Na Yusuph Mwamba
IMEKUWA ni kitu cha kawaida pindi makocha wanapofanya vibaya na kupelekea kibarua chake kuota nyasi, na sio makocha tu bali hata wachezaji nao wamekuwa katika wimbi hilo, hili sio jambo geni machoni mwetu, hata kama unamkataba watavunja ili mradi mambo yaende sawa, lakini jipya limeibuka baada ya leo aliyekuwa kocha wa zamani wa Manchester United, David Moyes, ametema sumu na kusema kuwa hakufanyiwa haki katika kufukuzwa kazi kunako klabu hiyo.
Moyes, mwenye uraia wa Scotl
and, ambapo ndipo alipozaliwa aliyekuwa Meneja wa zamani wa klabu hiyo, Sir Alex Furguso, kwa hali hiyo uswahiba nao ulionekana kuchukua nafasi baada ya Furguson kupendekeza jina lake na kurithi mikoba yake kunako klabu hiyo.
Mkataba alioingia nao Moyes Manchester United , ni mkataba wa muda wa miaka sita, lakini kibarua kilionekana kumshindwa baada ya matokeo mabaya aliyoyapata na kuifanya klabu hiyo kushika nafasi ya saba na kukosa michuano ya Klabu bingwa baada ya kutupwa nje kwenye michuano ya Europa ligi msimu wa 2013/2014.
Baada ya kutupiwa Virago na Manchester United, alifanikiwa kupata kibarua kipya Nchini Hispainia cha kuinoa klabu ya soka ya Real Sociedad, huku akimuachia mikoba Mholanzi ,Louis van Gaal, ambaye alifanikiwa kumaliza ligi United ikishika nafasi ya nne na kuwa miongoni mwa timu zilizo shiriki kombe la Europa na kufanikiwa kulibeba chini ya Van gaal licha ya kuchukua maamuzi magumu ya kumfukuza kazi na nafasi yake kuchukuliwa na Jose Mourinho msimu huu.
Moyes, anaamini kuwa, alikuwa ni mtu sahihi kuinoa Manchester United, baada ya Furguson kujihudhuru, imani yake imekuja baada ya kuongoza klabu ya Everton kutoka nafasi ya chini katika ligi hadi kuingia tano bora na kufanikiwa kushiriki michuano ya Europa ligi bila kutambua Everton ni klabu ndogo zaidi ya Manchester United.
"Huwezi kupata ofa kubwa za kifundisha vilabu vikubwa kama Real Madrid, Barcelona, Manchester United, bila ya kuwa na sababu ya msingi, kwahiyo kitendo cha United kunifukuza kilinidharirisha kwa kuwa nilisaini miaka sita lakini nilijikuta natumikia klabu kwa muda wa miezi kumi jambo ambalo hawakutenda haki kwa upande wangu".Alizungumza Moyes katika magazeti ya Taifa
Kwa sasa, Moyes, ni kocha wa klabu ya soka ya Sunderland, amechukua nafasi hiyo baada ya aliyekuwa kocha wa zamani wa klabu hiyo Sam Allardyce, kukabidhiwa mikoba ya kukinoa kikosi cha timu ya Taifa ya Uingereza kufuatia kujiuzuru kwa aliyekuwa kocha wa Taifa hilo Roy Hugdson baada ya matoke mabaya aliyoyapata kwenye michuano ya fainali ya kombe la Euro 2016 yaliyofanyika Ufaransa.
JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.wabunifumedia.blogspot.com ku-install App ya wabunifumedia, bila ya kuingia websiteTweet@wabunifumediaonline, youtube@wabunifumediaonline TV, Fb@wabunifumediaonline, insta@wabunifumediaonline
Post a Comment