Halloween party ideas 2015
Image

Na Yusuph Mwamba

KLABU ya soka ya Everton, imesema kama Manchester City itakuwa inamuhitaji Nyota wao na mlinzi wa kati wa Kimataifa wa Uingereza, John Stones , basi watahitajika kutoa kiasi cha Poundi milioni 50 kama dili la uhamisho wake.
Aidha , inasemekana klabu hizo mbili zipo katika mawasiliano ili kukamilsha uhamisho wa nyota huyo, lakini chanzo chetu cha Sky sports kimesema mchakato huo unaonekana kuwa mgumu kutokana na bei walioitaja klabu ya Everton.


Licha ya Everton kutaka dau hilo, lakini maamuzi yote wanayo Man City kumchukua mchezaji huyo aua kuachana naye.
Wakati huo Everton wakisubiri maamuzi ya City, klabu hiyo bado inanyemelea saini ya nahodha wa klabu ya soka ya Swansea, Ashley Williams ili kuweza kuziba pengo la John Stone
Klabu ya Everton, kwa sasa ipo chini ya wamiliki wapya  huku benchi lao la ufundi likiongozwa na Meneja Ronald Koeman, ambaye ameweka mezani kiasi cha Poundi milioni 10 kunasa saini ya Williams kutoka Swansea City.

JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.wabunifumedia.blogspot.com ku-install App ya wabunifumedia,  bila ya kuingia websiteTweet@wabunifumediaonline, youtube@wabunifumediaonline TV, Fb@wabunifumediaonline, insta@wabunifumediaonline

Post a Comment

Theme images by Maliketh. Powered by Blogger.