Halloween party ideas 2015
Image

Na Yusuph Mwamba
KLABU ya soka ya Manchester City wamekamilisha uhamisho wa Winga  wa  Kimataifa wa Ujerumani na klabu ya soka ya Schalke 04  ya Ujerumani baada ya kufanikiwa kunasa saini ya winga , Leroy Sane aliyezaliwa kaitika mji wa wa Essen, Nchini Ujerumani.
Sane, mwenye umri wa miaka 20, amefanikiwa kutua kunako klabu ya soka ya Manchester City  ndani ya Dimba la Etihad Stadium kwa dau la ada ya uhamisho wa paundi milioni 37 huku akitia saini ya kandarasi ya miaka mitano.

Mwanandinga huyo, alifanikiwa kumaliza msimu wa ligi kuu ya Bundesliga  wa 2015/2016 baada ya kufanikiwa kufumania nyavu mara sita huku akiwa na pasi za mwisho ( assists) sita katika klabu yake ya Schalke04
Usajili huo unakuwa usajili wa pili wa Meneja mpya wa klabu hiyo Pep Guardiola, uliotumia pesa nyingi kufuatia usajili ulimalizika wa nyota Nolito kutoka Celta Vigo kwa dau la Euro milioni 13.8
Taarifa zaidi juu ya mwanandinga huyo ya jezi atakayo ivaa nyota baada ya kudondosha saini , mtandao wa klabu hiyo  Official website  kimeripoti kuwa, Sane atapewa jezi namba 9
"Nina furaha sana najisikia vizuri  , unapofanya kazi kisha ukatoka nje inanipa matumaini ukizingatia City ni miongoni mwa vilabu vikubwa  sana Duniani, moja ya sababu ya kujiunga City ilikuwa ni ushawishi wa  Pep Guardiola, najua nitajifunza mengi kutoka kwake na kufanikiwa kupiga hatua zaidi ya hapa nilipofika".Alisema Sane
Licha ya Sane kutua City, bado amekuwa na imani juu ya kocha huyo na kummwagia sifa kedekede baada ya kukiri kupata ujuzi zaidi pindi alipokuwa anafanya naye kazi akiwa naye kunako vilabu viwili tofauti yani klabu ya  Barcelona  na klabu ya  Bayern Muniches kipindi akiwa chipukizi 
"Nafikiri anaweza kunisaidia mimi kuwa mchezaji bora na aliyekamilika, nafikiria huu ndio wakati wangu wakupambana ili niweze kuanza katika kikosi cha kwanza kwasababu hii ni ligi kubwa na imejaa na ushindani wa hali ya juu na kuna kila aina ya wachezaji ambao watanifanya niwe bora zaidi na kuleta chngamoto ndani ya klabu yangu". Aliongeza Sane

JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.wabunifumedia.blogspot.com ku-install App ya wabunifumedia,  bila ya kuingia websiteTweet@wabunifumediaonline, youtube@wabunifumediaonline TV, Fb@wabunifumediaonline, insta@wabunifumediaonline

Post a Comment

Theme images by Maliketh. Powered by Blogger.