Halloween party ideas 2015
Image

Na Yusuph Mwamba
MLINZI wa kushoto wa Kimataifa wa Ghana na  klabu ya soka ya Chelsea ,Baba Rahman ,yupo kwenye hatua za mwisho za kuafanyiwa vipomo vya afya na klabu ya soka ya  Schalke ili kujiunga na klabu hiyo katika msimu huu wa usajili kwa mkopo.
Baba Rahman
Rahman, mwenye umri wa miaka 22, alijiunga na klabu ya soka ya Chelsea akitokea kunako klabu ya  Augsburg msimu uliopita na kusaini kandarasi ya miaka mitano katika Dimba la Stamford Bridge  na kushindania namba na Mhispainia  ,Azpilicueta, aliyekuwa  chaguo la kwanza  katika kikosi cha The Blues  msimu uliopita.
Antonio Conte ,akizungumza na mlinzi wake wa kushoto wa Chelsea ,Cesar Azpilicueta a katika maandalizi ya msimu wa ligi kuu ya  EPL mwaka 2016/2017
Baba Rahma, mwenye uraia wa Ghana, mpaka sasa amefanikiwa kucheza jumla ya michezo 23 ya ushindani katika klabu hiyo msimu wa 2015/2016 lakini amekuwa ni miongoni mwa nyota ambao hawapo kwenye mipango ya  Meneja mpya wa klabu hiyo ,Antonio Conte, licha ya kutakiwa Bundasliga. 

Ujio wa Meneja mpya wa klabu ya soka ya Chelsea ,Conte, mpaka sasa ameonesha dhamira ya kujenga timu na kuwaondoa kwa mikopo wachezaji wake chipukizi ili wakakuze upya vipaji vyao na waendane na hali ya ushindani, miongoni mwa nyota vijana waliowashiwa taa nyekundu ni pamoja na  Nathan Ake, Charly Musonda and Lewis Baker
Rahman , ameshatumikia jumla ya miaka mitatu akiwa Ujerumani kabla ya kujiunga na Chelsea, huku akiwa ametumikia miaka miwili ligi ya Bundesliga 2 akiwa na klabu ya  Greuther Furth, ambapo amecheza jumla ya michezo 48 akifanikiwa kufunga magoli mawili.
Hata hivyo, safari ya mwanandinga huyo mpaka kufikia kunako klabu ya soka ya Chelsea, ilianzia Bundesliga 2 akiwa na klabu ya  Greuther Furth kisha kujiunga na klabu ya Bundesliga ya Augsburg mnamo Agosti, 2014 na kufanikiwa kumaliza vyema msimu wa mwaka 2013/2014 kunako klabu yake aliyochezea jumla ya michezo 31 na baada ya hapo alijiunga na klabu ya soka ya  Chelsea. 
Wakati huo  baba akiwa katika mipango ya kuihama Chelsea, Meneja Conte, amesema kuwa hana uhakika kama Mshambuliaji wa zamani wa Kimataifa wa Hispainia, Diego Costa kama atabakia kunako klabu hiyo au atachukua uamuzi wa kuondoka licha ya kuwa na mipango naye msimu ujao.
JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.wabunifumedia.blogspot.com ku-install App ya wabunifumedia,  bila ya kuingia websiteTweet@wabunifumediaonline, youtube@wabunifumediaonline TV, Fb@wabunifumediaonline, insta@wabunifumediaonline





Post a Comment

Theme images by Maliketh. Powered by Blogger.