Na Yusuph Mwamba
Kumekuwa na wanasoka wachanga sana wenye vipaji vikubwa vya kusakata kabumbu, lakini mwisho wa siku unawakuta tayari wamepiga hatua kimaendeleo hii inatokana na mfumo wa soka wa Nchi husika na jinsi wanavyopewa matunzo ya kimpira kwa kuwa Taifa au vilabu wanavyochezea hutambua umuhimu wa kukuza vipaji hivyo hawana budi kuwalea katika malezi na sayansi ya mpira kwa maendeleo ya Soka lao lakini kwa Nchi zetu hapa Afrika Mashariki bado sna haswa kwa upande wa Tanzania.
Hapa simwingine tuna mzungumzia Nyota wa kimataifa wa Ubeligij na klabu ya A.S Roma ya Italia mwnandinga Radja Naiggolan.
HISTORA YAKE KWA UFUPI
Radja Naiggolan alizaliwa Nchi ya Ubeligij katika Mji wa Antwerp, Mei 4, 1988, pia ni mtoto wa tatu wa familia ya mzee Lizy Bogaerts yenye jumla ya watoto 3 na dada zake ni wachezaji wa mpira kama ilivyo yeye kiufupi ametoka kwenye familia ya mpira. Mama yake alifariki dunia mwaka 2010.
Lugha anazozungumza mwanandinga huyo ni pamoja na Kifaransa, Kibelgij, Kingereza, Kidachi pamoja na Kitaliano. Dhehebu lake ni muumini wa kanisa la Romania Cathoric.
MAISHA NDANI YA KLABU YA PIACENZA
Alijiunga na klabu ya Piancenza ya Nchini Italia 2005 na kufanikiwa kufunga jumla ya magoli 3 katika michezo 38 aliyoicheza tangu mwaka 2008 -2009, akiwa na umri wa miaka 17 akitokea kunako klabu ya K.F.C Germinal Beerscht
MAISHA NDANI YA KLABU YA CAGRIALI
Januari 27, 2010, alifanikiwa kujiunga na klabu hiyo yenye maskani yake Italia kwenye ligi ya Sirie A huku akiwa mchezaji wa mkopo wa klabu hiyo.
Radja akiwajibika uwanjani |
MAISHA NDANI YA AS ROMA
Kufikia mwaka 2014 januari alifanikiwa kujiunga kwa mkopo na klabu ya AS Roma ya Italia, akitokea kunako klabu ya Cagriali, na mchezo wake wa kwanza alianza kwa ushindi baada ya kufanikiwa kuifunga timu ya U.C. Sampdoria kwa bao 1-0 katika kombe la kopa Italia.
Pia alifanikiwa kuifikisha klabu hiyo katika hatua ya nusu fainali ya michuano ya klabu bingwa ulaya maarufu kama Uefa Champions League na kusadia Roma kuitoa klabu ya Juventus kwenye mashindano ya Uefa.
Mwaka 2014, Februari 22 alifanikiwa kufunga bao lake la kwanza akiwa na klabu yake ya AS Roma baada ya kuibuka na ushindi dhidi ya klabu ya Bologna FC wa bao 1-0, pia aliisaidia klabu ya AS Roma kuindosha mashindaoni klabu ya Fiorentina kwenye michuano ya Uefa .
Alisaini mkataba wa kudumu na klabu ya AS Roma 2015 baada ya kumalizika kwa msimu wa ligi hiyo kwa kiasi cha ada ya uhamisho wa Pauni milioni 9.
KUITWA TIMU YA TAIFA YA UBELGIJ
Mwanandinga huyo alianza kuitwa rasmi kwenye timu ya Taifa ya Ubelgihj Mei 29 mwaka 2009, mechi yake ya kwanza ilikuwa dhidi ya timu ya Taifa ya Chile ambapo Machi 5, 2014 alifanikiwa kufunga bao lake la kwanza kunako Taifa hilo baada ya kutuo sare ya mabao 2-2 kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya Taifa ya Ivory Coast , wakati huo hadi kufikia Mei 13, 2014 aliorodheshwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Ubelgij kwenye michuano ya fainali ya kombe la Dunia iliyofanyika Nchini Brazil na Ujerumani kufanikiwa kutwaa ndoo hiyo baada ya kuifunga timu ya Taifa ya Argentina kwa bao 1-0 lililowekwa kimyani na Mario Gotze.
Licha ya udogo wa jina lakje, lakini nyota huyo alitokea kuvivutia na baadhi ya vilabu vikubwa barani Ulaya ikiwemo klabu ya soka ya Chelsea ya Uingereza baada ya kumtangazia dau la pauni milioni 23, huku AS Roma wakidai pesa hiyo iongezwe hadi kufikia pauni milioni 32 ambapo kwa klabu ya Chelsea ilionekana kuwa kiasi hiucho cha fedha kuwa kikubwa na hakiendani na thamani ya nyota huyo.
Radja Nainggolan |
Post a Comment