Halloween party ideas 2015
Image

Na Yusuph Mwamba

KIKOSI cha timu ya Taifa ya Uingereza kimefanikiwa kujiweka katika mazingira rafiki ya kusonga mbele katika michuano ya fainali ya Eoro 2016 baada ya kufanikiwa kuidhibu timu ya Taifa ya Wales  jumla ya mabao 2-1.

Mchezo huo ambao ulitawaliwa na hisia kubwa za mashabiki,  kwani ulikua na upinzani mkubwa sana kutokana na timu zote kutoka katika falme moja ya Uingereza.

Mwanandinga wa kimataifa na klabu ya soka ya Real Madrid , Gareth Bale alifanikiwa kuwaamsha mashabiki wa Wales baaada ya kufanikiwa kutikisa nyavu  ya Uingereza kunako dakika ya 42 kabla ya kuelekea mapumziko mwa mchezo huo.

Licha ya Wales kutangulia kupata bao, lakini kipindi cha pili timu zote zilionekana kucheza kwa kukamiana , lakini Ungereza walionekana dhahiri kuutawala mchezo huo.

Kipindi cha pili kocha wa Uingereza alifanya baadhi ya mabadiliko alipo watoa nyota Hary Kaene anaye kipiga kunako klabu ya Totenham Spurs na Raheem Sterling anekipiga Manchester City na nafasi zao kuchukuliwa na Wanandinga Daniel Sturrudge anaekipiga klabu ya Liverpool na Jamie Vard kutoka klabu ya Leicer City.

Mabadiliko hayo yalionekana kuzaa matunda kwa upande wa kikosi cha Uingereza, punde ya mchezo mwanandinga Jamie Vard alifanikiwa kuisawazishia kikosi chake baao safi kunako dakika ya 59 ya mchezo, huku Nyota Daniel Sturridge akionekana mwiba kwa Wales baada ya kupigilia msumari wa mwisho na wa ushindi wa kikosi hicho cha Roy Hodgson.

Kwa matokeo hayo, Uingereza inahiji alama moja katika mchezo wao wa jumatatu ili kuweza kujiweka kjatika mazingira mazuri ya kufuzu katika hatua ya 16 bora ya fainali ya michuano ya Euro 2016.






Post a Comment

Theme images by Maliketh. Powered by Blogger.