Halloween party ideas 2015
Image

Na Yusuph Mwamba

NGULI wa Masumbwi ya uzito Duniani, Manny Pacquiao, amethibitisha kurejea tena ulingoni baada ya tetesi zilizo zagaa za mwanamasumbwi huyo, kustaafu mchezo huo mwaka huu.


Hayo yamethibitishwa leo na Meneja wa Pacquiao, Michael Kncz, baada ya kusema kuwa kila kitu kinakwenda sawa kwa mujibu wa mikataba waliosaini mapema ya wikii na kuthibitisha pambano hilo linaweza likapigwa kati ya Septemba 8 kwa 10 katika Jiji la Los Angeles Nchini Marekani.

Pacquiao, mwenye umri wa miaka 37, Raia wa Kifilipino, alifanikiwa kushinda tuzo 8 katika michezo yake aliyoicheza, amefungaka na kuweka wazi mipango yake juu ya kurejea Ulingoni.


Akizungumza na Waandishi wa Habari, katika mkutano uliofanyika Mjini Manila, mwanamasumbwi huyo alikutana na Msimamizi wa pambano hilo, Bob Arum, nakuthibitisha kurejea ulingoni

" Kweli natarajia kupanda Ulingoni  pambano letu linatarajiwa kupigwa kati ya Septemba 8 kwa 10 katika pambano la WBO, Welterweight Champion ". Alisema Pacquiao

Pacquiao, alistaafu mchezo wa Ngumi, baada ya kushinda pambano lake la April dhidi ya Mmarekani, Timothy Bradley, na kuamua kujikita zaidi katika siasa.

Nguli huyo , alichaguliwa kuongoza wananchi wa Philipino akiwa na cheo cha Senator, na baada ya kuchaguliwa alitangaza kutojihusisha na maswala ya Ngumi tena.

Juu ya kurudi tena Ulingoni, Pacquiao, amesema hawezi kuacha mchezo wa Ngumi kwa kuwa anatambua mchango wake na pia ni mchezo ambao unamuingizia kiasi kikubwa cha fedha kuliko mmshara wa Serikalini.

"Naisadia Familia Yangu pamoja na mke wangu, pia na wale wote wanaonizunguka mimi nimekuwa msaada wao mkubw sana ni mchezo ambao na uheshimu sana ".Aliongeza Pacquiao


JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.wabunifumedia.blogspot.com ku-install App ya wabunifumedia,  bila ya kuingia websiteTweet@wabunifumediaonline, youtube@wabunifumediaonline TV, Fb@wabunifumediaonline, insta@wabunifumediaonline




Post a Comment

Theme images by Maliketh. Powered by Blogger.