Na Yusuph Mwamba
MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Uingereza na klabu ya soka ya Arsenal, Theo Walcott, amefunguka na kumtaka meneja wake kumbadilisha namba aliyokuwa nayo sasa na kumfanya kuwa winga huku akiamini ndio nafasi pekee anayoweza kutendea haki.

Licha ya kumaliza msimu wa 2015/2016 akiwa nafasi ya mshambuliaji, alifanikiwa kufumania nyavu mara 20 katika jumla ya michezo yote aliyocheza kunako klabu hiyo lakini kwa sasa ameona ni wakati wa yeye kutumika zaidi katika mashambulizi ya pembeni ili kuletea klabu yake ushindi.
"Nahitaji kucheza nafasi yangu ya kawaida ya winga wa kulia, kwa kuwa najua jinsi ya kuitendea haki na ndiyo iliyonifikisha hapa na kipindi nilipokuwa nacheza nafasi ya winga nilifanikiwa kufikisha jumla ya magoli 85 katika michezo 334 niliyoitumikia klabu yangu". Alisema Walcott
Moja ya changamoto atakazo kutana nazo Walcott, kama atacheza nafasi ya kulia basi ushindani wake utakuwa na wachezaji kama Alexis Sanchez, Alex Oxlade-Chamberlain na mchezaji wa akiba Alex Iwobi kwa nafasi ya winga .
Wakati huo Welcot ,akihitaji mabadiliko ya namba kutoka ushambuliaji hadi winga kocha wa Arsenal, arsene Wenger, bado hajasita na kukata tamaa ya kunyemelea saini ya mwanandinga wa klabu ya Lyon, Alexandre Lacazette katika kuimarisha safu yake ya ushambuliaji iliyokuwa ikiongozwa na Girou pamoja na Welcott.
JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.wabunifumedia.blogspot.com ku-install App ya wabunifumedia, bila ya kuingia websiteTweet@wabunifumediaonline, youtube@wabunifumediaonline TV, Fb@wabunifumediaonline, insta@wabunifumediaonline
Post a Comment