizi wazuri wa vipindi vyao katika kudumisha m
aadili ya vyombo vya habari katika kuhabarisha umma.


Mapunda ,alisema kamati hiyo imekipa onyo na kukipiga faini ya Sh milioni 10, kituo cha televisheni cha ITV kwa makosa mawili.
Kosa la  kwanza,  ni kupitia kipindi chake cha Kumekucha 
kilichoendeshwa  Juni 15,2016 mwaka huu ka
ti ya majira ya  saa 1:00 na 1:30 asubuhi ambapo mtangazaji alifanya mahojiano na Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa ,kuhusu mwenendo wa Bunge la Bajeti, na Mchungaji Msigwa alitamka maneno ya kashfa dhidi ya Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , Dk Tulia Ackson.
"Katika mahujiano hayo ,mtangazaji hakuchukua jitihada za kumwomba Mheshimiwa Peter Msigwa kufuta lugha ya matusi aliyoitumia, "bali alionekana akifurahia na kuendelea kumuuliza maswali mengine,” alisema Mapunda.
Katika kosa la pili, Mapunda alisema kituo hicho kilikiuka kanuni katika taarifa ya habari iliyosomwa mnamo Juni 23 , 2016 kati ya mishale ya  saa 1:00 na 2:00 asubuhi, kilitangaza taarifa ya msichana wa miaka 16 aliyebakwa na kupewa ujauzito na walitumia utambulisho wa msichana huyo kwa jina na shule anayosoma kitu ambacho kimaadili ya habari ni kinyume na sheria za utangazaji .
Akitoa utetezu huo juu ya taarifa hizo zilizowafanya kuwaweka hatiaani, Mwakilishi wa ITV, Stephen Chuwa, alikiri kuwa Mchungaji Msigwa alitoa maneno ya kashfa na hakutembea katika ahadi yake ya kutomkashifu mtu.
Aidha, alisema kama mtangazaji angemuomba kufuta kauli, basi mjadala huo ungekuwa mkubwa zaidi. Alisema watachukua hatua za kumwomba radhi Dk Tulia kutokana na kashfa hiyo.
Kwa upande wa Kituo cha Clouds Tv, kituo hicho kimepewa onyo na kupigwa faini ya Sh milioni nne 
ambazo wanapaswa kulipa ndani ya siku 30 kuanzia siku ya hukumu.



Mapunda, alisema kituo hicho kupitia kipindi chake cha Hip Hop, kilichorushwa kati ya saa 8:00 mchana na 12:00 jioni, kilirusha video ya nyimbo za Asanteni kwa Kuja wa Mwana FA na Break It Down wa Lil Bebbie, ambazo zinadhalilisha utu wa mwanamke.
Aidha, Clouds Fm pia imepewa onyo na kupigwa faini ya Sh milioni tano kwa vipindi vyake vya ‘Power Breakfast’ na Jahazi kwa walikiuka kanuni za utangazaji.

Alisema katika kipindi cha Jahazi cha Mei 9, kilichorushwa kati ya saa 10:00 hadi 12:55 jioni, watangazaji walisikika wakishabikia taarifa ya mtu kufanya ngono na mbuzi, ambako walieleza kuwa mtu huyo na mbuzi ni kama mtu na mpenzi wake, jambo lililoonesha wanahamasisha vitendo hivyo.
 Aidha, Mei 18, mwaka huu katika kipindi cha Power Breakfast, kilichorushwa kati ya sa 12:00 na 4:00 asubuhi baada ya kusoma taarifa ya Hospitali ya Taifa Muhimbili kuhusu kupandikizwa kwa sehemu za siri za kiume kwa mtoto wa miaka mitatu, aliyezaliwa akiwa hana na kulelewa kama mtoto wa kike.


JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.wabunifumedia.blogspot.com ku-install App ya wabunifumedia,  bila ya kuingia websiteTweet@wabunifumediaonline, youtube@wabunifumediaonline TV, Fb@wabunifumediaonline, insta@wabunifumediaonline




Post a Comment

Theme images by Maliketh. Powered by Blogger.