Na Issa Ramadhani
WAZIRI wa habari na utamaduni , sanaa na michezo, Nape Nnauye, amevifungia rasmi vituoviwili vya habari Magic fm na Radio 5 kwa kile kinachodaiwa kukiuka kanuni na sheria za maadili ya vyombo vya habari.
Akizungumza na waandishi wa Habari jana Jijini Dar es salaam, Nape, amesema kuwa uamuzi huo umekuja baada ya kujiridhisha kuwa mwenendo wa vituo hivyo umekiuka mashariti ya kanuni zilizopo.
Waziri Nape, amesema kuwa, kwa mamlaka aliyopewa, chini ya kifungu cha 28(1) cha sheria ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania 2013 ameamua kuvifungia vituo hivyo kwa siku zisizo julikana hadi hapo kamati ya maudhui itkapokutana na kuwasikiliza kwa kina zaidi na kushauri hatua zaidi za kuchukua kwa mujibu wa kanuni a utangazaji 2015.
Aidha,Waziri Nape, amesema kuwa kosa lililopelekea kufungiwa kwa kituo cha Radio 5, limetokana na kipindi chake cha matukio kilichorushwa tarehe 25, Agosti, 2016, saa 2:00-3;00 Usiku ambapo katika kipindi cha mahojiano mgeni rasmi alikuwa Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, alitoa maneno ya uchochezi.
Amesema kuwa, licha ya Mbunge huyo kutoa lugha hizo, Watangazaji wa kipindi hicho walishindwa kumsahihisha jambo analodai limekwenda kinyume na sheria ya Utangazaji.
Kwa upande wa Radio Magic, kipindi cha Morning Magic, kilichorushwa tarehe 17, Agosti, 2016, saa 1:00-2:30 katika Kipengele cha Kupanga Rangi, Watangazaji wa kipindi hicho walisikika wakitoa maneno anayoyaeleza ni ya ki uchochezi.
"Watangazaji wa Magic . walisema kama Rais anavunja katiba sasa wananchi wa chini wafanyaje . nao lazima watafanya hivyo". Alisema Nape
JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.wabunifumedia.blogspot.com ku-install App ya wabunifumedia, bila ya kuingia websiteTweet@wabunifumediaonline, youtube@wabunifumediaonline TV, Fb@wabunifumediaonline, insta@wabunifumediaonline
Post a Comment