CHAMA cha siasa hapa Nchini Tanzania, ACT Wazalendo, kimewataka Watanzania kuacha porojo za kisiasa na chuki binafsi zilizokuwa na chembe chembe za uchochezi na kupelekea mvurugano wa amani na badala yake wajikite zaidi kushirikiana na Serikali ya awamu ya Tano katika kufanikisha maendeleoa na kukuza uchumi wa Taifa.
Akizungumza na waandishi wa habari jana Jijini Dar es salaaam,Kiongozi mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe, wakati akitoa tamko la kamati kuu ya chama hicho baada ya kufanyika kikao chake chakawaida jana.Kushoto ni kaimu katibu mkuu wa chama hicho Juma Sanani na kulia ni Makamu Mwenyekiti Tanzania Bara, Shabani Mambo.


Zito amesema kuwa katika kipindi cha miaka 10-15 iliyopita, nchi yetu imejenga uchumi ambao umekuwa ukikua kwa kiwango cha asilimia 6-7 kwa mwaka katika kipindi chote hiki. Ukuaji huu wa uchumi ulitokana na juhudi za nchi katika kuvutia wawekezaji na kuchochea shughuli za uzalishaji mali kwa wananchi wenye kipato cha chini.
"Kamati kuu yetu imeshtushwa na hali ya kuanza kudorora kwa shughuli za uchumi katika kipindi cha miezi kumi ya utawala wa awamu ya tano" amesema Kabwe
Licha ya kutoa tamko hilo, Kabwe, ametoa wito kwa viongozi pamoja na wananchi wasijenge imani potofu ya kusaidiwa pasipo na kuonesha jitihada huku akiwataka washirikiane na Serikali katika kujenga misingi imara ya kufanya kazi na kukuza uchumi wa Nchi yetu.
JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.wabunifumedia.blogspot.com ku-install App ya wabunifumedia, bila ya kuingia websiteTweet@wabunifumediaonline, youtube@wabunifumediaonline TV, Fb@wabunifumediaonline, insta@wabunifumediaonline
Post a Comment