Na Yusuph Mwamba
HUKU pazia la usajili likiendelea kushika kasi barani ulaya na Mataifa mbalimbali kwa ajili ya kuimarisha timu ili kuleta ushindani katika ligi zao, Meneja wa klabu ya Arsenal, Mzee Wenga ameonekana kuvutiwa zaidi na mwanandinga wa klabu ya Lyon Alexandre Lacazette.
Lacazette, mwenye umri wa miaka 25, amefanikiwa kumaliza msimu wa 2015/2016 baada ya kuzifumania nyavu mara 92 katika jumla ya michezo 230 aliyoicheza akiwa na klabu yake ya Lyon katika ligi 1 Nchini Ufaransa.
Kufuatia hatua hiyo ya Arsenal kutaka kuimarisha kikosi chake, naye Meneja wa klabu hiyo ya Lyon,Bruno Genesio mwenye umri wa miaka 29, amethibitisha kuwa na mipango na mwanandinga huyo na kuifanya klabu ya Arsenal kuwa na matumaini hafifu ya kunasa saini ya nyota huyo.
Dau ambalo lingemuwezesha nyota huyo kutua Emirates ilikadiriwa kufikia kiasi cha kitita cha fedha chenye thamani ya Paundi milioni 30, kiasi ambapo kilionekana kuwa kikubwa mno na kumfanya Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger, kuwataka wakae mezani ili kujadiri upya dau hilo.
Akizungumza na chanzo chetu cha Sky spors, Meneja wa klabu ya soka ya Lyon alikuwa na haya ya kuyazungumza;
"Kuna baadhi ya ofa ambazo huwezi kuzikataa, lakini kwa ofa ambayo klabu ya Arsenal wameitoa nafikiri itakuwa ngumu, lakini kama Lyon wataamu maamuzi yao anaweza akaondoka kunako klabu hiyo lakini mimi kama kocha kwa fikira yangu sitapenda aondoke nataka abakie kwakuwa ni mtu muhimu sana katika timu yetu ".Alisema Genesio
Licha ya kocha huyo kuthitisha kutouzwa kwa nyota huyo, naye Rais wa klabu ya Lyon,Jean-Michel Aulas, amesema kuwa atahakikisha kuwa nyota huyo hauzwi kwa gharama yoyote ile.
"Nimehakikishiwa na Rais wetu na kusema atafanya juu chini kumbakiza nyota huyo lakini kamwe hutuwezi tukajua nini kitatokea mbeleni kikubwa tusubirie mpaka kufungwa kwa pazia la usajili Augusti 31, 2016 ndipo majibu kamili yatapatikana" Aliongeza Genesio

Post a Comment