Halloween party ideas 2015
Image

Na Issa Ramadhani, Dar es salaam

MSHAMBULIAJI wa zamani  Klabu ya Soka ya Aston Villa, Dalian Atkinson, amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika Mji wa Meadow Close, baada ya shambulio la Polisi liliotokea katika Mji huo Nchini Uingereza.

Dalian, mwenye umri wa miaka 48, aliyepigwa risasi baada ya shambulio hilo la Polisi dhidi ya watu waliodaiwa kuwa ni Majambazi katika ukumbi huo wa Starehe, alikimbizwa katika Hospitali ya Princess Royal katika mji wa  Shropshire kujaribu kupatiwa matibabu lakini hali hiyo ilishindikana na kuchukua dakika 90 tu baadaya ya kupoteza maisha yake.


Mwanandinga huyo, aliweka rekodi ya mwaka 1994, ya kuifungia timu yake ya Aston Villa katika ufunguzi wa kombe la Ligi kuu na kuibuka na ushindi dhidi ya klabu ya Manchester United katika Dimba la Wembley.


Katika kuonesha uhodari wake wa kufumania nyavu, Dalian, pia alifanikiwa kuwa mfungaji wa kwanza kufumania nyavu katika ufunguzi wa ligi mwaka 1992/1993.




Licha ya kuicheza Aston Villa, pia alijiunga na timu ya Taifa ya Vijana ya Uingereza na kufanikiwa kuiwezesha timu yake kuibuka na ushindi wa jumla ya mabao 4-1 dhidi ya timu ya Vijana ya Jamhuri ya Ireland mwaka

 1990.



Atkinson, pamoja na kuichezea klabu ya soka ya Aston Villa, pia miongoni mwa timu nyingine alizowahi pata kuzichezea ni pamoja na klabua ya soka ya Ipswich, Sheffield Wednesday, Real Sociedad, Fenebahce na klabu ya Manchester City ya Jijini London Uingereza.


Akizungumzia juu ya kifo hicho, mkuu wa kitengo cha kutoa huduma cha Mashariki ya kati ya hospitali ya Princes ambapo alikimbizwa mwanandinga huy baada ya kupigwa risasi , amesema pamoja na jitihada zote zilizo fanyika lakini ilishindikana na kupelekea Nyota huyo kupoteza Maisha yake.


"Pamoja na jitihada nyingi zilizo fanywa na Madaktari wetu lakini ilishindikana kuokoa maisha yake na hatimaye kufariki Dunia katika Hospitali hiyo muda mfupi baada ya kufanyika kwa jitihada za matibabu". Alisema mkuu wa kitengo hicho

Mshambuliaji Atkinson, akiwa katika moja ya majukumu ya imu yake ya Real Sociadad baada ya kuibuka na  ushindi wa 3-2 dhidi ya Real Madrid katika ligi kuu ya Hispainia 

Tukio hilo mashambilizi ya Polisi  dhidi ya wahalifu sio kwa mara ya kwanza kutokea Katika mji huo, hata mwishoni mwa mwaka 2015 zaidi ya watu 10329 walishikiliwa na Polisi baada ya kutumia nguvu  ng zaidi katika mji wa Uingereza na Walesi lakini kwa sasa limeonekana kuzidi kwa 2% ukilinganisha na mwaka 2015


JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.wabunifumedia.blogspot.com ku-install App ya wabunifumedia,  bila ya kuingia websiteTweet@wabunifumediaonline, youtube@wabunifumediaonline TV, Fb@wabunifumediaonline, insta@wabunifumediaonline


Post a Comment

Theme images by Maliketh. Powered by Blogger.