Na Yusuph Mwamba
Huku michuano ya fainali ya Euro ikiendelea kushika kasi, maajabu mengine yalitokea jana wakati kukiwa na pambano kati ya timu ya Taifa ya Iceland dhidi ya timu ya Taifa ya Uingereza, lakini matokeo ya pambano hilo yaliwashtua wengi japo kwenye mpira lolote linawezekana.
Pambano la jana lilikuwa la kusisimua, huku Uingereza wakijikuta wakiyaaga mashindano hayo baada ya kuadhibiwa na wavuvi wa Iceland kwa jumla ya mabao 2-1 kwenye hatua ya mtoano ya kusaka timu zitakazo ingia robo fainali ya michuano hiyo ya fainali ya Euro 2016 yanayoendelea Nchini Ufaransa.
Uingereza ndiyo ilikuwa timu ya kwanza kuandika bao lake kunako dakika ya 4 ya mchezo kwa mkwaju wa penalti baada ya mshambuliaji wake Daniel Sturrdge kuangushwa kwenye eneo la hatari na Golikipa wa Iceland na refarii wa mchezo kuamuru penalti ipiogwe na nahodha wa kikosi hicho cha Hugdson Wayne Roioney kuipatia timu yake bao la kuongoza.
Kikosi cha timu ya Taifa ya Uingereza kilicho yaaga mashindano ya Eoru 2016 jana baada ya kudhibiwa na Iceland kwa jumla ya mabao 2-1 |
Kipindi cha kwanza kilimalizka timu hizo zikenda mapumziko huku Iceland wakiwa wanaongoza kwa jumla ya mabao 2-1, licha ya Uingereza kucheza vizuri na kuapata nafasi nyingi, pamoja na mabadiliko aliyo yafanya dakika ya 77 ya mchezo ya kuwatoa baadhi ya nyota wake kama Eric Dier na nafasi yake kuchukuliwa na Jack Wilshare,,Raheem Sterling nafasi yake kuchukuliwa na mwandinga anayekipiga Leicer City Jamie Vardy na kumtoa nahodha wa kikosi Wayne Rooney na nafasi yake kuchukuliwa na Marcaus Rashford lakini mabdiliko hayo hayakuweza kuzaa matunda na kujikuta wakitupwa nje ya michuano hiyo.
Kikosi cha timu ya Taifa ya Iceland kilichoisambaratisha Uingereza michuano ya Euro 2016 Jana baada ya kuidhibu jumla ya mabao 2-1 |
Kokosi cha Iceland kilichopo chini ya kocha Lars Lagerbaeck, kilifanya mabadfiliko yake baada ya kuwatoa baadhi ya nyota wake kama Kolbenn Sightharsson mfungajiwa bao la pili la Iceland na nafasi yake kuchukuliwa na Elmar Bjarnasson, huku akimtoa Jon Dad Boedvarsson na nafasi yake kuchukuliwa na Arnor Ingvi Traustason lakini mabadiliko hayo yaliweza kuwaletea matunda na kufanikiwa kuwatoa vigogo hao wa Uingereza.
Ikumbukwe kisiwa cha Iceland kinajumla ya wakazi wapatao 330,000 na asilimia ya wakazi hao ni wavuvi huku asili ya lugha yao ikiwa ni ki- Norwei, kufuzu kwake katika michuano ya Euro 2016 ilitokea baada ya kupata sare ya bao moja kwa moja 1-1 na timu ya Taifa ya Kazakhstan huku ilikuwa ikihitaji alama moja kuweza kuongoza kundi A.
Timu ya Uingereza ilicheza mfumo wa 4-3-3, huku Iceland wakicheza mfumo wa 4-4-2.
Mpaka sasa timu ambazo zimekwisha tinga hatua ya robo fainali ya michuano hiyo ya Euro 2016 ni pamoja na wenyeji wa fainali hiyo Ufaransa, Ubelgij, Italia, Ureno, Iceland na Ujerumani huku bingwa mtetezi akiyaaga mashindano hayo kwa kichapo cha mabao 2-1 dhidi ya Italia katika pambano lao la jana.
Michezo ya hatua ya robo fainali itachezwa julai 6 kwa 7, huku fainali ya michuano hiyo ya Euro 2016 inatarajia kufanyika Julai 10, 2016 Nchini Ufaransa
Post a Comment