Samahani lakini kwa picha hii Habari na Zephania Kapaya |
Baadhi ya wanafunzi hao wanatumia
mtandao wa ‘University Tanzania Jokes’, ‘Jicho la Mvulana Liko Fasta
Kuliko Google’, ‘Benki ya Utamu Tanzania’ na nyingine katika kufanikisha
biashara hiyo ya ngono.
PENGINE haya tunaweza kuyaweka kwenye kundi la madhara yatokanayo na utandawazi. Mitandao ya kijamii ipo inayowasaidia wanafunzi katika masomo yao na kazi, lakini wengine wanatumia mitandao hiyo visivyo.
PENGINE haya tunaweza kuyaweka kwenye kundi la madhara yatokanayo na utandawazi. Mitandao ya kijamii ipo inayowasaidia wanafunzi katika masomo yao na kazi, lakini wengine wanatumia mitandao hiyo visivyo.
Uchunguzi wa Mwananchi umebaini kuwa
matumizi mabaya ya teknolojia hasa mitandao ya kijamii yamechochea
ongezeko la uhalifu, ubakaji, matumizi ya dawa za kulevya na zaidi
biashara ya ukahaba vyuoni.
Mitandao ya ‘Facebook’, ‘Twitter’,
‘BBM’, ‘Instagram’ inafahamika kwa namna inavyoweza kuwaunganisha watu
kutokana na urahisi wake katika kuitumia.
Mwananchi limebaini kuwa katika mitandao hiyo makundi mbalimbali yameanzishwa yakiwa na malengo tofauti.
Baadhi wameanzisha makundi kwa lengo la
kujenga mitandao ya kibishara, kidini, michezo, burudani, vichekesho na
mengine ambayo mara nyingi huwa wazi na yeyote anaweza kujiunga na kuona
kinachoendelea ndani.
Mbali na hayo ndani ya mtandao wa
‘Facebook na ‘BBM’ yapo makundi yanayoendesha biashara ya ukahaba,
yakiwahusisha wanafunzi wa vyuo vikuu mbalimbali nchini.
Uchunguzi umebaini kuwa wanafunzi hao
wanaofanya biashara ya ukahaba kwa kutumia mitandao wameweka picha na
namba kwa ajili ya mawasiliano kwa mteja atakayekubaliana na bei
waliyoweka.
Baadhi ya wanafunzi hao wanatumia
mtandao wa ‘University Tanzania Jokes’, ‘Jicho la Mvulana Liko Fasta
Kuliko Google’, ‘Benki ya Utamu Tanzania’ na nyingine katika kufanikisha
biashara hiyo ya ngono.
Ukiingia katika mitandao ya Facebook,
Twitter, BBM, Instagram, utabaini kuwapo kwa makundi yaliyoundwa
kutengeneza mitandao ya ngono, ambayo huweka pia namba za simu za
wahusika, zikiambatana na picha, ambao ikiwa utaangalia picha na
kuvutiwa, unaweza ukapiga simu husika kuzungumza naye kwa kufanya
mapatano kabla ya kukubaliana.
Uchunguzi wa Mwananchi Jumapili umebaini kuwa mwanamume anaweza kumpata msichana kutoka chuo kikuu chochote nchini anayefanya biashara ya ukahaba kupitia mitandao hiyo.
Baadhi ya vyuo wanavyotoka wasichana wanaofanya biashara hiyo na kujitangaza kwenye mitandao ni pamoja na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine (SAUT), Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) na Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM).
JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.wabunifumedia.blogspot.com ku-install App ya wabunifumedia, bila ya kuingia website
Tweet@wabunifumediaonline, youtube@wabunifumediaonline TV, Fb@wabunifumediaonline, insta@wabunifumediaonline .
Post a Comment