Halloween party ideas 2015
Image

MANCHESTER CITY YABOMOA SAFU YA KIUNGO YA MELBOURNE CITY

Na Yusuph Mwamba


KLABU ya Soka ya Manchester City imekamilisha dili la kuinasa saini ya Kiungo wa kimataifa wa Australia nayekipiga kunako klabu ya Melbourne City, Aaron Mooy tayari kuwatumikia matajiri hao wa London katika msimu ujao wa mwaka 2016/2017.

Mooy, ambaye amefanikiwa kumaliza msimu wake 2015/2016 wa ligi kuu

ya Australia akifanikiwa kufumania nyavu mara 5 katika michezo yake 16 aliyocheza kunako klabu hiyo, amesaini kandarasi ya miaka3 na klabu hiyo mpaka 2019.


Mooy alyevaa jezi ya njano akiwajibika katika moja ya mchezo 
Mwanandinga huyo mwenye umri wa miaka 25, ameshawahi kuweka rekodi ya kuwa mwanasoka bora wa ligi hiyo ya Austaralia mara mbili katika msimu wake wa kwanza wa ligi hiyo  tangua ajiunge na klabu ya Melbourne mwaka 2014 na kufanikiwa kuibuka  kinara wa pasi za mwisho alizotoa kwenye ligi hiyo ya jumla ya pasi 21 huku akifanikiwa kufumania nyavu mara 11 katia huo msimu wa kwanza kuichezea klabu ya Melbourne City.

Kocha wa klabu ya Melbourne, John Van's Schip, alikuwa na haya ya kusema baada ya kumpoteza mwanandinga wake wa kutegemewa.

" Mooy ni mchezaji mzuri sana, alikuwa na mchango mkubwa sana kwetu lakini kama mchezaji ana uhuru wa kuchagua timu aitakayo na City imempa fursa basi naamini atafanikiwa huko aendapo".Alisema Schip.

Licha ya Kocha , Schip ya kuzungumza juu ya uwezo wa Mooy, lakini mkurugenzi wa Manchester City, Marwood, naye alisikika akiongea haya katika moja ya mitandao ya kijamii ya klabu ya Melbourne official Website juu ya kutua kwa nyota huyo kunako klabu ya City

"Mooy ni mchezaji mzuri sana, na ni mchezaji mwenye kipaji cha hari ya juu naamini kutua City kutaifanya klabu yetu kuwa bora haswa katika safu ya kiungo na pia kutampa faida kubwa ya kumfanya awe bora zaidi kwa vile city kuna vipaji vingi vitakavyo mletea changamoto katika timu hiyo na kumfanya afike mbali zaidi ya hapa alipo".Alisema Marwood 
Mooy Aaron akitambulishwa klabu ya Man City jana kwnye makaoo makuu ya klabu hiyo na mkurugenzi wa klabu ya City  Marwood

















Post a Comment

Theme images by Maliketh. Powered by Blogger.