ZIKIWA zimepita takribani majuma kadhaa tangu kwa ,Dr John Pombe Magufuli, kuteuliwa kuwa mwenyekiti mpya wa chama hicho kwa muda wa miaka 10, kwa kukabidhiwa kijiti na aliyekuwa mwenyekiti wa zamani aliyemaliza muda wake , Dr Jakaya Kikwete, leo Dr Magufuli ameingia rasmi mjengoni huku akiwajaza matumaini lukuki wanachama wa chama hicho pamoja na Watanzania kwa ujumla.
Rais Dkt John Pombe Magufuli aliyepigiwa kura na Wajumbe wa Mkutano Mkuu maalum na kuibuka na kura zote za ndio kutoka kwa Wajumbe 2398 na hakuna kura zilizokuwa zimeharika.
Akizungumza na waandishi wa habari, katika Mkao makuu ya Chama hicho, Lumumba, Dar es salaam leo, Dr Magufuli, amewataka Watanzania waachanae na siasa uchwara na badaa yake wajikite katika kujenga umoja na mshikamano na kumpa ushirikiano katika kuhakikisha Tanzania inafanikiwa ktika nyanja zote za Uchumi, siasa na Elimu.
Kuhusu Serikali kuhamia Dodoma, Dr Magufuli, amesema kuwa atahakikisha Serikali inahamia Dodoma na kupisha Jiji la Dar es salaam kuwa jiji la kibiashara za Kimataifa.
Katika maswala ya miundombinu, Dr Magufuli, amesema kwa sasa wapo katika mpango wa kutengeneza Fly Road maeneo ya Tazara ,na mpango huo unatarajiwa kumalizik mapema mwaka huu na kutanua wigo wa njia za Reli ili zitumike kwa kurahisha huduma ya biashara na kijamii nje na ndani ya Nchi
Aidha, Dr Magufuli, amesema kuwa katika kuhakikisha urahisishaji wa foleni kwa Jiji la Dar es salaam, wapo katika mpango wa kuongeza Magari ya Mwendokasi ili kupunguza adha ya usafiri Jijini.
Licha ya kuhakikisha Serikali yke inakuwa na mafnikio na maendeleo, amegusia swala la kodi na kusema lazima watu walipe kodi ili kuingiza pato la Taifa ili kuchochea maendeleo ya Taifa
"Taifa lolote ili liendelee ni lazima watu wake walipe kodi, ili kufanikisha mipango ya Serikali kama hutolipa kodi ni wazi kuwa utakwamisha maendeleo ya Taifa lako, nawaagiza TRA na TCRA mhakikishe mnakusanya kodi za kutosha ili tufikie malengo tuliojiwekea na ahadi tulizo waahidi wananchi katika kipindi cha kampeni, nimechaguliwa na masikini basi nitawatumikia masikini".Alisema Magufuli
Pia , Dr Magufuli, amegusia swala la Majipu nakusema kuwa ataendelea kutumbua majipu mapa ahakikishe wae wote wanochukulia Tanzania ni shamba la bibi , basi wajue nchi hii ina misingi na sheria zake na sio kujichukulia fedha kiholela
"Majipu nitayatumbua sana, ili twende sawa na katika chama changu cha CCM, kuna majipu pia , kunawale waliokimbia chama mapema kwa kuogopa kutumbuliwa nawajua na nitawatumbua na wale walio salia pia nitawatumbua, na nimesikia Jengo la Vijana kuna majipu , vinaja wanajimilikia nyumba kiholela wajiandae kuwajibika na kusema kodi wanazipeleka wapi, kasi hii tukiungana kwa pamoja tutafika".Aliongeza Dr Magufuli
Pia, Dr Magufuli, amempongeza sana aliyekuwa mwenyekiti wa wa chama hicho na Rais mstaafu aliyemaliza muda wake kwa awamu ya nne, Dr Jakaya Kikete, kwa kusimamia haki, upendo na misingi ya chama kwa muda wote aliokuwa madarakani akiwa ameshika nyadhifa hiyo.
Dr Magufuli, alienda mbali zaidi na kuwashukuru pia wle wote waliokuwa nyuma ya Dr Jakaya Kikwete. akiweno Rais mstaafu wa awamu ya pili, Ally Hasssan Mwinyi, makau mwenyekiti w Bara na Zanzibar na viongozi wote waliopambana kuhakikisha chama cha mapinduzi kianashika dora kw awamu ya tano.
JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.wabunifumedia.blogspot.com ku-install App ya wabunifumedia, bila ya kuingia websiteTweet@wabunifumediaonline, youtube@wabunifumediaonline TV, Fb@wabunifumediaonline, insta@wabunifumediaonline
Post a Comment