Halloween party ideas 2015
Image

Na Mwandishi wetu, Dar                                                           WAKATI kilele cha maadhimisho ya siku ya Saccos Duniani, yakikiwa yamemalizika ambapo Kitaifa yamefanyika Jijini Dar es salaam huku ikiwa yamefanyika mara 6 Jiji la Dar es salaa huku yakifanyika kwa mara 1 nje ya Jiji hili, lakini tumeshududia vikundi mbalimbali vya ushirika ambavyo vilileta maonesho yao licha ya kuwa na changamoto za hapa na pale.




Miongono mwa vikundi vya Ushirika vya vyama vya kuweka na kukopa (SACCOS)  vilivyo fanya vizuri ni pamoja na TANESCO SACCOS ambacho kilijinyakulia tuzo ya cheti pamoja na kikombe baada ya kutawazwa kuibuka kidedea katika mashindano hayo wakifuatiwa na Ndugumbi Saccos pamoja na Bandari Saccos kuibuka washindi wa tatu.







MISINGI YA CHAMA

DIRA
Kuwa Saccos inayoongoza nchini Tanzania inayokidhi mahitaji ya kijamii na kiuchumi ya wanachama wake kupitia husuma bora za kifedha.

DHAMIRA
Kuhamasiha na kuimarisha ukusanyaji wa akiba, hisa na amana kupitia utoaji wa elimu ya mikopo na huduma bora kwa wateja wake.


Bidhaa ambazo zilitolewa na Tanesco Saccos, katika siku ya kilele cha maadhimisho cha siku ya Saccos Duniani iliyomalizika Jijini Dar es salaam, oktoba 13 mwaka 2016.

Tanesco Saccos ni Chama cha Ushiriika wa Akiba na Mikopo cha Wafanyakazi wa Shirika la Umeme TANESCO. Wafanyakazi wa TANESCO SACCOS, Wastaafu wa TANESCO, wafanyakazi wa muda maalum wa TANESCO, Wafanyakazi wa Wizara ya Nishati na Madini
      na Kampuni au Taasisi zilizo katika sekta ya Nishati ambao wamejiunga pamoja kwa hiari kwa madhumuni ya kuinua na kustawisha hali ya uchumi nan maisha yao kwa kuanzisha na kumiliki TANESCO SACCOS kwa kufuata sheria, kanuni na taratibu za vyama vya Ushirika.  

                                             

MALENGO
Chama hiki kilianzishwa kikiwa na lengo la kuhamasisha wanachama wake kujenga tabia ya kujiwekea akiba na kuwapa fursa ya kukopa kwa riba nafuu kwa ajili ya kukidhi magitaji mbalimbali ya kijamii na kiuchumi. 
MAADILI
WALEDI (PROFESSIONALISM)
Kuwa na wafanyakazi walioelimika na wenye ujuzi na mtazamo chanya juu ya Dira, Dhamira, na malengo ya Chama ili kutoa huduma kwa wanachama         


UWAZI (TRANSPARENCY)
Chama kitawahudumia wanachama kwa uwazi na kujitahidi kuimarisha mawasiliano baina yake na wanachama

KUFANYA KAZI PAMOJA
Chama kimejipanga kusimamia dhana ya uwajibikaji wa pamoja ili kufikia malengo tarajiwa

UANACHAMA
Chama cha Ushiriuika wanachama wa TANESCO SACCOS uko wazi kwa wafanyakazi wa shirika la umeme Tanzania (TANESCO) bna wafanyakazi wa TANESCO SACCOS, Wastaafu wa TANESCO, Wafanyakazi wa muda maalumu wa TANESCO, Wafanyakazi wa Wizara ya Nishati na Madini na Kampuni au Taasisi zilizo katikan sekta ya Nishati.


MIKOPO
Chama kinatoa mikopo kwa wanachama wake kwa kufuata Sera ya mikopo ambayo iko wazi kwa kufuata utaratibu wa kwanza kuleta maombi ndio wakwanza kuhudumiwa

AINA ZA MIKOPO
1:MKOPO WA MAENDELEO
Mkopo huu unatolewa mara tatu ya akiba za mwanacham

a na unarejeshwa ndani ya kipindi kisichozidi miezi 48. Riba ya mkopo huu ina asilimia 1.375 kwa mwezi juu ya baki ya mkopo.

2:MKOPO WA DHARURA 
Unatolewa ili kukidhi mahitaji ya dharura ya mwanachama kwa kiwango kisichozidi shilingi milioni mbili na kurejeshwa ndani ya miezi sita kwa riba ya asilimia mbili kwa mwezi ya baki ya mkopo

3:MKOPO WA ELIMU
Unatolewa kulipia ada kwa mwanachama au tegemezi wake. Kwa kiwango kinacholingana na mshahara/ pensheni ya mwezi ya mwnachama na kurjrsha ndani ya miezi 6au kiwango kinacholingana na mara mbili ya mshahara/ pensheni ya mwezi na kurejesha ndani ya miezi 12 kwa riba ya 5%

HUDUMA NYINGINEZO
1:PAPO KWA PAPO
Hii ni huduma ya matangulizi ya mshahara kwa mwanachama na hutolewa kati ya tarehe 10-20 na makaton kufanyika mara moja katika mwezi unaofuata. Kiwango cha juu kwa huduma hii ni shilingi 200000/= na riba ya 10%

2:RAMBI RAMBI KWA WANACHAMA
Chama kinatoa huduma za rambi ramvbi kwa mwanachama atakayefiwa na mke/mume au mtoto. Rambi rambi hii ina nia ya kumfariji mwanachama katika kipindi kigumu cha kumpoteza mpendwa wake
Kwa mwanachama anayefiwa na mke/mume/mtoto atapatiwa rambi rambi ya shilingi 400000/= na ikitokea mwanachama mwenyewe amefariki chama kitatoa rambi rambi ya shilingi 700000/= kwa warithiwa mwanachama husika.

MFUKO WA TAHADHARI
Chama katiaka mpango wake wa kuwajali wanachama na kulinda mali za chama kimneanzisha mfuko wa tahadhari wa kukinga mikopo inayotolewa kwa wanachama kwa kuzingatia vigezo mbalimbali. Mfuko huu utakinga mikopo yote inatolewa na chama, nia ikiwa ni kuwaweka huru na madeni wanachama wote watakaofikwa na majanga yalianishwa katika sera za mfuko wa tahadhari, fedha za mfiko huu zinatokana na tozo katika mikopo inayotolewa na chama
Mkopo wa maendeleo utakatiwa tozo ya asilimia 0.06 kwa kiasi na muda wa mkopo
Mkopo wa Elimu na Dharura itakatiwa tozo ya asilimia 0.003 kwa kiasi na muda wa mkopo

Mwanachama atanufaika na huduma zifuatazo iwapo atafikiwa na majanga yaliyoainishwa katika sera za mfuko huu;
(a).Kiasi kitakachokingwa -Baki ya mkopo wa mwanachama aliyochukua kitafidiwa 
(b).Mafao ya mazishi-Ikitokea mwanachama aliyechukua mkopo akafariki mfuko utalipa shilingin 800000/= na iwapo atafiwa na mwenza mfuko utatoa kiasi cha shilingi 200000/= kama gharama ya mazishi kwa kufiwa.


WAHUSIKA WA MFUKO HUU
Wahusika wa Mfuko huu wa tahadhari ni wanachama wote wa TANESCO SACCOS, ambao wamefika umri wa miaka 18 na hawajavuka umri wa miaka 65

4.ELIMU NA MAFUNZO KWA WANACHAMA
Chama kinatambua umuhimu wa elimu. Chama kila mwaka huandaa bajeti na ratiba ya kutoa elimu kwa wanchama wake wote nchi nzima juu ya masuala mbalimbali yenye kuboresha ustawi wa wanachama, sehemu ya elimu na mafunzo hayo ni pamoja na ; Elimu ya ujasiriamali, Ushirika, Uwekezaji n.k

MATARAJIO YA BAADAE
1.Kufungua wigo wa uanachama kwa kufungua fungamanisho (common bond) kwa kuruhusu makundi mbalimbali kuendelea/ kujiunga na chama. Makundi hayo ni pamoja na Wastaafu kuendelea kuwa wanachama, kuruhusu wafanyakazi wa kampuni ya umeme na makampuni mengine yatakayoomba na kuidhinishwa na Bodi kuwa wanachama, kuruhusu wafanyakazi wa muda (temporary employees), mme/mke wa mwanachama kuwa wanachama.

2.UWEKEZAJI
Kuongeza mapato kipitia uwekezaji katika kiwanja cha kibaha, kuanza utekelezaji katika kiwanja cha kibaha, kuanza utekelezaji wa biashara ya ujenzi
(a)Kuunda kampuni ya uwekezaji ya chama
(b)Kuuza hisa kwa ajili ya ujenzi

3. KUANZISHA BIDHAA NA HUDUMA MBALI MBALI
Chama katika mikakati ya kujiimarisha kaimapato na kimtaji kinatarajia kuanzisha huduma na bidhaa mbali mbali zenye lengo la utoaji huduma wa sasa na kuwapa wigo mpana wa huduma wanachama wenye mahitaji tofauti, huduma hizo ni pamoja na ;
(a)Kuanzishwa kwa akaunti ya Amana (mwanachama ataweza kuweka  na kutoa fedha wakati wowote)
(b)Kutoa mkopo kwa viwango na masharti tofauti kupitia mishahara ya wanachama
(c)Kufungua akaunti za wanachama kwa ajli ya kupitishia mikopo na mishahara yao

 Makala hii imeandaliwa kwa hisani ya WABUNIFUMEDIA
Mwandishi wa makala hii ni Yusuph Mwamba +25557636650
Kwa mawasiliano zaidi kujua kiundani Tanesco saccos ungana nasi kupitia;
Millenium Business Park,
S.L.P 9024 Dar es salaam,
Simu:+255,222450472,
Nukushi:+25522245042,
Barua pepe:info:saccos@tanesco.co.tz.
Tovuti:www.tanescosaccos.or.tz

JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.wabunifumedia.blogspot.com ku-install App ya wabunifumedia,  bila ya kuingia websiteTweet@wabunifumediaonline, youtube@wabunifumediaonline TV, Fb@wabunifumediaonline, insta@wabunifumediaonline



Post a Comment

Theme images by Maliketh. Powered by Blogger.