Halloween party ideas 2015
Image

Na Yusuph Mwamba

Soka ni mchezo unaopendwa na watu takribani Dunia kote, mchezo huu ni mchezo ambao umewanufaisha wachezaji wengi na timu nyingi zimekuwa matajiri shauri ya mchezo huu, pia umekuwa ni ajira kwa vijana na kupelekea mtu kujikimu kimaisha.



Licha  ya kuwa ni ajira lakini sifa za mchezo huu bwana umekuwa na ushindani wa kila aina, ushindani huu unaanzia katika Timu, wachezaji, Viwanja, wadhamini, pamoja na mikataba ya wachezaji ila kubwa zaidi katika mchezo na jambo ambalo wazungu haswa ndilo linalowapelekea kuwa na maendeleo zaidi ya wa Afrika ni suala la Kuvunja rekodi hicho ndicho kimenipelekea kuandika makala hii.






Leo tunakwenda kumwangalia Mshambuliaji Nguli aliyekuwa akikipiga kunako klabu ya West Ham na Timu ya Taifa ya 
Uingereza, Sir Geoffrey Charles Hurst, unaweza kuwazungumzia Maradona, Pele, Ronaldo Delima, Ronaldinho, Zidane pamoja na wakali wa soka wa karne hii yani Cristian Ronaldo pamoja na Lionel Mess lakini kwa Sir Giff Hurst anaonekana kuwazidi kete Nyota wote hapo juu baada ya kuweka Rekodi ya kupiga Hat Trick katika mchezo mmoja wa fainali ya Kombe la Dunia .




Mwaka 1966, Timu ya Taifa ya Uingereza wakiwa wenyeji wa michuano hiyo ya kombe la Dunia, walifanikiwa kuibuka mabingwa baada ya kuwafunga Timu ya Taifa ya Ujerumani Magharibi kwa jumla ya mabao 4-2 kwa muda wa ziada (Extra time).

Hadi dakika 90 za mchezo zinakamilika timu zote zilitoshana nguvu ya mabao 2-2. Huku shujaa wa England alikuwa, Sir Geoffrey Hurst, aliyefunga mabao matatu " hat-trick"akiweka rekodi a mchezaji pekee kufunga Hat trick katika mchezo wa fainali za kombe la Dunia katika dimba la zamani la Wembley Jijini London Uingereza.

Mwaka 1968, alifanikiwa kucheza tena katika michuano ya fainali ya kombe la Euro 1968 na mwaka 1970 alishiriki kwa mara ya mwisho kombe la Dunia akiwa na timu yake ya Taifa ya Uingereza

Staa huyo wa Uingereza licha ya kujipatia mafanikio hayo kede wa kede, pia alishawahi kuvichezea vilabu mbalimbali Barani Ulaya kabla ya kutundika Daluga lake na kuendelea na soka katika upande wa Ukocha, miongoni mwa timu alizowahi kuzichezea ni pamoja na West Ham, Stoke City, West Bomwich.

Maisha yake na safari yake ya Soka ya Sir Hurst, yalianzia kunako timu ya Vijana ya klabu ya soka ya West Ham United, na baada ya kuonesha kiwango cha hali ya juu na kufanya kuleta ushawishi wa kuoredheshwa katika kikosi cha timu ya wakubwa ya West Ham mnamo mwaka 1957-1972, wakati akiwa na timu ya hiyo ndipo alipo pata nafasi ya kujiunga na kikosi cha vijana cha Timu ya Taifa ya Uingereza.

Mwaka 1964, alifanikiwa kunyakuwa kombe la FA Cup, akiwa na klabu yake ya West Ham United

Akiwa na timu ya wakubwa ya West Ham United, Sir Hurst, alifanikiwa kucheza jumla ya michezo 411 na kufunga jumla ya magoli 180, baada ya kumalizika kwa mkataba wake nyota huyo alijiunga na klabu ya soka ya Stoke City mwaka 1972-1975  kwa mauzo ya Paundi milioni 80000 kwa mkataba wa miaka mitatu  huku akicheza jumla ya michezo 108 na kufunga magoli 30.

Baada ya kumalizika kwa mkataba wake, nyota huyo alitolewa kwa mkopo na klabu yake na kumpeleka kunako klabu ya soka ya Cape Town City huko nako pamoja na kutofanikiwa kudumu kwa muda mrefu alicheza jumla ya michezo 6 na kufunga magoli 5, kabla ya kutupa karata yake kunako klabu ya soka ya West Bromwich mwaka 1975-1976 huku akicheza jumla ya michezo 10 na kufunga magoli 2.

Mwaka 1976, alijiunga na klabu ya soka ya Cork Celtic ya Jamhuri ya Ireland huko nako hakukumpa mafanikio akijikuta akifumania nyavu mara 3 katika michezo 3 aliyochezea kunako klabu hiyo, baada ya hapo alipiga hodi kunako klabu ya Seattle Soundes ya Marekani huko nako alicheza jumla ya michezo 23 na kufunga magoli 8.

Mwaka  1979-1981, alifundisha klabu ya soka ya Chelsea baada ya hapo alijiunga kuifundisha klabu ya soka ya Kuwait SC mwaka 1982-1984

 Ukiangalia hizo rekodi yake utagundua mpaka hapo alifanikiwa kucheza jumla ya michezo 561 na kufumania nyavu mara 228 katia historia yake ya soka.


TIMU YA VIJANA YA UINGEREZA

Mwaka 1959, Sir Geoff, alifanikiwa kuitwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Vijana ya Uingereza huku akiwa na  miaka 18, lakini mwaka huo huo katika kikosi hicho alifanikiwa kucheza jumla ya michezo 6 kati ya michezo hiyo hajafanikiwa kufunga hata goli.

TIMU YA VIJANA CHINI YA UMRI WA MIAKA 23
Huku akishindwa kufanya vyema zaidi katika timu ya vijana ya Uingereza lakini bahati nyingine ikamwangukia Nyota huyo na kuitwa kwenye Timu ya Taifa ya Vijana chini ya umri wa miaka 23 lakini huko nako licha ya kukosa namba kwa muda mrefu lakini alicheza jumla ya michezo 4 na kufunga golin1. 

Mwaka 1964, alifanikiwa kufunga ndoa na mkewe Judith na walifanikiwa kupata jumla ya watoto watatu, Baba yake na  Sir Hurst ajulikanaye kwa jina la Charlie Hurst, pia alishawahi kuwa mchezaji wa nafasi ya ulinzi wa kati, miongoni mwa timu alizowahi kuzitumikia ni pamoja na Bristol Roves. Oldham Athletic. na klabu ya soka ya Rochdale.

Huyo ndiye Nyota aliyeweka rekodi ya kupiga Hat Trick katika fainali ya michuano ya kombe la Dunia Tangu kuanzishwa kwake  labda pengine tutegemee nyota wengine kuja kuvunja rekodi hiyo katiak mpira lolote linaweza kutokea kwani wenzetu wamekuwa wakiangalia sana rekodi kuliko kitu kingine chochote Duniani katika aina yoyote ya mashindano

JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.wabunifumedia.blogspot.com ku-install App ya wabunifumedia,  bila ya kuingia websiteTweet@wabunifumediaonline, youtube@wabunifumediaonline TV, Fb@wabunifumediaonline, insta@wabunifumediaonline









Post a Comment

Theme images by Maliketh. Powered by Blogger.