KIKOSI cha Timu ya Taifa , Taifa Stars kinatarajiwa kupaa usiku wa leo kuelekea Nchini Nigeria kwa ajili ya pambano la kuwania kuchezo fainali za kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON2017) huko Nchini Gaboni.
Katika mchezo huo unaotarajiwa kupigwa Septemba 3, 2016 siku ya Jumamosi, mchezo huo utakuwa ni mchezo wa mwisho wa kukamilisha ratiba kwa timu yetu ya Taifa Stars .ambapo kwa mujibu wa kundi letu mpaka sasa Timu ya Taifa ya Misri imeshafuzu katika kundi G baada ya kufuatia kujitoa kwa timu ya Taifa ya Chadi
Akizungumza na chombo kimoja cha Habari cha E-FM, leo asubuhi katika kipindi cha Sports Head Quater, mkuu wa msafara huo, Mussa Kisoki, amesema kuwa kikosi kitaondoka leo usiku na kufika Nchini Nigeria mchana wa kesho huku mwanandinga wa Kimataifa wa Tanzania anayecheza Soko la kulipwa Ubelgij, Mbwana Samatta naye atawasili kesho huko Nigeria kwa ajili ya kujiunga na Timu ya Taifa.
"Kikosi kitaondoka leo usiku na kitawasili kesho mchana, ila kwa mujibu wa ratiba tuliyopewa ni kwamba mchezo huo utachezwa nje kidogo ya Lagos katika Jimbo la Oyo yapata kilomita 350, na juu ya muda wa mchezo utachezwa muda gani sijapewa ratiba ila jioni nitakuwa na Press na shirikisho lao na kuwahabarisha Watanzania lakini kwa sheria za mpira wa miguu timu ikicheza umbali wa kilomita 200 ,timu husika itakuwa na jukumu la kuisafirisha timu ngeni kwa hiyo tutaondoka tena hapa kwa ndege mpaka Jimbo la Oyo". Alisema Kisoki
Kikosi kinachounda Timu ya Taifa Stars kinaongozwa na Golikipa, Aisha Manula
Walinzi, Kelvin Yondani, Vicent Andrew, Mwinyi Haji (Yanga), Mohamed Hussein (Simba), Shomari Kapombe, David Mwantika wote kutoka Azam FC.
Viungo, Hamid Mao (Azam FC), Shiza Kichuya (Simba SC), Ibrahim Jeba (Mtibwa Sugar), Jonas Mkude, Muzamiri Yassin (Simba), Juma Mahadhi (Yanga SC) na Farid Mussa kutoka Tenerif ya Hispainia.
Washambuliaji, Simon Msuva (Yanga SC), Jamali Mnyate, Ibrahim Ajib (Simba SC), John Bocco ( Azam FC) pamoja na Mbwana Samatta kutoka KC Genk ya Ubelgij.
JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.wabunifumedia.blogspot.com ku-install App ya wabunifumedia, bila ya kuingia websiteTweet@wabunifumediaonline, youtube@wabunifumediaonline TV, Fb@wabunifumediaonline, insta@wabunifumediaonline
Post a Comment