Na Mwandishi wetu
Serikali imewatoa hofu
watumishi wote wa Kampuni Hodhi ya Rasilimali za Reli (RAHCO), na Shirika la
Reli Tanzania (TRL), kwa kuwahakikishia
kuwa ajira zao hazitaathirika kwa kuwa sheria mpya ya Reli ya Mwaka 2017 imeweka
utaratibu maalum kwa watumishi hao kuhamia kwenye taasisi mpya ya Kampuni ya
Reli Tanzania (TRC).
Katibu Mkuu wa Wizara
ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Sekta ya Uchukuzi, Dkt. Leonard Chamuriho amesema
hayo katika mahojiano maalum mjini Dodoma na kusisitiza taratibu zote za
kiutumishi zitafuatwa kwa watumishi watakoendelea na kazi kwenye kampuni mpya.
"Sheria mpya ya reli
mwaka 2017 imezigatia maslahi ya watumishi kwa kuweka mazingira mazuri kwa
wafanyakzi wa RAHCO na TRL hivyo
atakaetaka kuendelea kutumikia umma katika shirika hili jipya ataendelea na
kazi na atakaetaka kucha kazi basi taratibu za kiutumishi zitafuatwa kwa mujibu
wa taratibu na Kanuni" amesema Dkt. Chamuriho.
Dkt. Chamuriho amesema
kuwa lengo la kuunganisha taasisi hizo ni kuongeza ufanisi wa shirika hasa
kwenye usaifirishaji wa mizigo na kuondoa tofauti zilizokuepo kati ya RAHCO na
TRL ambazo zimekuepo kwa muda mrefu kwenye usimamizi na uendeshaji wa shirika
hilo.
Kwa upande wa Reli ya
Kisasa (SGR) Dkt. Chamuriho amesema kuanzishwa kwa sheria mpya kutaongeza
ufanisi wa utekelezaji wa mradi huo kwa awamu ya kwanza ambayo inahusisha awamu
tano ambapo awamu ya kwanza itajengwa kuanzia Dar es Salaam- Morogoro, Awamu ya
pili Morogoro-Makutupora, awamu ya tatu Makutupora-Tabora, awamu ya nne
Tabora-Isaka na awamu ya tano Isaka-Mwanza.
Aidha ameongeza kuwa
baada ya awamu hizo kukamilika Serikali itaanza awamu ya pili itakayohusisha
sehemu za Tabora-Kigoma, Mpanda-Kaliua na Ruvu-Tanga-Moshi-Arusha.
Kupitishwa kwa Sheria
ya Reli ya mwaka 2017 na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kunaifuta
sheria ya Reli No. 4 ya mwaka 2002 na sheria hii itaanza kutumika baada ya Rais
wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania kuisaini.
JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.wabunifumedia.blogspot.com ku-install App ya wabunifumedia, bila ya kuingia websiteTweet@wabunifumediaonline, youtube@wabunifumediaonline TV, Fb@wabunifumediaonline, insta@wabunifumediaonlin
Post a Comment