Halloween party ideas 2015
Image

Na Yusuph Mwamba

DIRISHA  la usajili la msimu huu kwa vilabu vya soka barani Ulaya linazidi kuvutia zaidina kutia hamasa, huku tukishudia  vilabu vingi sasa vikiwa katika mipango ya kutaka kuwarudisha katika timu zao wachezaji wao wa zamani kwa gharama kubwa wakati waliwaacha waondoke kirahisi misimu kadhaa iliyopita.

Hapa tunakuja kupata funzo kubwa kupitia kwa Wachezaji wa Kimataifa na Wakitaifa  na kutufanya kujua utofauti wa wachezaji wetu walioachwa na timu zao kwa ajili ya kurekebisha viwango vyao na wachezaji wa Ulaya ambao nao walifanya hivyo baada ya vilabu vyao kutoridhishwa na viwango vyao licha ya figisu figisu kuhusishwa


Soka la sasa limekuwa ni ajira tofauti na miaka ya nyuma ambapo miongoni mwa wachezaji walikuwa wakijitolea na kufanya ridhaa kwa taifa lao shauri ya kutetea uzalendo kwa Taifa lao

Licha ya kuwa nia ajira lakini tumekuwa tukishuhudia soka letu kuendeshwa katika mfumo holela usio na mageuzi huku tukishuhudia soka letu la Tanzania kutawaliwa na vilabu kongwe yani Simba na Yanga licha ya Azam FC kuja kuleta mapinduzi ya soka japo nayo kwa sasa imeonekana kutawaliwa na U -simba na U- Yanga jambo ambalo limeifanya klabu hiyo kuanza kupoteza ubora wake.

Hata katika Ligi yetu, bado swala la timu kujiendesha limekuwa ni changamoto kubwa sana, hii inataokana na baadhi ya timu zote kukosa udhamini wa kutosha na wawekezaji na badala yake timu kuendeshwa na kikundi cha watu wachache tena kwa kutoa pesa zao mfukoni kitu ambacho ni jambo la aibu na kupelekea kutokuwa na maendeleo kisoka.


Hali ya kukosa wadhamini imechangia kwa kiasi kikubwa huku tukiona baadhi ya vilabu vikipanda daraja na hatimaye kushuka tena je kwa hali hii hata wale wachezaji wanaotolewa kwa mkopo katika hivi vilabu watakuza viwango vyao ipasavyo? jibu hapa ni ngumu sana kwahiyo hili ni tatizo tofauti na ulaya hali kwao ni shwari kabisa


Mfumo mbovu wa uendeshwaji wa ligi nao ni kikwazo kwa wachezaji wetu kukuza taaluma yao ya soka na kufanya apige hatua, hii inapelekea wachezaji kujihusisha na ligi za mchangani maarufu kama Ndondo cup kwa ajili ya kuimarisha kiwango chake na kujitafutia ridhiki nyingine katika kujikimu na maisha japo si jambo zuri kwa Proffesional Player kudili na ndondo kwani endapo atapata madhara itaigharimu klabu yake na maisha yake ya soka.


Tukitazama kwa upande wa pili, wachezaji wetu wamekuwa wavivu na wazito sana kujituma, jambo ambalo hupelekea kushuka kiwango na kufanya kiwango chake kuwa cha msimu tofauti na wachezaji wa Ulaya wao wamekuwa wepesi sana kujituma na kujua nini anatakiwa kufanya awapo nje au ndani ya Uwanja.


Soka la sasa limekuwa na ushindani wa hali ya juu, kila siku unatakiwa kuonesha kiwango tofauti na jana, mchezo wa soka ni mchezo mgumu sana ni nikazi ngumu ambayo unatakiwa uwe bora kila siku iitwayo leo na  kama utakuwa mzembe na mvivu lakini kama utazingatia matakwa ya mchezo huo utafanikiwa na kupiga hatua ya kimaendeleo na kufikia lengo ulilojiwekea mwanzo.


Nini maana ya kutolewa kwa mkopo? mkopo hutolewa endapo uongozi wa klabu ukishirikiana na Benchi la Ufundi uliopo chini ya kocha mkuu kutokubaliana na uwezo wako uwanjani na kutokuwa chaguo lake basi maamuzi mawili yanaweza kutolewa aidha kukuuza au kukutoa kwa mkopo ikiwa na lengo la kutafuta kasi zaidi mahala fulani ili uendabe na kasi ya mchezo autakao.


Pia, mchezaji anaweza kutolewa kwa mkopo endapo kutakuwa na maelewano mabaya baina ya Uongozi na mchezaji au kutokuwa na mahusiano mazuri baina ya mchezaji na  benchi la ufundi likiwa chini ya kocha au kikiuka maagizo ya kocha na kadharika basi mchezaji anaweza kutolewa kwa mkopo kwa makubaliano maalumu au kama mkataba wake umeisha basi atakuwa mchezaji huru na kujiunga na klabu aitakayo.


Miongoni mwa wachezaji walioondoka kunako klabu zao kwa bei chee na kutakiwa kurudi kwa bei ya gharama kama wafalme ni pamoja na ;



POUL POGBA
Huyu ni nyota wa kimataifa wa Ufaransa na klabu ya soka ya Juventus ya Italia. mwanandinga huyo ni miongoni mwa wachezaji walioifikisha timu yao ya Taifa ya Ufaransa kaitka hatu ya fainali ya michuano ya Euro 2016 licha ya kulikosa kombe hilo pamoja na kuwa wenyeji wa mashindano hayo.

Pogba, ambaye ameingia katika orodha ya wachezaji waliotengeneza umaarufu katika dirisha la usajili msimu huu nchini Italia huku akifuatiwa na mwanandinga wa kimataifa wa Argentina Higuain ambaye ametua hivi karibuni kunako klabu ya Juventus.

Mpaka sasa klabu ya soka ya Manchester United, wametenga kiasi cha Euro milioni 111 kama dili la uahmisho wa Pogba, huku akiwa aliondoka buree mwaka 2013 wakati kikosi hicho kipo chini ya aliyekuwa meneja wa klabu ya United, Sir Alex Furguson

ALVARO MORATA
Klabu ya soka ya Real Mdrid nayo wapo katika mapngo wa kumrjesha mashambuliaji wa kimaaifa wa Hispainia Alvaro Morata, aliyetumikia klabu hiyo baada ya kuhamia kunako klabu ya soka ya Juventus msimu uliopita.

MARIO GOTZE
Klabu ay soka ya Borussia Dortmund, wamemrejesha nyota wao wa kimataifa wa Ujerumani na aliyekuwa klabu ya soka ya Real madrid ,Mario Gotze mwenye umri wa miaka 23.



ROMELU  LUKAKU

Klabu ya Chelsea nayo ipo mbioni kutka kunasa saini ya Mshambuliaji wa kimataifa wa Ubelgij Romelu Lukakau anyaekipiga kunako klabu ya soka ya Everton ambaye kabla ya kutua Everton alikipiga kunako klabu ya Chelsea na sasa anarejeshwa kwa nia ya kuimarisha safu ya ushambuliaji inayoongozwa na Mbelgij Eden Hazard na Mhispainia Diego Costa ambaye huendenda akatimka klabu hiyo japo mpaka sasa hajathibitisha rasmi.
Lakini dau la Lukaku linaonekana kutaka kuweka rekodo huku akitaka kiasi cha kitita cha Euro milioni 80 ili kuishawishi klabu ya soka ya Everton na kujiunga Stamford Bridge

Hizo ni Baadhi ya Sajili zinazotikisa Dunia kwa sasa, ikiwa ni wachezaji walitumikia timu hizo mwazo wakiwa kaika mipango ya kurejeshwa kwa mamilioni ya pesa, je tunajifunza nini hapa? wachezaji wetu nyanyukeni na kuanza harakai za kufanya vizuri ili kunufaika na kuwa miongoni mwa watumwa waliogeuka kuwa wafalme.


JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.wabunifumedia.blogspot.com ku-install App ya wabunifumedia,  bila ya kuingia websiteTweet@wabunifumediaonline, youtube@wabunifumediaonline TV, Fb@wabunifumediaonline, insta@wabunifumediaonline





Post a Comment

Theme images by Maliketh. Powered by Blogger.