WAZIRI mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majariwa Kassim, yupo mbioni kuhamisha makazi yake ya kiofisi rasmi Makao makuu ya Tanzania Dodoma, Septemba mosi ikiwa ni agizo na utekelezaji kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ,Dkt John Pombe Magufuli kutaka Serikali kuhamia Dodoma.
Akizungumza na Waandishi wa Habari kwenye maadhimisho ya Siku ya kumbukumbu ya Mashujaa zilizofanyika kwa mara ya kwanza kwenye uwanja wa Mashujaa, Mjini humo, Majaliwa, amesema kuwa kwa sasa kilichombele yake ni kuhakikisha ifikapo Tarehe 1, Septemba, 2016 anahamia rasmi makazi mapya katika kutekeleza agizo la Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Dkt Magufuli.
"Nataka kuwaambia kwa sasa tupo katika maandalizi ya kuhamia Dodoma, huu ndio mwanzo wa Serikali yote kuhamia huko japo tutahamia kwa mafungu lakini kutokana na Serikali yetu kuonesha nia ya dhati ya kuihamisha Serikali yote naamini tutafanikiwa na kuhamia rasmi Dodoma safari yangu itaanza Tarehe 1 Septemba, 2016".Alisema Majaliwa
Wakati huo Majaliwa akiwa katika maandalizi hayo, Mkuu wa Wilaya ya Dososma Mjini, Christina Mndeme, amewataka Wananchi kujitokeza kwa wingi siku ya hiyo kumpokea Waziri Mkuu.
"Maandalizi yanaendelea vizuri na ninawaomba wakazi wa Dodoma kujitokeza kwa wingi kumpokea Waziri Mkuu kwa sababu hili ni tukio la Kihistoria".Alisema Mndeme
JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.wabunifumedia.blogspot.com ku-install App ya wabunifumedia, bila ya kuingia websiteTweet@wabunifumediaonline, youtube@wabunifumediaonline TV, Fb@wabunifumediaonline, insta@wabunifumediaonline
Post a Comment