Na Mwandishi wetu
CHUO kikuu cha Teofilo Kisanji
kilichopo mjini mbeya kimetoa mashuka themanini(80) katika hospitali teule
(moraviani) Sikonge ikiwa ni kawaida ya chuo hicho kutoa misaada hiyo kila
mwaka kwa watu wenye mahitaji maalumu.
Chuo kikuu cha Teofilo Kisanji |
Akitoa msaada huo profesa wa
chuo hicho ndugu Kasimoto Lubi alisema huwa wanautaratibu wa kutoa misaada
sehemu mbalimbali lakini mwaka huu chuo kimeona kitoe msaada katika hospitali hiyo
kwa ajiri ya wajawazito na watoto.
Aliongeza kuwa mwaka 2009 chuo
kilitoa msaada katika jimbo la kusini rungwe kwa ajiri ya watoto yatima na
wafungwa waliopo mjini mbea .
Akipokea msaada huo mkuu wa wilaya
ya Sikonge Hanifa Selengu alikishukuru
chuo hicho kwa kuwa na moyo wa kujitolea na kuwajali watu wasiojiweza kama
wagonjwa na watoto yatima.
Aliwaasa wakunga na wauguzi wa
hospitali hiyo kuwahudumia akina mama vizuri bila kutumia lugha za kejeli,
matusi na dharau kwani serikali itawachukulia hatuakali.
“Nasisitiza wauguzi kutoa
huduma nzuri kwa wanawake kwa uzito mkubwa bila kuwabeza na kuwatukana matusi
vinginevyo serikali itachukua hatua dhidi yao” Alisema Hanifa.
Post a Comment