LEO ni siku muhimu kwa Taifa na kwa wale wanafunzi wote wanaohitimu elimu ya shule ya msingi (PSLE) darasa la saba wakiwa katika hatua ya kwanza ya kuanza safari ya kuelekea hatua ya pili ya elimu ya sekondari kwa kufamya mitihani ya Taifa.
Baraza la Taifa la Mitihani (NECTA) limesema watahiniwa 775,729 wakiwamo wasichana 414,227 na wavulana 361,502, wanatarajiwa kufanya mitihani ya taifa ya kuhitimu darasa la saba leo katika shule 16,096 za Tanzania bara.
Akizungumza na waandishi wa habari, katibu Mtendaji wa NECTA, Dkt Charles Msonde, amesema kuwa mitihani hiyo inafanyika kwa siku mbili (leo na kesho) na itahusisha masomo matano ya Kiswahili, Hisabati, Sayansi, Kingereza na Maarifa ya jamii.
Aidha, Dk. Msonde amesema kuwa watahiniwa wote watakaofanya mitihani leowatapewa upendeleo kwa kuongezewa dakika 20 katika kila saa moja kwa somo la Hisabati na dakika 10 kwa masomo mengine.
Pia. Dkt Charles Msonde. ametoa wito kwa wanafunzi, walimu na wasimamizi wote kila mmoja kwa nafasi yake kuzingatia taratibu za kufanya mitihani na kusisitiza kuwa hatua kali zitachukuliwa dhidi ya watakaokiuka taratibu hizo.
"Maandalizi yote ya mitihani hiyo yamekamilika ikiwa ni pamoja na kusambaza karatasi za mitihani, fomu maalumu za OMR za kujibia mitihani na nyaraka zote muhimu zinazohusu mtihani huo,” amesema Dk. Msonde.
Dkt Msonde, alienda mbali zaidi na kusema kuwa watahiniwa 748,514 watafanya mitihani kwa Kiswahili na wengine 27,215 watafanya mitihani yao kwa Kiingereza, lugha ambazo wamekuwa wakizitumia siku zote kujifunzia.
JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.wabunifumedia.blogspot.com ku-install App ya wabunifumedia, bila ya kuingia websiteTweet@wabunifumediaonline, youtube@wabunifumediaonline TV, Fb@wabunifumediaonline, insta@wabunifumediaonline
Post a Comment