KAMPUNI ya simu ya Tigo, leo imetoa masaada wa Madawati 135 mkoa wa Geita , yenye thamani ya shilingi Milioni 35 kama moja ya mchango wao kwa ajili ya kusaidia Serikali katika mpango wake wa Elimu bure Nchini Tanzania.
Baadhi ya Madawati yalitolewa na kampuni ya Tigo katika kusaidia mpango wa Elimu bure mkoani Geita |
Mkuu wa mkoa wa Geita, Mh: Meja Jenerali (MST) Ezekiel Ekyunga, naye kwa upande wake hakusita kuzungumzia mchango huo na kuwata wale wote wenye moyo wa kuchangia Elimu ya Tanzania wajitokeze kwa wingi katika kufanikisha mpango wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli.
Mkuu wa mkoa wa Geita, Mh: Meja Jenerali Ezekiel Ekyunga |
Aidha, kabla ya ujio wa mchango huo kutoka kampuni ya Tigo, Wananchi wa mkoa wa Geita, walifanya harambee ya kuchangishana na kufikisha kiasi cha fedha chenye thamani ya Bilioni 1.7 kwa ajili ya utengenezaji wa Madawati.
Tigo kwa sasa ndio waandalizi wa Tamasha la Fiesta 2016, linaloshrikisha baadhi ya wasanii katika makundi tofauti tofauti katika tasnia ya Muziki hapa Nchini kwa kushirikiana na Prime time Promotion chini ya Clouds Media Group.
JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.wabunifumedia.blogspot.com ku-install App ya wabunifumedia, bila ya kuingia websiteTweet@wabunifumediaonline, youtube@wabunifumediaonline TV, Fb@wabunifumediaonline, insta@wabunifumediaonline
Post a Comment