Na Yusuph Mwamba
WATU waliopembezoni ambao wamekuwa na shida kubwa ya kupata madaktari bingwa, wataanza kupata nafuu baada ya kuanza kwa mradi wa tiba mtandao unaoendeshwa kwa pamoja kati ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi-Muhimbili, UNESCO pamoja na wadau wengine.
Hayo yalisemwa katika warsha ya siku mbili ya kujadili na kuiangalia dhana ya tiba mtandao na namna ya kuitekeleza.Kwa mujibu wa Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) Zulmira Rodrigues utoaji huo wa tiba mtandao kwa majaribio utaanza mapema zaidi kabla ya mwezi Oktoba mwaka huu.
Mratibu wa E-Medicine kutoka Idara ya Tiba Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dr. Liggy Vumilia akisoma hotuba kwa niaba ya Katibu Mkuu wa wizara hiyo wakati wa ufunguzi wa warsha ya siku mbili ya kujadili na kuiangalia dhana ya tiba mtandao na namna ya kuitekeleza inayoendelea katika ukumbi wa MUHAS jijini Dar Es Salaam.
Alikuwa anatarajia mifumo yote kuwa tayari ifikapo Julai na hivyo kuwa na nafasi ya kuwa katika matibabu ifikapo Oktoba. Katika warsha hiyo aliwahimiza wataalamu kujadiliana kiundani changamoto mbalimbali na namna ya kuweka ripoti ili kuja kusaidia wakati mradi utakapoenda kitaifa.
Katika warsha hiyo iliyokutanisha wataalamu mbalimbali wa tehama na madaktari kutoka Arusha, Manyara, Kilimanjaro na Dar es Salaam Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Mpoki Ulisubisya katika hotuba yake ya ufunguzi iliyosomwa na Dk Liggyle Vumilia alielezea matumaini yake kuhusiana na mradi huo wa majaribio.
Aliwataka washiriki wa warsha hiyo kuona uwezekano wa kuanza mradio huo mapema zaidi baada ya kuhakikisha kwamba dhana imekubalika na namna ya kuitekeleza inaeleweka miongoni mwa wadau.
Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi-Muhimbili (MUHAS), Prof Eligius Lyamuya alipokuwa akitoa neno la ukaribisho kwa washiriki wa warsha ya siku mbili ya kujadili na kuiangalia dhana ya tiba mtandao na namna ya kuitekeleza inayoendelea chuoni hapo jijini Dar es Salaam.
Mradio huo unaoanza kwa majaribio kufuatia juhudi za UNESCO zilizoanzishwa kwa msaada wa Samsung unahusisha zaidi wagonjwa wanaoweza kufika kupata matibabu katika kijiji cha kidigitali cha Ololosokwan na kwa kuanzia huduma hiyo itatolewa kwa mama na mtoto na afya ya kinywa, masikio, pua na koo (ENT), ambapo mabingwa kutoka KCMC na MUHAS wanaweza kufanya tiba kwa kutumia mtandao.
Kliniki ya Digitali ilizinduliwa katika kijiji cha Ololosokwan Ngorororo, Arusha mnamo mwezi Novemba mwaka 2016.
Wataalamu hao kutoka Shirika la Afya Duniani, Mwakilishi wa Tamisemi, Wizara ya Afya, DMO wa Ngorongoro, wataalamu kutoka KCMC na MUHAS wamekutana jana katika Kampasi ya Muhimbili (MUHAS), ili kuangalia dhana mpya kwa ajili ya utoaji huduma za afya kwa njia ya mtandao katika kijiji cha Wamasai, Mkoani Arusha cha Ololosokwan.
Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO), Zulmira Rodrigues akizungumza katika warsha ya siku mbili ya kujadili na kuiangalia dhana ya tiba mtandao na namna ya kuitekeleza inayoendelea jijini Dar Es Salaam
Kijiji hicho tayari kina uwezo wa kupata huduma hizo.
Mradi huo ukifanikiwa unatarajiwa kupanuliwa kwenda sehemu mbalimbali zinazohitaji matibabu ya mabingwa lakini uwezo wa kufika huko haupo.
"Dhana hii itawezesha kuendelea na utoaji wa huduma bora za afya, zenye ufanisi wa kitaalamu zaidi katika maeneo ya vijijini, ambayo mara nyingi huachwa nyuma katika utoaji wa huduma hizo," alisema Zulmira na kuongeza kuwa dhana ya utabibu mtandao inalenga hasa kuinua utumiaji wa teknolojia ya kidigitali ya kisasa, ambapo utekelezaji wake utakuwa mfano elekezi wa kuboresha matumizi ya teknologia katika karne ya ishirini na moja katika utoaji wa huduma za afya nchini na barani Afrika.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria Tanzania (OUT), Prof. Elifas Bisanda akitoa neno katika warsha ya siku mbili ya kujadili na kuiangalia dhana ya tiba mtandao na namna ya kuitekeleza inayoendelea katika ukumbi wa MUHAS jijini Dar Es Salaam.
Warsha inayochambua dhana ya tiba mtandao ni awamu ya pili yenye kuendeleza juhudi za kutumia uwapo wa huduma hiyo Ololosokwan kwa kuwakutanisha wabunifu, wataalamu wa afya na wanateknolojia ili kudadavua dhana ya utekelezaji kamilifu wa jaribio la utoaji wa huduma za afya kwa kutumia teknolojia ya kisasa, na baadaye kuirasimisha kama mfumo wa kuboresha afya maeneo yaliyo pembezoni ya miji na vijijini.
Katika warsha hiyo washiriki walipata nafasi ya kushuhudia utiaji saini wa makubaliano kati ya Unesco na MUHAS wa ushirikiano katika utekelezaji wa dhana hiyo ya tiba mtandao.
Akifafanua zaidi Dk Vumilia alisema kwamba tiba mtandao itahusisha upasuaji mdogo ambao utafanywa na wataalamu waliopo katika kliniki za kijiji hicho wakielekezwa na mtaalamu bingwa.
JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.wabunifumedia.blogspot.com ku-install App ya wabunifumedia, bila ya kuingia website
Tweet@wabunifumediaonline, youtube@wabunifumediaonline TV, Fb@wabunifumediaonline, insta@wabunifumediaonline
.
Post a Comment