Na Mwandishi wetu
SERIKALI imeshauriwa
kubadili sharti la mtu anayetaka kujenga shule binafsi kuwa na ukubwa wa ekari tatu kutokana na sharti
hilo kuwa kikwazo kwa Watanzania wenye mtaji mdogo kushindwa kumiliki shule.
Mwenyekiti wa Bodi ya Shule binafsi ya Decent English Medium, Baraka Koka, akipandisha bendera ya Taifa baada ya kutembelewa na waandishi wa habari hivi karibuni |
Ushauri huo ulitolewa na Mwenyekiti wa Bodi ya
Shule binafsi ya Decent English Medium iliyopo eneo la Buyuni mtaa wa Mgeule
Juu, Kata ya Buyuni Ilala jijini Dar es Salaam, Baraka Koka wakati akizungumza
na waandishi wa habari waliotembelea maendeleo ya elimu katika kata hiyo.
Alisema sharti hilo la
serikali ni mpango mzuri wenye nia ya kupunguza msongamano wa wanafunzi
darasani ingawa ni muhimu sharti hilo kutazamwa upya hasa maeneo ya mijini
ikiwa ni pamoja na kupunguza kutoka umiliki wa akari tatu kuwa angalau ekari
mbili.
“Sisi hatupingi uamuzi
huu, ila tunaiomba serikali yetu sikivu kubadili sharti hili kutokana na bei
kubwa na gharama za umiliki wa ardhi kwa maeneo ya mijini. Sisi tunaamini
kwamba kiwanja cha ukubwa wa ekari mbili ikikiwa na mchoro mzuri yanapatikana
madaraka makubwa ya kutosha ya
idadi ya wanafunzi 45 kwa darasa
kulingana na takwa la sera,”alisema.
Alifafanua kuwa umiliki
wa ekari mbili utatoa fursa zaidi kwa Watanzania
ambao wameshindwa kununua ardhi, kumudu gharama za kupima licha ya kuwa na shauku ya kusaidia juhudi za serikali
za kuongeza wasomi na kuondoa tatizo la ujinga hapa nchini.
Mwalimu mkuu msaidizi
wa shule hiyo, Twamilway Kidala alisema shule yake imefanikiwa kutimiza sharti
la kisera la kutumia mtaala wa Tanzania kufundishia.
Alisema kitaalamu
mitaala huandaliwa kulingana na mazingira ya
taifa husika ingawa suala hilo limekuwa likipuuzwa na shule nyingi
binafsi kutumia mtaala wa nje kufundisha jambo ambalo huweza kumuathiri
mwanafunzi pindi mzazi anaposhindwa kumudu kulipa ada hadi mwisho wa masomo au
elimu ya ngazi husika.
“Sisi tumeweza kutimiza
wajibu huu wa kisera na kumekuwa na mapokeo mazuri kwa wazazi…tunawapokea
wanafunzi wa ngazi zote bila kujali hali ya kipato cha mazazi ikiwamo
kugharamia ada kwa wanafunzi yatima, kwasasa tuna gharamia mwanafunzi mmoja
yatima,”alisema.
Alisema shule yake ina madarasa ya kutosha, magari ya
shule, jengo la utawala na mpango ni kujenga jengo kubwa la ghorofa ili kuongeza madarasa na idara mbalimbali.
“Uongozi wa shule
tunawakaribisha wazazi kuleta watoto wao kusoma hapa na kwa muda mfupi
watabaini tofauti yetu kitaaluma, kimaadili kulinganisha na maeneo
mengine,”alisisitiza Kidala.
Shule ya Decent English
Medium ni mojawapo kati ya shule zenye
mzingira mazuri, eneo kubwa, viwanja vya michezo na mandhari ya kuvutia yanayomfanya
mwanafunzi kusoma kwa utulivu na kuelewa.
JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.wabunifumedia.blogspot.com ku-install App ya wabunifumedia, bila ya kuingia website
Tweet@wabunifumediaonline, youtube@wabunifumediaonline TV, Fb@wabunifumediaonline, insta@wabunifumediaonline
Tweet@wabunifumediaonline, youtube@wabunifumediaonline TV, Fb@wabunifumediaonline, insta@wabunifumediaonline
Post a Comment