Halloween party ideas 2015
Image

Na Yusuph Mwamba

NYOTA wa zamani wa kimataifa wa Uingereza na klabu ya Arsena, Alan Smith amemtaka kocha wa timu ya Taifa ya Uingereza Hugdson kukifanyia mabadiliko kikosi chake kwenye mchezo ujao dhidi ya Solvakia kama anahitaji kusonga mbele.

Smith mwenye umri wa miaka 54, aliyewahi kuvitumikia baadhi ya vilabu mbalimbali vya soka ikiwemo timu ya Taifa ya Uingereza amesema kama Hugdson anahitaji timu hiyo isonge mbele katika hatua ya 16 bora basi hana budi kufanya mabadiliko katika kikosi chake.

Miongoni mwa vilabu alivyopata kuvitumikia Smith enzi za ujana wake ni Arsenal FC, ikiwemo mabingwa wapya wa ligi kuu ya Uingereza klabu ya Leicer City. Mwanandinga huyo alizaliwa mwaka 21 November, 1962, Jiji la Hollwood na alifanikiwa kujinga na klabu ya Leicer City 1982 na kuhamia klabu ya Arsenal mnamo mwaka 1987.

Mwanandinga huyo amesema kunahaja ya Uingereza kufanya mabadiliko haswa safu ya ushambuliaji inayoongozwa na Wayne Rooney, Daniel Sturrudge pamoja na Jamie Vard kwani mfumo anautumia kocha wa kikosi hicho ni rahisi maadui kusoma mapema na kupelekea timu kutofanya vizuri. Amesema kwamba kupanga timu kwa bahati nasibu kutamgharimu, endapo atazingatia maboresho hayo na atatengeneza mazingira rafiki ya kusonga mbele katika michuano hiyo kwani inahitaji alama moja kufuzu 16 bora.

Kikosi cha Uingereza kinaundwa na jumla ya wanandinga 23 katika michuano ya faina ya Ero 2016 yanayofanyika huko Nchini Ufaransa ni ; Walinda mlangoJoe Hart (Manchester City), Fraser Forster (Southampton), Tom Heaton (Burnley).


Mabeki: Ryan Bertrand (Southampton), Gary Cahill (Chelsea), Nathaniel Clyne (Liverpool), Danny Rose (Tottenham), Chris Smalling (Manchester United), John Stones (Everton), Kyle Walker (Tottenham).
ViungoDele Alli (Tottenham), Ross Barkley (Everton), Fabian Delph (Manchester City), Eric Dier (Tottenham), Danny Drinkwater (Leicester), Jordan Henderson (Liverpool), Adam Lallana (Liverpool), James Milner (Liverpool), Raheem Sterling (Manchester City), Andros Townsend (Newcastle), Jack Wilshere (Arsenal)
Washambulizi: Harry Kane (Tottenham), Marcus Rashford (Manchester United), Wayne Rooney (Manchester United), Daniel Sturridge (Liverpool), Jamie Vardy (Leicester)
 

Post a Comment

Theme images by Maliketh. Powered by Blogger.