Na Yusuph Mwamba
MENEJA wa Klabu ya soka ya Chelsea FC, Antonio Conte., amefunguka rasmi na kumpigia debe Nahodha wa klabu yake John Terry, kurudishwa timu ya Taifa ya Uingereza.
Conte, amezungumza hayo kufutia matokeo mabaya na kiwango kibovu kilichooneshwa na Timu hiyo ya Taifa katika michuano ya fainali ya Euro2016 iliyomalizika mwezi uliopita Nchini Ufaransa na kutolewa robo fainali dhidi ya Ireland kwa jumla ya 2-1, huku kukidaiwa kukosa wazalendo wenye mapenzi ya kweli na nidhamu kwa Taifa hilo.
Ikumbukwe kuwa, Nahodha huyo wa Chelsea, alitundika daluga lake la kuitumikia Timu yake ya Taifa ya Uingereza mwaka 2012, lakini kukosekana kwa muungano mzuri wa wachezaji na ukosefu wa Mlinzi mzuri hiki ndicho kitu kilichopelekea Sam Allardyce kumrudisha tena nahodha huyo kundini.
Kocha huyo wa Uingereza, kwa sasa anajiandaa kumuorodhesha nahodha huyo katika kikosi cha kwanza kinachotarajia kujianda na michuano ya kuwania nafasi ya kufuzu fainali ya kombe la Dunia dhidi ya timu ya Taifa ya Slovakia mchezo huo unaotarajiwa kupigwa Septemba 4 mwaka huu.
Allardyce, amesema kuwa kwa sasa anaangalia uwezekano wa kukaa naye nahodha huyo meza moja ili kuangalia uwezekano wa kumrejesha nahodha huyo katika nafasi yake katika kuleta heshima ndani ya kikosi hicho na Taifa zima kwa ujumla.
"Mimi ni kocha mzoefu katika kufundisha Timu ya Taifa, ninauelewa na ualedi wa kutosha najua hii hali ilitengenezwa muda mrefu na maelewano mazuri ya wawii hao ndio ilipelekea maamuzi yao kuwa rahisi, huu ni uamuzi mzuri na njia nzuri katika kuokoa jahazi la Uingereza".Alisema Conte
"John Terry ni mtu mwenye uelewa mkubwa sana kipindi cha mafunzo na amekuwa ni mtu anaye fanya kazi kwa bidii na kwa moyo wote, nina furaha kubwa sana kwa kwa kukubali ombi langu, lakini sio kwangu bali kwa manufaa ya Timu ya Taifa, ni jambo zuri walioafikiana kati ya Sam Allardyce na John Terry".Aliongeza Conte
Licha ya ushindi wa mwisho wa 78 ambao John Tery, alifanikiwa kushinda akiwa na timu yake ya Taifa dhidi ya timu ya Taifa ya Moldova wa mabao 5-0 lakini hakuweza kujumuishwa katika kikosi hicho cha Uingereza chini ya aliyekuwa meneja timu hiyo Roy Hodgson.
JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.wabunifumedia.blogspot.com ku-install App ya wabunifumedia, bila ya kuingia websiteTweet@wabunifumediaonline, youtube@wabunifumediaonline TV, Fb@wabunifumediaonline, insta@wabunifumediaonline
Post a Comment