Na Mohamed Ally, TSJ
HALMASHAURI ya Manispaa ya Ilala jijini Dar es
Salaam imeitaka mitaa ambayo haina soko kuandika barua kwa Mkurugenzi wa
manispaa kuhusu ombi hilo kupitia afisa mtendaji wa kata husika.
Ushauri huo ulitolewa mapema wiki hii na Afisa
Masoko Mkuu wa Manispaa hiyo, Solomoni Mushi,
katika mahojiano maalumu na mwandishi wa habari hizi aliyetaka ufafanuzi
wa Manispaa kuhusu malalamiko ya wakazi wa mitaa miwili ya Mgeule na Mgeule Juu,
kata ya Buyuni katika Manispaa hiyo kukosa huduma ya soko.
Alisema kumekuwa na malalamiko miongoni mwa wananchi
katika baadhi ya mitaa ya Manispaa hiyo kufuata huduma hiyo maeneo ya mbali na kusema kuwa baadhi ya mitaa na kata hawana
ufahamu kuhusu taratibu za kuwa na soko.
“Ujenzi wa soko unafuata ramani ya Manispaa. Kama
upo mtaa ulitenga eneo kwa ajili ya soko au eneo la wazi kwa ajili ya huduma za
jamii, wakazi wa mtaa husika wanapaswa kuandika maombi kupitia kwa afisa
mtendaji wa kata (WEO), “alisema na kuongeza:
WEO ataitisha mkutano kati ya wakazi, viongozi wa
mtaa akitushirikisha sisi watu wa biashara
na masoko, tuko tayari kuwasaidia.
Katika kufanikisha mpango hup aliwataka vongozi wa
mitaa hasa pembezoni mwa jiji
kusaidia utekelezwaji wa sheria ya
mipango miji na matumizi bora ya ardhi kwa kutenga maeneo ya huduma za jamii
ili kupunguza gharama pindi serikali inapoamua kupeleka huduma hizo.
Wakazi wa Mtaa wa Mgeule Juu, wakiwa katika mkutano na waandishi wa habari WM , baada yawaandishi hao kutembelea mtaa huo ili kujua kero za wananchi wa eneo hilo (PICHA ETHAN MSUYA) |
Alifafanua kuwa serikali ina wajibu wa kupeleka
huduma za jamii kwa wananchi kwenye maeneo yaliyopangwa lakini wakati mwingine
inashindwa kutokana ujenzi holela
kutokana na baadhi ya viongozi wa mitaa kuuza maeneo bila utaratibu.
Wakazi wa Mtaa wa Mgeule Juu, wakitoa kero zao mbele za waandishi wa habari wa WM, hivi karibuni baada ya kutembelewa na waandishi hao (PICHA ETHAN MSUYA). |
Alisema lengo
la serikali ni kuona kila mwananchi anajiinua kiuchumi kupitia fursa
zilizopo, kulipa kodi ili inayopatikana kuingia serikalini na kutumika kuleta
maendeleo.
Awali wakizungumza kwa nyakati tofauti na timu ya
waandishi wa habari waliotembelea miradi ya maendeleo katika mitaa hiyo iliyopo
nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam wananchi hao waliilalamikia Manispaa hiyo
kushindwa kuwapelekea huduma muhimu ya soko.
Mmoja wa wananchi hao, Zaituni Omary mkazi wa Mgeule
Juu alisema wamekuwa wakilazimika kusafiri
kwenye masoko ya mbali kwa zaidi ya kilometa sita hadi saba kununua
mahitaji kata kama wanahitaji kununua
bidhaa ya bei ya chini.
“Hata tunalazimika kwenda Chanika mwisho na Pugu,
unalipa nauli ya Sh.2,000 kwenda kununu
bidhaa za 5,000, kweli hii ni haki?”, alihoji Omary.
Naye Elizabert Mwakapangala mkazi wa Mgeule
alisema ukosefu wa soko kwenye eneo hilo
kumechangia wananchi wengi hasa wanawake kushindwa kuthubutu shughuli za
ujasiriamali
kushindwa
kuanzisha biashara ndogondogo
shughuri za kibiashara kukwama kwani wakazi wanashindwa
kufanya biashara ndogondogo ingawa ndio chanzo cha viwanda
"Tunashukuru
juhudi za baadhi ya viongozi wa mtaa wetu
kuhakikisha tatizo hili linafikia tamati lakini bado juhudi hazijazaa
matunda hivyo tunaiomba Manispaa ituangalie kwa jicho la huruma,”alisema.
Mjumbe wa kamati ya maendeleo ya serikali ya mtaa wa
Mgeule Juu, Baraka Koka alisema juhudi za pamoja kati ya wananchi, uongozi wa
mtaa zinafanyika ili kuzungumza na wakazi wenye maeneo makubwa ili kupata eneo
la soko.
Mjumbe wa kamati ya maendeleo ya mtaa wa Mgeule Juu , Baraka Koka, akizungumza na waandishi wa habari wa taasisi ya Wabunifumedia walipotembelea mtaa huo hivi karibuni( PICHA ETHAN MSUYA). |
Kwa upande wake mjumbe wa kamati ya maendeleo ya
mtaa wa Mgeule, Maliki Shemtandulo alisema mtaa huo umetenga eneo la zaidi ya
ekari mbili kwa ajili ya soko, ingawa tatizo lililopo ni ukata hivyo kushondwa
kufanikisha ujenzi wa mradi huo.
Hivi karibuni timu ya waandishi wa taasisi ya habari
ya Wabunifu na ile ya Wandishi wa Habari za Uchunguzi, Sauti ya wasiokuwa na
sauti vijijini (TTAJA) walitembelea mitaa hiyo na kubaini changamoto mbalimbali
zikiwamo maji safi na salama, shule, zahanati, barabara na daraja.
Tweet@wabunifumediaonline, youtube@wabunifumediaonline TV, Fb@wabunifumediaonline, insta@wabunifumediaonline
Post a Comment