Halloween party ideas 2015
Image

Na Yusuph Mwamba

KADRI siku zinavyo dhidi kwenda  kila kukicha kumekuwa kukigubikwa na wimbi kubwa la wataalamu wa waganga wa Jadi na Tiba asilia lakini miongoni mwa wataalamu hao wengi wao wamekuwa matapeli na kukosa sifa za kuwa tabibu hii yote ni kutokana na kutozingatia mfumo mzuri uliopangwa na  Serikali katika kusajili Kliniki na vituo vyao vya kazi pamojaa na tiba wanazozitoa.
Dawa asili hazina uhusiano wowote na masuala ya tiba yanayoshughulikiwa na waganga wa  kienyeji wanaotumia mazingaombwe, ushirikina, mizimu, mashetani na mambo kama hayo.



Tunaposema tiba asilia tunamaanisha dawa zinazotokana na majani, magome ya miti, mizizi, matunda kwa ajii ya kunywa, kupaka kichwani na hata kunusa.


Tiba hii ya kutumia dawa za asilia ilikuwepo kabla ya ujio wa wakoloni. Wakoloni walipoingia hapa nchini walileta dawa za vidonge, vimiminika huku vikiambatana na matuminzi ya sindano.

Ujio huu wa dawa zakigeni kuingia nchini kwa tiba kwa wagonjwa mbalimbali, umeibuka mtindo hivi sasa wa kudharau na kutupa tiba asilia. Pia ulaji wa vyakula asili umepunguana sehemu nyingine umeachwa kabisa.

Mawazo finyu tuliyopata ni kwamba tiba asilia ni mbaya jambo hili limefanya tujenge dhima ya kutothamini kilicho chetu kwa kuthamini kila kinachotoka nje.

Ikumbukwe wataalamu wa Mrekani, China, DPRC, India, waliwahi kufanya utafiti wa kisayansi na waligundua uwezekano wa kupata aina mbalimbali za madini, virutubisho, vitamini na lishe na kwa watoto wachanga, wazee na wagonjwa kwa kutumia mimea asilia.

Imebainika kuwa maradhi kama kisukari, vidonda vya tumbo, maradhi ya kinywa, fidhi, ngozi na pia meno huweza kutibiwa kwa kutumia vidonge na vimiminika vitokanavyo na mimea asilia.

Lengo na utafiti huu ni kuachana na tiba ya kigeni na kuachana na mtindo uliozoeleka wa kuchomwa sindano na kutumia vidonge vyenye kemikali ambazo husababisha maradhi na kuathiri mwili kwa ujumla.

Dkt Maximilian, ambaye ni mkurugenzi wa Baraza la Waganga na  Tiba asilia Tanzania (BAWATA) Manispaa ya Kinondoni na Mmiliki wa kituo cha Tiba asilia cha IFAKARA HERBALIST CLINIC kilichopo  eneo la Sinza Tandale Sokoni mkabala na kanisa la Romani Katoriki, kwa sasa anajihusisha na kutibu wagnjwa kwa kutumia madawa asilia pasipo kutumia aina yoyote yenye mchanganyiko wa kemikali huku akidai kuwa kitendo cha kuchanganya kemikali kwenye dawa asili ni kutoa uasilia  wa dawa.

Tabibu Lyana, alifafanua  zaidi na kuelezea kwanini wataalamu wengi  dawa zao zimekosa ubora huku akisema kuwa wengi wao hawajui jinsi ya kuzitunza dawa pamoja na matengenezo ya dawa hizo za asili.

Kwa mujibu wa Dkt: Maximilian Lyana,  dawa zinatakiwa kukaushwa kwa wastani wa jua la kawaida na kivuli cha kawaida hii ikiwa ina maanisha kuzuia kupoteza uasii wa dawa lakini kama dawa itaanikwa kwenye kiasi kikubwa cha jua pasipo na maangalizi bora ya kutengeneza dawa hizo  basi ni dhahiri kwamba  dawa hizo zitapoteza uasilia wake.

Katika kukausha dawa wengi wao haswa wale wanaojua mazingatio ya utengenezaji wa dawa hizo, kama watakausha katika jua kali basi sharti lazima dawa zifunikwe na kitambaa cheusi ambacho kazi kubwa itakuwa inaakisi jua na kupelekea mionzi ya jua kupenya kwa kiasi kidogo katika dawa.


Baadhi ya tiba na  dawa anazotoa Dkt Maximilian Lyana ambazo zinapatikana Ifakara Herbalist Clinic ni pamoja na Dawa ya vidonda vya tumbo, mlesha dawa ya kupooza kwa mwili, dawa ya fangasi ya ngozi, NF3 -dawa ya uvimbe wa uzazi, mlomo -dawa ya kutibu miguu kuwaka moto, MR- dawa ya Malaria, mitundo- dawa ya kusafisha kibofu cha mkojo, fimbo -dawa ya nguvu za kiume, kikoza -dawa ya pumu, M4- dawa ya kinga ya mwili, mfyasa dawa ya kusafisha mfuko wa uzazi, pamoja na  kalimatika dawa ya kupandikiza uzazi.




JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.wabunifumedia.blogspot.com ku-install App ya wabunifumedia,  bila ya kuingia websiteTweet@wabunifumediaonline, youtube@wabunifumediaonline TV, Fb@wabunifumediaonline, insta@wabunifumediaonline








Post a Comment

Theme images by Maliketh. Powered by Blogger.