Halloween party ideas 2015
Image

 Na Yusuph Mwamba

KUTOKANA na Ongezeko la magonjwa mbali mbali na magonjwa sugu yanayo tukabili kila kukicha pamoja na  gharama za  matibabu kupanda, na idadi ndogo ya madaktari hapa  Nchini ni baadhi ya sababu zinazochangia kwa kiasi kikubwa wagonjwa wengi kukimbilia kwa waganga wa tiba za jadi ili kupata matibabu.Licha ya wagonjwa wengi kwenda katika kliniki za waganga hao kwa kificho.

MWAKA WA MATUMAINI NA

IFAKARA HERBOR CLINIIC DK. MAXIMILIAN YEAR OF HOP

Ukiwauliza wagonjwa wengi kwa nini wawanajificha wanapokwenda katika kliniki za waganga wa tiba za jadi kupata matibabu, utaambiwa ni kwa sababu wengi wanahusisha uganga na imani za kishirikina au uchawi. 




Lakini ukipata nafasi ya kuzungumza na walio bahatika kufika na kupata matibabu katika kliniki hizo, wanakiri tiba za waganga wa jadi ni bora na pengine kuliko hata zinazopatikana katika hospitali za madaktari wa kisayansi. 
Baadhi ya dawa zinazopatikana Ifakara Herbor Clinic








 Tanzania ni moja kati ya nchi 46 wanachama wa Chama cha Tiba Asilia Afrika Mashariki, kwahiyo kutokana na mpango huo kuna haja ya kuhakikisha kuwa wanaunda umoja wa dhati katika kufanikisha juhudi zao za kuwasaidia na kutoa huduma kwa wagonjwa wenye magonjwa sugu na kupelekea pato la Taifa husika.






 Mwanzoni mwa miaka ya 80 wakati Rais wa Kwanza wa Tanzania, Julius Nyerere akizindua utafiti wa dawa asilia, aina ya dawa zilizokuwa zikitumika kwa tiba zilikuwa 108, lakini hivi sasa zimeongezeka maradufu hadi kufikia zaidi ya dawa elifu kumi.

Baadhi ya dawa zinazopatikana kwa Dkt Maximilian 

Hapa tuna kwenda moja kwa moja kumwangalia Dkt wa Tiba asilia, Dkt Maximilian William Lyana, wengi wao hupenda kumuita Dkt Willy , kutoka mkoani Morogoro lakini kwa sasa amehamisha makazi yake hapa Jijini Dar es salaam, kwa ajili ya kutoa huduma zake za asili kwa wale wenye magonjwa, sugu.


Dkt Maxlyana, ni Mtaalamu wa Tiba asilia wa kurithi kutoka kwa ukoo wake huku Baba yake mzee Lyana ,pamoja na babu na bibi yake wote kwa ujumla walishafanya kazi ya utabibu wa asilia.

Kutokana na kurithi huko, Dkt Max, alifanikiwa kuanza kazi akiwa na umri w miaka 14 lakini ndani ya miaka hiyo yapo yliyomfanya aingie katika kazi hiyo , kwa sasa amefikisha umri wa miaka 30 katika kazi hiyo ya kutoa huduma ya Tiba asilia kwa wagonjwa.

Tabibu Lyana, ni mtaalamu wa maswala ya Tiba asilia na alishawahi kuwa Dkt wa Hospitali ya kisayansi lakini kutokana na ujuzi wake na kuwa na fursa aliona ni vema kujikita zaidi katika maswala ya Tiba asilia huku akiamini ndio njia sahihi ya kuwasaidia wagonjwa kutokana na miti shamba licha ya kuwepo kwa changamoto nyingi katika tasnia hii.

Tabibu Lyana, akizungumzia juu ya utofauti kati ya wataalamu walio katika tasnia hiyo ya Tiba asilia, amesema kuwa baadhi ya wataalamu hao wengi wao wamekuwa hawatendei haki dawa hizo na badala yake wamekuwa wakigeuza dawa asilia kwa kuchanganya na kemikali huku akidai kwamba huo si utabibu bali wanatoka katika njia ya ualisia na kufanya baadhi ya dawa hizo kuto kufanya kazi na kukosa ubora wake.

Dkt Lyana, alienda mbali zaidi na kuelezea utofauti uliopo na kusema kuwa kwa sasa licha ya baadhi ya tuhuma nyingi wanazozipata lakinii amefunguka na kuelezea makundi mawili ambayo yanajihusisha na taaluma hiyo ya Tiba asilia, kundi la kwanza ni Waganga wa kurithi na Waganga wa kupeana kiurafiki na kuwashutumu wanaopeana ndio wanao haribu soko la matabibu asilia na kufanya wengi wao kutokuwa na imani nao.

Miongoni mwa Nchi ambazo Dkt Lyana, alipata kuzunguka katika kufanya kazi zake za kitabibu ni Nchi ya Msumbiji, Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo (DRC),a  Kenya pamoja na Uganda huko alikwenda kwa ajili ya mialiko.

Dkt Lyana, hakusita kuzungumzia matatizo ya uzazi yanayo wakumba  wanawake na kupelekea mwanamke kutokupata mimba, katika matatizo hayo Dkt Lyana, ameyataja kwa njia ya kiasili na kuzungumzia kwa njia ya kiswahili ili kujaribu kutoa elimu ambayo itawasaidia wagonjwa hawa kujinasua na tatizo la uzazi.

Ndatila, Neno hili ni neno la kiasili ambalo limejaribiwa kufafanuliwa kwa lugha ya kiswahili fasaha ikimaanisha kuwa ni swala la kufunga kwa uzazi/ kutokupatwa kwa  siku zake huku likisindikizwa na maumivu makali chini ya kitovu.

Ngeketa, Neno hili ni neno la kiasili ambalo limejaribiwa kufafanuliwa kwa lugha ya kiswahili fasaha likimaanisha kuwa ni swala la kupatwa maumivu chini ya tumbo na  kutokuona siku zake katika hali yake ya kawaida swala hili likimtokea mwanamke basi hilo litakuwa ni tatizo litakalo mpelekea kutokupata mimba.

Liholera, Neno hili ni neno la kiasili ambalo limejaribiwa kufafanuliwa kwa lugha ya kiswahili fasaha likimaanisha kutokwa kwa damu mfululizo kwa wingi na kutokwa na madonge meusi pamoja na kutokwa kwa harufu mbaya  na kwali katika sehemu za siri.

Kisheria, mwanamke haruhusiwi kuona siku zake tangu pale alipopata mimba lakini kama itatokea akaona siku zake basi atakuwa na tatizo na kupelekea kutokupata mimba hii inachangiwa na mfuko wa uzazi kuwa na nafasi ya kupenyeza damu.

Baada ya kujifungua, kisheria mwanamke anatakiwa kuona siku yake baada ya miezi sita lakini hili linatokana na mfumo wa homoni alionao.

Kuhusu changamoto, Dkt Lyana, amesema kuwa changamoto kubwa zaidi zinasababishwa na waganga wenyewe kutokuwa waaminifu na kazi hii huku waakiwapelekea wengi wao kutoa pesa bila mafanikio, kuharibu mfumo wo wa kimaisha pamoja, vifo pamoja na kuwatelekeza wagonjwa wakiwaacha na majeraha ya kudumu.

Viongozi wa dini, Dkt Lyana,  amesema kuwa  baadhi ya viongozi wa dini nao wamekuwa kikwazo kwa kuwaponda wawapo katika nyumba za ibada badala yake kuwahamasisha waumini wao na kuwapiga vita kali waganga na kutoa utofauti kati ya waganga wa jadi na wachawi.

Wito kwa Serikali, Dkt Lyana, amewasihi Viongozi wa Serikali pamoja na wadau mbali mbali wenye mapenzi mema na Nchi yetu kutowadharau na  kutambua umuhimu wa waganga wa jadi katika  kuwapa kipaumbele katika kujenga uhusiano mzuri wa kuchangia pato la Taifa na kuboresha miundo mbinu katika sekta ya afya.


Dkt Lyana, ameeleza mipango yake ya baadae  huku akitaka kusambaza huduma hiyo katika mikoa mbalimbali licha ya kuwa na ktuo Mkoa wa Morogoro, Wilaya Kilombero kata ya Lipungalala Tarafa ya Ifakara , huku akitaka kupiga hatua zaidi kuvuka nje ya mipaka ya Tanzania na kulifanya soko hilo kuenea katika ukanda wa Afika mashariki na kati.


 JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.wabunifumedia.blogspot.com ku-install App ya wabunifumedia,  bila ya kuingia websiteTweet@wabunifumediaonline, youtube@wabunifumediaonline TV, Fb@wabunifumediaonline, insta@wabunifumediaonline








Post a Comment

Theme images by Maliketh. Powered by Blogger.