Halloween party ideas 2015
Image

Na Yusuph Mwamba 

KAMPUNI ya Am art Promotion kwa kushirikia na Kanumba The Great Company leo wameanza kuzindua  rasmi na kuelezea mipango yao juu ya mchakato wa kumpata mwigizaji bora ambaye atakuwa akiigiza kama alivyo Hayati Steven Kanumba katika filamu ijulikano kama "MAISHA YA KANUMBA".


Uzinduzi  huo wa michakao ya kumpata mrithi bora wa Marehemu Steven Kanumba umefunguliwa leo katika idara ya  Habari ( Maelezo )Jijini Dar es salaam huku tukishuhudia baadhi ya viongozi wa kampuni hizo na wadhamini wa shindano hilo wakielezea adhima ya kufanya jambo hilo lenye manufaa kwa tasnia ya Filamu hapa Nchini

Akizungumza na WABUNIFUMEDIA , Mkurugenzi  wa kampuni ya simu  aina ya KZG , ambapo pia ni  wadhamini wakubwa wa  shindano hilo la kusaka vipaji maarufu kama " Kanumba Star Search" Raymond Kalikawe, amesema lengo la kampuni hizo mbili kuanzisha mradi huu wa kusaka vipaji ni kwa ajili ya kumpata mwakilishi bora atakayebeba uhusika wa aliyekuwa Nguli wa Filamu hapa Nchini na Afrika Mashariki na kati, hayati Steven Kanumba katika filamu ijulikanoyo kwa jina la " MAISHA YA KANUMBA"


Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya AM Arts Promotion, James Mwombeki amesema kuwa marehemu Kanumba alikuwa na mchango mkubwa katika kuitangaza nchi kimataifa pamoja na kuibua vipaji vya wasanii wa maigizo hivyo hatuna budi kumuenzi kwa kuiendeleza Sanaa ya uigizaji.

“Sisi kama AM Arts Promotion tumeamua kushirikiana kwa pamoja na Mama Kanumba kufanya shindano hili kwa nia ya kuendeleza tasnia ya filamu nchini kama vile marehemu Kanumba alivyokua akijitahidi kuwapa fursa ya uigizaji watu wa kila rika”, Alisema Mwombeki.

Naye, Msanii wa filamu, Mayasa Mrisho ,amewasisitiza wananchi kushiriki kwa wingi kwenye mashindano hayo kwani Sanaa ya uigizaji ni njia mojawapo ya kujipatia kipato na kuinua maisha ya mtu binafsi na Taifa kwa ujumla.


Hta hivyo , ameelezea juu ya mipango na zoezi zima la mchakato wa kumpata mwakilishi wa filamu hiyo, huku akisema kuwa zoezi hilo ni la Mikoa yote Tanzania lakini afafanua zaidi na kusema kuwa zoezi hilo la kumpata mwakilishi wao  litaanzia Kanda ya Ziwa kama heshima ya Marehemu Kanumba na baada ya hapo litaeleakea Nyanza za Pwani 

Kuhusu zawadi ya shindano hilo, Raymond ,amesema kuwa washiriki wote watakao jitokeza watapaitiwa zawadi ndogo ndogo ndogo huku washindi watakao patikana kaika kumtafuta mrithi wa Kanumba watapatiwa zawadi ya Simu kutoka kampuni hiyo.


Katika wawakilishi wa   hizo mbili, kwa upande wa Kampuni ya Kanumba  The Gret, mama mzazi wa Marehemu Kanumba ,Florence Mutegoa ,  atawakilisha akiwa kama mmoja wa Partner watakao simamia zoezi hilo la kumsaka mshiriki atakaye beba uhusika wa Steven Kanumba ambye alileta chachu kubwa ya maendeleo ya Tasnia ya Filamu hapa Nchini.

"Tunatambua thamani ya maigizo ndio sababu tumeamua kuanzisha shindano hili ili kuibua vipaji vilivyojificha, hivyo tunawakaribisha wananchi wote wenye uwezo wa kuigiza waje washiriki kwenye mashindano yetu pia tunaomba wadhamini kujitokeza zaidi ili watusaidie kufanikisha shindano hili”, Alisema Mutegoa.

Shindano hilo linatarajiwa kuanza mwezi Septemba mwaka huu, litaanzia Mikoa ya Kanda ya ziwa na baadae kuendelea katika Mikoa mingine.Washindi wataigiza filamu ya kumuenzi marehemu Kanumba itakayojulikana kama “Maisha ya Kanumba.


JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.wabunifumedia.blogspot.com ku-install App ya wabunifumedia,  bila ya kuingia websiteTweet@wabunifumediaonline, youtube@wabunifumediaonline TV, Fb@wabunifumediaonline, insta@wabunifumediaonline



Post a Comment

Theme images by Maliketh. Powered by Blogger.