Na Zephania Kapaya.
Tumeshuudia wachezaji wengi sana wakishindwa kuendelea na mpira sababu tu ya majeraha ya mara kwa mara na wengine wakishindwa kuendana na kasi ya mpira kwa sababu ya umri kuwatupa mkono, tumeshuudia wachezaji wengi sana lakini kwa hawa ndio kwanza kunakucha.
Kwenye mpira wa miguu, mchezaji akishafikisha miaka 30 huonekana mzee
na hata kama akisajiliwa thamani yake kipesa huwa sio kubwa kama vijana
wa miaka 22-28. Wachezaji wengi wakifikisha zaidi ya miaka 30 huonekana
mizigo uwanjani na mara nyingi viwango vyao huporomoka na hili
linadhihirika kila kukicha. Kwa baadhi ya wachezaji imekuwa tofauti
kwani umri wao ni zaidi ya miaka 31 lakini viwango vyao bado
vinahitajika kwenye timu na mashabiki wao.
Kutokana na hili, leo tuwatazame baadhi ya wachezaji ambao kiumri
wanaonekana wazee ila kiuhalisia uwanjani wanaonekna bado vijana wadogo
na ushahidi wa hili ulionekana msimu uliopita katika vilabu vyao.
Frank Ribéry ni winga wa Bayern Munich ambaye
anaweza kunyumbulika upande wa kushoto au hata kulia kama kuna pengo.
Ribery amehudumu Bayern kwa takribani miaka 10 tangu alipotoka Marseille
mwaka 2007. Miaka 34 aliyonayo hivi sasa haitofautiani na winga wa
miaka 23 anayecheza ‘Top flight league’. Msimu uliopita Frank aliisaidia
Bayern kufika nusu fainali huku penati aliyokosa Vidal akiisababisha
yeye. Ribery ni mfaransa ambaye amejijengea heshima Ujerumani.
Uwezo wake mkubwa umemfanya kuaminiwa na Ancelot japokuwa majeraha
yamekuwa yakimuandama. Kiungo huyu mshambuliaji mwenye imani ya kiislamu
amekuwa na misimu mizuri tangu ajiunge Bayern na ukweli ni kwamba
namuona akizeeka na utamu wake uwanjani.
Arjen Robben ni mholanzi ambaye anajuta kuzaliwa
kipindi ambacho dunia ina winga hatari kama Cristiano Ronaldo. Mchezaji
huyu mwenye sura ya kizee ni ‘shida’ pindi anapokuwa na mpira. Robben
anaweza kukugeuza anavyotaka, anakukimbiza vile anavyojiskia. Kwa sasa
ana miaka 33, wachezaji alioanza nao karia wengi wamepotea ila yeye bado
hajulikani ni lini ataanza kuanzia benchi. Chelsea ilimuuza kwenda
Madrid ila ujio wa CR7 ulimfanya aende Bayern ambapo amechukua mataji
yote.
Msimu uliomalizika alicheza michezo 37 na kufunga magoli 16 akiwa na
klabu yake na kumfanya kuwa wa pili baada ya Lewandosk. Magoli 43
aliyoyafunga Roberto Lewandosk msimu uliomalizika yametokana na usumbufu
wa winga huyu ambaye amechukua vikombe vyote isipokuwa World Cup.
Andres Iniesta ni kiungo mchezeshaji wa FC
Barcelona. Wakati mwingine unapata kigugumizi kusema eti Messi na CR7
ndio wachezaji bora wa Dunia tangu 2008 hadi sasa. Iniesta anastahili
kuitwa fundi wa mpira japokuwa hadi sasa ana miaka takriban 33. Msimu
uliomalizika aliisaidia Barca japokuwa Barca walishindwa kujisaidia
wenyewe. Amejaaliwa nidhamu na kipaji cha hali juu hasa katika kupiga
pasi. Messi anafurahia uwepo wa Iniesta na huenda anatamani Iniesta
azidi kuwa kama sasa.
Msimu uliomalizika Iniesta alicheza michezo 37, japokuwa umri
umekwenda uwezo wake ulikwa ni kama wa kiungo ‘mbichi’ wa miaka 20.
Naweza kusema kwa kujiamini kuwa huyu jamaa huenda akastaafu na utamu
wake kama ‘Pacha’ wake Xavi Hernandez ambaye Lamasia inam-msi hadi sasa.
Cristiano Ronaldo ni moja kati ya wachezaji bora
kabisa kuwahi kutokea katika zama hizi. Nikisema CR7 analijua goli
kuliko mchezaji yoyote sizani kama nitakuwa nakosea japo nakuruhusu
unikosoe. Katika michezo 265 aliyoichezea Madrid, CR7 amefunga magoli
285. Kwa sasa anaelekea mwaka wa 33 ila akiwa kwenye kumi na nane za
wapinzani, CR7 amekuwa ‘Clinical finisher’ mzuri na hili lilidhihirika
kwenye ligi ya mabingwa Ulaya msimu uliopita kutokana na ‘hat-trick’
alizopiga.
Msimu uliomalizika CR7 alicheza mechi 46 na kufunga magoli 42 huku
akiisaidia Madrid kushinda taji la 12 la UEFA na ubingwa wa La liga pia.
Ronaldo hawezi kupiga tena mikasi au kukimbia kwa kasi ila hajazeeka
kwenye ufungaji. CR7 naweza kusema anazeeka na utamu wake wa ufungaji.
Dani Alves ni beki wa kulia aliyezaliwa nchini
Brazil miaka 34 iliyopita. Kwa sasa amesajiliwa na matajiri wa PSG
akitokea Juventus kama mchezaji huru. Barca hadi kesho itawachukua muda
mrefu kumpata beki wa kulia mwenye sifa kama za Alves. Uwezo wake wa
kupanda na kushuka hautofautiani na Marcelo anayecheza kushoto pale
Madrid. Baada ya kuondoka Barca, Juventus walifurahia huduma yake licha
ya umri wake kuwa mkubwa. Dani Alves haendani kabisa na umri wake.
Msimu uliomalizika Alves aliichezea Juventus michezo 33 na kufunga
magoli 6. Man City wamejaribu mara kadhaa kumsajili ila PSG waliwazidi
kete. Alves anazeeka na ufundi wake kwani kasi yake haitofautiani na ile
ya 2010.
latan Ibrahmovich ni Mshambuliaji hatari ambaye
amekamilika. Zlatan kacheza katika vilabu vikubwa barani Ulaya kwa
kiwango cha juu. Msimu uliopita Kadabra aliwabeba Mashetani wekundu na
lau kama majeraha yasingemuandama huenda angefunga zaidi ya magoli
aliyokuwa nayo. Japokuwa Man United wamemuacha kwenye usajili ila
kilichosababisha ni majeraha na sio kiwango. Miaka aliyonayo
Mshambuliaji huyu haiendani na kiwango chake kabisa.
Post a Comment