Na Yusuph Mwamba
SHIRIKA la kimataifa la kupambana na rushwa Transparency International limesema rushwa kwenye jeshi la Nigeria inafifisha juhudi za kupambana na wapiganaji wa Boko Haram.
Shirika hilo linawashutumu maafisa kwa kutengeneza mikataba bandia ambapo wamekuwa wakiiba pesa kwa madai ya kununua vifaa muhimu.Transparency International |
Ripoti hiyo imesema hali hiyo imelifanya Jeshi kuwa na rasimali pungufu pamoja na kutokakuwa na mafunzo ya kutosha.
Msemaji wa Jeshi la Nigeria Meja Jenerali John Enenche amesema tuhuma hizo haziwahusu maafisa wa sasa Jeshi.
Amesema hatua kubwa zimefanyika kuboresha mafunzo na kuinua ari kwa vikosi vya jeshi
JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.wabunifumedia.blogspot.com ku-install App ya wabunifumedia, bila ya kuingia website
Tweet@wabunifumediaonline, youtube@wabunifumediaonline TV, Fb@wabunifumediaonline, insta@wabunifumediaonline
.
Post a Comment